Tanzania kununua Ndege nyingine mpya Mwezi Julai Mwaka Huu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Serikali iko kwenye mpango wa kuongeza ndege nyingine moja ili zizidi kufika sehemu nyingi zaidi Tanzania ambapo Naibu Waziri wa wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amesema July 2017 ndio inanunuliwa nyingine.

Amesema Ndege hiyo itakayonunuliwa July ni aina ya Dash 8-Q 400 ambapo hatua hiyo italifanya shirika la ATCL kufikisha Ndege nne (4) ambazo zitaongeza safari zake kwa kuhudumia masoko yake ya ndani na miji ya Nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Ni kauli ambayo aliitoa wakati wa uzinduzi wa safari za Ndege za ATCL kwenye mkoa Tabora na kuongezea kwamba lengo la Serikali ni kuhakikisha hadi kufikia July 2018 Shirika la Ndege Tanzania liwe linamiliki Ndege sita zenye uwezo wa kubeba abiria kwa kiwango tofauti tofauti na kusafiri mikoa mingi na nje ya Tanzania.

Naibu Waziri alisema hadi sasa Serikali imeshanunua ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na hatua inayofuata ni ununuzi wa ndege nyingine tatu aina ya Bombardier Dash 8-Q400 yenye uwezo kubeba abiria 76, CS 300 mbili zitakazobeba abiria 132 kila moja na Boeing 787 ya kubeba abiria 262.

Alisema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege hapa nchini na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege katika mikoa ambayo haina viwanja hivyo kwa sasa ili ifike siku mikoa yote Tanzania iweze kuunganishwa na usafiri wa anga

Chanzo: Mpekuzi
 
Kila la heri kwa jambo jema la kimaendeleo. Ila wawe na transparency kuondoa maneno yanayozagaa kama yalivyo kwa ndege za sasa.
 
Kila wakati sherehe za uzinduzi, wakizindua mara moja si inatosha, naona kama ni matumizi mabaya ya resources,
 
hospital hazina madawa ndege za nini?
Ni wazo zuri serikali maskini kama ya Tanzania kuwa na ndege zake lakini sio kipaumbele kwa wakati huu mgumu.
kwani JPM hana washauri wa uchumi?
wenzake waliomtangulia walitumia ushauri wa wataalamu wao ndio imetufikisha hapa kama taifa.
huku ni kukurupuka tu huwezi mtu mwenye akili timamu unakopa ili kununua ndege wakati huduma za kijamii hasa afya,chakula,elimu,nk ni adimu au hazipatikani kabisa kwa wananchi wa kawaida.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Hata mkiwekewa dawa bure bado hamtaridhika na mtakuja na usemi mwngine wauguzi wana nyanyasa wagonjwa kisa ni bure,,so hakuna jema kwenu,
 
Kuwe na business plan kwenye hii sekta..

Airline business ni ngumu na has a lot of complexity..

Ku secure route sio kitu cha mchezo..

Kenya Airways wamepaki baadhi ya ndege zao hivi sasa kwasababu hazina routes..

Asifikiri kununua mindege tu ndio sifa.

Lazima uwe na plan.. Lazima uwe na focus.

Kwa mfano strategy ingekuwa kuhakikisha ATCL ina win route zote za ndani.. Na hii ni kwa kuboresha huduma zao ikiwamo kuwa na competitive fare rates uki compare to Fast Jet na Precision Air...affordable fare rates.

Then ndio tuanze pole pole ku secure routes za neighbouring countries/ East Africa region etc.pole pole mpaka tufike route za mbali huko duniani.
 
hospital hazina madawa ndege za nini?
Ni wazo zuri serikali maskini kama ya Tanzania kuwa na ndege zake lakini sio kipaumbele kwa wakati huu mgumu.
kwani JPM hana washauri wa uchumi?
wenzake waliomtangulia walitumia ushauri wa wataalamu wao ndio imetufikisha hapa kama taifa.
huku ni kukurupuka tu huwezi mtu mwenye akili timamu unakopa ili kununua ndege wakati huduma za kijamii hasa afya,chakula,elimu,nk ni adimu au hazipatikani kabisa kwa wananchi wa kawaida.
Binadamu ana hulka ya kutoridhika. Hilo halina ubishi, ndio maana leo hii unaandika kuwa dawa hakuna, elimu mbovu, miundombinu ni mibovu etc.

Lakini approach ya serikali ni nzuri, kukiwa na transparency hizo ndege zitaleta faida na kuwanunulia wananchi dawa, kuboresha elimu na afya, miundombinu nk.

Sio kila kitu tupinge tu, tunahitaji kuwa na image ya taifa, ni aibu nchi kubwa kama Tanzania haina ndege zake.
 
huyu mzee upara tushamuambia aachane na huu ununuzi wa MAGUTA lakini hasikii,ndio maana umeshauriwa utembee tembee huko nje labda utajifunza kitu
 
hospital hazina madawa ndege za nini?
Ni wazo zuri serikali maskini kama ya Tanzania kuwa na ndege zake lakini sio kipaumbele kwa wakati huu mgumu.
kwani JPM hana washauri wa uchumi?
wenzake waliomtangulia walitumia ushauri wa wataalamu wao ndio imetufikisha hapa kama taifa.
huku ni kukurupuka tu huwezi mtu mwenye akili timamu unakopa ili kununua ndege wakati huduma za kijamii hasa afya,chakula,elimu,nk ni adimu au hazipatikani kabisa kwa wananchi wa kawaida.
Kasome IRANI YA CCM 2015-2020 ili ujue kuwa ndege ni kipaumbele au hapana. Siyo mnakurupuka kuandika mambo ambayo hamna uhakika nayo!
 
YAHERI MUNGU: Kwa hiyo 'IRANI' ya CCM 2015-2020 ni ndege za Bombadier na siyo afya, chakula na elimu. Hivi inaitwa IRANI au ILANI? Kweli CCM inapendwa na watu wenye elimu mgogoro, a.k.a mbumbumbu
 
hospital hazina madawa ndege za nini?
Ni wazo zuri serikali maskini kama ya Tanzania kuwa na ndege zake lakini sio kipaumbele kwa wakati huu mgumu.
kwani JPM hana washauri wa uchumi?
wenzake waliomtangulia walitumia ushauri wa wataalamu wao ndio imetufikisha hapa kama taifa.
huku ni kukurupuka tu huwezi mtu mwenye akili timamu unakopa ili kununua ndege wakati huduma za kijamii hasa afya,chakula,elimu,nk ni adimu au hazipatikani kabisa kwa wananchi wa kawaida.
Unapaswa kujua kuwa pesa ya kununua ndege siyo inayopelekwa kugharimia elimu, afya wala chakula. Ukiangalia kwa jicho la kitaalam utaona kuwa wananchi wana uwezo wa kugharimia elimu, afya (public health preventive measures) na chakula, isipokuwa ndege. Kwa hiyo uamuzi wa serikali Ni sahihi. Mikoa ambaya haikuwahi kuwa na flights (matharani Ruvuma) sasa ndege zinatua na kuruka huko.
 
Back
Top Bottom