Tanzania kuna wazalendo halisi na pia kuna majambazi


Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
5,163
Points
2,000
Age
66
Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
5,163 2,000
Katika utawala wa Mwl Nyerere kulikuwa na kipindi asubuhi kwenye Radio Tanzania kwamba ''Ulinzi na usalama wa Tanzania ni wa Watanzania wenyewe, kila Mtanzania, kila mzalendo na kila njamaa!

Hiyo slogan ilijenga taifa hili tangu mwanzo kwenye vichwa vyetu tulielewa hivyo!! Sasa kumeibuka watu ambao wamekaa kwenye madaraka makubwa kyenye nchii hii wala hawajali usalama wa nchi hii nikimaanaisha uchumi na mali zetu!! Watu wakubwa wameamua kugeka mafisadi kuhujumu uchumi wa nchi bila woga wala huruma!!! Mtu mkubwa meli zake zinakamatwa na pembe za ndovu anakataa kuwa si zake bila kuchukua hatua yoyote ya kuokoa nyara za taifa hili, wenzake wanamwangalia tuu, wanazidi kumwongezea madaraka, je huo ni uzalendo???

Mtu mkubwa tuu anaingiza nchi kwenye mikataba mibovu inayofilisi nchi hadi sasa tuna madeni makubwa yanatakiwa kulipwa DOWANS, RICHIMOND anayelipwa wala hajulikani, je huo ni uzalendo???? Wapo watu kwenye kambi hizo hizo wanaojitahidi kuokoa taifa na mali zake, wanasukiwa zengwe hata la kupewa sumu wauwawe, wanapigwa vita za ajabu, lakini kwa uzalenda wao wanatumikia taifa kwa uaminifu!! Wanafufua reli iliyokufa ya Mwanza, ndugu zangu kand aya ziwa wanajua umuhimu wa reli kwetu huko!! Reli hadi Ubungo to City Center, imekuja sasa Fast Jet nauli mchekechea!! Bandarini bado hujuma anafanyiwa huyo mtu lakini hakati tamaa ni mzalendo!!

Mhe Kagasheki, Mhe Nyarandu, Mhe Prof Muhongo, Mhe Maghufuli pamoja na mapungufu yake lakini anajitahidi!! Hao ni wazalendo wachache wanaopigana kwenye giza la ufisadi lililo gubika taifa hili tajiri lenye jina la umaskini!!! Kwanini Watanzani wazalendo wenye uchungu na nchi maana ni nchiyetu hatuna pa kwenda, tuchukue hatua zipi za maana kuwaondoa hao mafisadi na wahujumu uchumi wa nchi hiii???

Nchi inaachwa mashimo, mali za asili zinakwisha, hawana huruma na misitu wala tembo zetu, wanatuchekea lakini ni wauwaji!!! Je tuwaangalie huku taifa linadidimia tuu na kufilisika???Nimeepuka kataja chama chochote maana Tanzania ni yetu woote bila kujali tupo chama gani!!!
 

Forum statistics

Threads 1,283,903
Members 493,869
Posts 30,805,564
Top