Tanzania kuilipa CAF kuwa mwenyeji wa AFCON 2027, ni utaratibu wa kawaida kikanuni, Kenya na Uganda nao wamefanya hivyo

Tanzania kuilipa CAF kuwa mwenyeji wa AFCON 2027, ni utaratibu wa kawaida kikanuni, Kenya na Uganda nao wamefanya hivyo

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Kwa mujibu wa kanuni na mikataba ya uenyeji ya CAF, nchi inayopata nafasi ya kuandaa AFCON hulazimika kusaini makubaliano ya uenyeji yanayojumuisha majukumu mbalimbali ya kifedha. Miongoni mwa masharti hayo ni kulipa kile kinachoitwa “hosting” au “commitment fee”, ambacho ni ada ya makubaliano inayothibitisha kuwa nchi husika imejitolea kugharamia maandalizi ya mashindano hayo.

Kwa mfano, katika maandalizi ya AFCON 2027, kila nchi mwenyeji anapaswa kuchangia takribani dola milioni 30 za Marekani kwa CAF kama sehemu ya makubaliano ya uenyeji. Mfano mzuri kama kilichofanyika na Tanzania imetoa Tsh. Bilioni 82 Hata hivyo, kwa upande wa Kenya Kenya imepanga kulipa karibu KSh 3.9 bilioni na Uganda Shs112.407Bilioni

Soma habari hizi pia:
Uganda To Pay CAF Shs112bn To Co-Host 2027 AFCON » Business Focus

Wataalamu wa michezo wanaeleza kuwa ada hiyo si malipo ya kununua mashindano, bali ni sehemu ya utaratibu wa kiutawala na kifedha wa kuendesha mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Soma Pia: Makonda: Serikali imelipa CAF Tsh. Bilioni 82, Tanzania kuwa mwenyeji wa AFCON 2027

Mbali na ada hiyo, nchi mwenyeji pia hutakiwa kugharamia maandalizi makubwa ikiwemo ujenzi au ukarabati wa viwanja vya kisasa, kuboresha miundombinu kama barabara na viwanja vya ndege, pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa hoteli, usalama na huduma nyingine muhimu kwa timu na wageni watakaoshiriki mashindano hayo.

Kwa mujibu wa CAF, masharti hayo yamewekwa ili kuhakikisha nchi mwenyeji ina uwezo wa kifedha na kiutendaji wa kuandaa mashindano kwa kiwango cha kimataifa, pamoja na kuzuia changamoto zilizowahi kujitokeza hapo awali ambapo baadhi ya nchi zilishindwa kukamilisha maandalizi yao kwa wakati.

Hivyo basi, ingawa Tanzania na washirika wake wamelipa ada hiyo kama sehemu ya makubaliano ya uenyeji, wataalamu wanasema hatua hiyo haimaanishi kuwa nchi imenunua uenyeji wa AFCON, bali ni sehemu ya masharti rasmi ya CAF kwa nchi zote zinazopata fursa ya kuandaa mashindano hayo.
 
Kwa mujibu wa CAF, masharti hayo yamewekwa ili kuhakikisha nchi mwenyeji ina uwezo wa kifedha na kiutendaji wa kuandaa mashindano kwa kiwango cha kimataifa, pamoja na kuzuia changamoto zilizowahi kujitokeza hapo awali ambapo baadhi ya nchi zilishindwa kukamilisha maandalizi yao kwa wakati.

IKiwa nchi moja inaandaa hayo mashindano kama ilivyokuwa kwa Morocco, ina maana watalipa mpunga wa jumla kama ulivyotolewa na nchi zote tatu za EAC?
 
Watu wanauliza nchi inanufaikaje na hayo mashindano? Mpo serious kweli nyie watu?
Yooote hayo yatakuwa na faida gani kwa nchi masikini kama Tanzania,
Sina uelewa naomba kufahamishwa 🙏


USA, Canada na Mexico wanafaidika vp Na kuandaa kombe la dunia?

Em tujifunze kuacha kulalamika kwenye kila jambo.
 
Back
Top Bottom