Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Ndoto njema ya alinacha ya Tanzania kugeuka kuwa nchi ya Viwanda inazidi kustawi kwa Watanzania waliobakia usingizini. Maudhui ya ndoto ni mema kwani inaliwaza na kupumbaza na kutengeneza nafasi ya kupumua alau kusahau kwa muda shida zinazo ikabili Tanzania
Watanzania lazima tujiulize nani katika ngazi ya uongozi tuliokua nao anaeweza kutuvua kutoka hapo tulipo kufikia hiyo nchi ya kufikirika ya viwanda?Ikumbukwe kuwa katika hii safu ya uongozi asilimia zaidi ya 80% wanaotegemea nguvu za giza kuwaongoza wafanyayo na sio weledi au maarifa ya akili zao.
Nasema hivi kwa kukumbuka Viongozi hawa walipokuwa wanapigana vikumbo kukimbilia "Loliondo - Mji wa wajinga ndio waliwao" kwa "babu" kugombea kupata kunywa kikombe cha tope za mizizi tena kwa kwa kulipia! Wengine walikimbia bunge, wengine kukodi ndege, na wengine kudiriki kutumia madaraka yao vibaya kwa kutumia fedha za walipa kodi kutengeneza miundombinu ya barabara na vikosi vya dola kuhakikisha " usalama" unakuwepo na " waliwao" wengi wamfikie BABU.
"Babu" ni mtu mwenye elimu isiyokadirika ( semi illiterate) na fikira pevu, hivyo aliweza,kuwalaghai, kuwapumbaza, na hata kuwadumaza akili viongozi(ubongo wa Taifa) kwa kuwapa kikombe kilichojaa tope za mizizi na kunywa huku wa kikigombaniana na kuridhika. Inashangazana lakini pia ni aibu tena hasa kwenye karne hii.Kutokana na kituko hiki nashindwa kumuona kiongozi ambae atakuwa mbunifu na weledi wa kujenga hoja za ushawishi kwa wawekezaji kutuvusha salama kutoka daraja hii kwnda daraja nyengine ya Viwanda.
Tunajidangnganya , tunahitaji miaka 50 ya kuwekeza kwenye Elimu kwanza, tuondokane na viongozi wenye fikira potofu za giza. Elimu,Elimu,Elimu,Elimu