Tanzania kugundua chanjo ya UKIMWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kugundua chanjo ya UKIMWI

Discussion in 'JF Doctor' started by Nzowa Godat, Dec 3, 2011.

 1. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Leon Bahati, Moshi

  WANASAYANSI wa Tanzania wameandika historia mpya ya kipekee duniani, baada ya kufanikisha utafiti utakaowezesha upatikanaji wa chanjo na tiba ya Ukimwi.Utafiti huo umeshangaza Ulimwengu baada ya wanasayansi hao kueleza kuwa wapo baadhi ya watu waliobainika kushambuliwa na Virusi vya Ukimwi (VVU), kwa muda fulani na baadaye kujijengea wenyewe kinga inayoweza kudhibiti virusi hivyo na kuwa na afya njema bila kuwa na haja ya kutumia dawa tena.

  Wataalamu hao wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, ambao walifanikisha utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 2006 na 2010, waliliambia Mwananchi jana kuwa kinachofanyika ni kutengeneza chanjo itakayowezesha watu wote kuwa na kinga hizo, hivyo kutoathirika na VVU.

  Kiongozi wa Ushirikiano wa kiutafiti kati ya KCMC na Chuo Kikuu cha Afya cha Duke cha nchini Marekani, Dk Elizabeth Reddy alisema jambo la msingi katika utafiti huo ni kugundulika kwa VVU kuwa wana gamba lenye protini iliyochanganyika na sukari, ambayo huvifanya kushindwa kutambuliwa na kinga za kawaida za mwili wa binadamu.

  Lakini, Dk Reddy alisema kuwa katika ugunduzi wao, wamebaini aina ya kinga za mwili ambazo hutambua virusi kupitia aina hiyo ya sukari kwenye gamba la nje la VVU na kuvishambulia hadi kuviua.

  Alisema kuwa utafiti huo ulifanyika katika Maabara ya KCMC kwa ushirikiano wa timu ya wataalamu wa afya wa Tanzania pamoja na wa Marekani.Alibainisha kuwa utafiti huo ulihusisha Watanzania kadhaa walioambukizwa VVU hapa nchini, lakini wamekuwa wakiishi bila kuathirika.

  Dk Reddy alisema kuwa utafiti huo umefanyika maeneo mengi duniani, lakini kituo cha KCMC ndicho kilichotoa mwanga mkubwa ambao hatua zake za mwisho zilithibitishwa na wataalamu waliobobea nchini Marekani.

  Kiongozi huyo wa utafiti, alisema kuwa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa inayosimamiwa na Mfuko wa Good Samaritani (GSF) ambao ndio pia unaosimamia taasisi nyingine kama vile Chuo Kikuu cha Afya cha Tumaini na Hospitali ya KCMC, ndiyo inayopaswa kupewa shukurani kwa matokeo hayo.

  Mkuu wa jopo la utafiti huo, Profesa Peter Kwong wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (NIAID), amesifu utafiti huo akisema kuwa umeonyesha mwanga kwa wanasayansi kupata njia rahisi ya kugundua chanjo ya Ukimwi.

  Profesa Kwong alisema katika dunia wamekuwepo watu wanaoambukizwa VVU, lakini wao wenyewe hawaonekani kuathirika.Alisema kuwa ugunduzi huo pia umetoa mwanga kwa wanasayansi wengine duniani wanaofanya utafiti wa dawa nyingine za chanjo na tiba ya Ukimwi.

  Mchunguzi huyo nguli katika baiolojia ya chembe za urithi za mwili wa binadamu, alisema utafiti huo umebaini pia kwamba kuna baadhi ya watu ambao baada ya kuambukizwa VVU na kuishi navyo kwa miaka kadhaa, hujikuta wanajijengea kinga.

  Akielezea kuhusu kinga hiyo, Profesa Kwong alisema kuwa huwafanya watu hao kuwa tofauti na wengine ambao baada ya kuambukizwa VVU, mfumo wao wa kinga huathirika na kujikuta CD4 zao zikipungua siku hadi siku.

