Tanzania kwa jambo hili itanufaika

Tanzania kwa jambo hili itanufaika

mtaftaukweli1

Member
Joined
Sep 21, 2012
Posts
27
Reaction score
1
wadau amani iwe nanyi, tanzania inacho takiwa kufanya ili ijikwamue katika kuwa nyuma ki uchumi na tekinolojia ni kuwa na uelekeo na kufahamu taifa lina enda wapi, kwa kufahamu hilo hata hoja na tafiti mbali mbali za wataalamu zita zingatiwa,umebaki kuwa ni wimbo eti kipindi cha miaka ya uhuru wa inchi yetu ,kiuchumi hatukuwa mbali sana na baadhi ya nchi za bara la Asia,lakini bila kutafakari na walau hata kuiga yale mazuri yaliyo sababisha wakafika walipo tuna baki kulalamika kuanzia mtu wa juu hadi wa chini ,sasa huu sijui ni utaratibu wa na mna gani katika jamii yoyote? na uta badili na kubortesha yapi? tutafakari ,India wamefanikiwa kupiga hatu kubwa katika kujaribu kutokomeza maradhi maana wali jipanga na kuamua kuweka mikakati ya kuhakukisha wana pata wataalamu na vifaa bora katika tiba. leo tanzania tangu ipate uhuru zaidi ya miaka hamsini HAINA kitu ambacho inaweza kujivunia kwamba kimesimama vizuri, mfano MAJI serhemu nyigi mijini na vijijini hazina maji msafi, UMEME ndo unapatikana maeneo machache tu ya mijini,ELIMU kila mara kuna mabadiliko tangu ngazi ya chini hadi elimu ya juu,hakuna sera? AFYA , ni ajabu hospitali kama muhimbili ambayo ni ya Taifa kukosa vifaa bora vya tiba, tusikimblie india tuboreshe ya kwetu, hospitali za rufaa na ile ya taifa ziwezeshwe ili ziweze kutoa tiba BORA kwa watanzania wote na sio kutumia hospitali za india , sasa kinacho fanyika utafikiri india iko ndani ya jamhuri maana rufaqa zinazo toka mhimbili kwenda india ni nyingi ajabu kiasi kwamba baadhi ya wagonjwa hawaendi kutokana na kushindwa kumudu garama za usafiri na matibabu
Jamani suala sio kujisifu kuwa eti serikali ina jari viongozi wake kisa tu ina wapeleka india kwenye matibabu ,kwani kuna watanzania wangapi wana kufa kwa kushindwa kwenda kutibiwa india? tusomeshe vijana ambao watarudi kufanya kazi hapa nyumbani, napia tuwawezeshe kwa vifaa bora vya kufanyia kazi. naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom