Siungi mkono Tanzania kushiriki katika michezo ya kimataifa hata kidogo.Maana kila tukishiriki tunatolewa katika hatua za mwanzo na kila siku tunaambiwa mandalizi mabovu,mimpira wamiguu kwa wanawake au wanaume,kikapu,riadha,baiskeli yani kwa miaka hamsini tumeshindwa hata kujikita katika aina moja ya mchezo tunaoweza jani?mimi siamini kama hatuna wanamichezo wanaoweza bali ni ubinafsi,siasa, rushwa na upendeleo.Sikuona sababu ya Tz kushiriki mchezo wa olimpic unaondelea kwasasa jijini London sababu viongozi walijua fika hawakuwa na mandalizi yakutosha na wanajua hawatapata medali hata moja lakini bado walitamani kwenda kufanya ziara tuu,Mimi ni mtanzania na mpenda michezo ila siungi mkono Tanzania kushiriki michezo ya kimataifa. mara ya mwisho kuchukua medali olimpic ni 1980 tena mbili tuu aubu kwa wadau wa michezo narudia kusema aibu, world cup ndiyo kabisaa hakuna matumaini labda tubakie kujivunia Kagame Cup