Tanzania kunufaika na Dola Bilioni 60 za China sekta ya Nishati

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
CHINA 1.jpg


Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imeitaja nchi ya Tanzania kuwa na nafasi kubwa ya kunufaika na fedha kiasi cha Dola Bilioni 60 kupitia uwekezaji sekta ya nishati, fedha zilizoahidiwa kutolewa na nchi hiyo wakati wa Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Ushirikiano baina ya China na Afrika, uliofanyika nchini Afrika Kusini mwezi Desemba,2015.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing na ujumbe wake alipokutana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, China ina imani kubwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyosimamia masuala mbalimbali nchini, pia Profesa Sospeter Muhongo kutokana na namna anavyoisimamia sekta ya Nishati na Madini.

Miongoni mwa Sekta zinazopewa kipaumbele katika fedha hizo ni pamoja na pamoja na miundombinu, afya, biashara, uwekezaji na kupunguza umaskini, barani Afrika.

Kutokana na mahusiano mazuri ambayo yamekuwepo kwa miongo kadhaa baina ya nchi hizo mbili, Balozi Youqing amemwakikishia Waziri Muhongo kuwa, China itaendeleza ushirikiano huo kwa kuhakikisha inazishawishi kampuni kubwa na zilizobobea kitaalamu na kiteknolojia za China, ili ziweze kushirikiana na Tanzania katika sekta ya nishati, na zaidi katika uzalishaji umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe kutokana na namna ambavyo Wizara inavyokipa kipaumbele chanzo hicho kuzalisha umeme nchini.

Wakati huo huo, China imesema itaendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi Watanzania kusoma masuala ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali nchini humo kutokana na umuhimu wa sekta hiyo na kwamba, China inapenda Tanzania ifanikiwe katika kuzalisha wataalam wa kutosha katika fani hizo na kuongeza kuwa, anatambua juhudi zinazofanywa na Waziri Muhongo kuhakikisha wanafunzi wengi wa kitanzania wanapata fursa ya kusoma masuala ya mafuta na gesi maeneo mbalimbali Duniani, ikiwemo China.
 
Prof.Muhongo tafadhali saidia Tanzania tuweze nufahika na sector hiyo maana wewe ni fani yako uliyobobea kwa hiyo Watanzania tunaimani na wewe katika maswala hayo ya nishati.
 
Inasikitisha sana kuona wahisani wakimwaga mabilioni ya dola ktk mradi ambayo inawahakikishia wao faida kubwa huko mbeleni na sisi Waafrika tunaona ndiyo misaada ya maana kweli....hakuna mradi mzuri ambao unahitaji uwekezaji mkubwa wa pesa kama elimu. Tunahitaji kuelekeza mabilioni ya dola ktk elimu.Inauma kuona kuna baadhi ya shule za secondary zinapokea shilingi milioni moja na laki sita kila mwezi.halafu ndo tunafikiria kuwa nchi ya viwanda?na hata hiyo sekta ya mafuta sijui tutafaidika nayo vipi kama elimu hatuipi umuhimu unaostahili.
 
Lakini kufundishwa kuzalisha ili uchumi wetu usiwe tengemezi nalo neno. Tukizalisha gesi na mafuta tukauza fedha hizo zitatumika kwenye elimu na mambo mengine ya maendeleo. Kufudishwa ili uweze kujitegemea ni vyema.
 
Lakini kufundishwa kuzalisha ili uchumi wetu usiwe tengemezi nalo neno. Tukizalisha gesi na mafuta tukauza fedha hizo zitatumika kwenye elimu na mambo mengine ya maendeleo. Kufudishwa ili uweze kujitegemea ni vyema.
 
Back
Top Bottom