  Alieleza kuwa kupungua huko kwa kinga ndiko kunakosababisha muathirika kushambuliwa kirahisi na magonjwa mengine na asipotumia dawa za kurefusha maisha, hukonda hadi kufa.

  Jinsi utafiti ulivyofanyika
  Dk Reddy anasema walifanya kazi kubwa ya kutafuta watu walioambukizwa VVU lakini hawaathiriki na huweza kuishi kwa muda mrefu wakiwa na afya njema."Tulichukua damu zao tukaziainisha chembechembe zote zilizomo kupitia maabara zetu…: Tuligundua wana chembechembe kinga za ziada," alisema Reddy.

  Alisema kuwa kimsingi binadamu yeyote anapoambukizwa VVU hutengeneza kinga za kushambulia VVU.Alibainisha kuwa pamoja na hali hiyo, lakini kwa bahati mbaya kinga nyingi zinazotengenezwa huwa hafifu katika kukabili VVU aliosema, wana kawaida ya kujibadilisha.

  "Hali hiyo huifanya kinga ya mwili iliyotengenezwa kushindwa kukabiliana na virusi. Kwa kawaida kinga hizi huwa hafifu…; Baadhi ya vipimo vya VVU ni vile ambavyo hutambua uwepo wa virusi hawa kwa kuangalia uwepo wa kinga hizi kwenye damu," alisema Dk Reddy.

  Alisema kuwa baadhi ya watu ambao huweza kutengeneza kinga imara, ndiyo ambao huonekana kuwa na virusi vichache, lakini huwa haviwezi kumuathiri kiafya muhusika.Alipoulizwa kama watu hao ndio ambao huzungumziwa mitaani kuwa wana virusi visivyooneka kuwaathiri lakini huweza kuwaambukiza watu wengi, Dk Reddy alisema "hapana!"

  Alieleza kuwa watu hali ya waliobainika kuwa na VVU lakini haviwaathiri hutokana na kinga yao na kwamba walibaini hata uwezo wa kuambukiza wengine ni mdogo."Inatokana na ukweli kwamba wanakuwa na idadi ndogo ya virusi katika miili yao kwa sababu chembechembe kinga walizo nazo huviua virusi," alisema.

  Alisema VVU vinadhibitiwa na chembechembe hizo za kinga hivyo hushindwa kupata fursa ya kushambulia CD4 za mwili ili kuzaliana.

  Alidokeza kuwa mazingira hayo ndiyo yanayosababisha baadhi ya wanandoa, mmoja kukutwa ameathirika na mwingine kuendelea kuwa na afya njema, ingawa ameambukizwa.Kuhusu sababu za baadhi ya watu kuwa na uwezo huo, Dk Reddy alisema kisayansi bado wanaendelea na utafiti.

  Sifa kwa Tanzania
  Dk Reddy alisema ugunduzi huo unawapa akili ya kutafuta namna ya kutengeneza chanjo itakayowezesha binadamu wote kuwa na chembechembe hizo kinga.Alisema kwa kiwango cha chini watahitaji miaka mitano kuweza kufanikisha upatikanaji wa chanjo hiyo.

  Dk Reddy alisema kitendo cha wataalamu wa Tanzania kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha ugunduzi huo, kutalifanya taifa lipewe kipaumbele katika kutumia chanjo hiyo.Alisema kuwa chanjo hiyo itaweza kuwasaidia watu ambao bado hawajaathirika kwa kuwatengenezea kinga ambayo pia itaweza kuwa tiba kwa wale walioathirika.

  "Wakati wote tunapotafuta chanjo, tunajitahidi pia kutafuta tiba," alisema Dk Reddy akisema upo uwezekano mkubwa wa kupata tiba pamoja na chanjo.Alisema muoainisho wa chembechembe hizo kinga, ulifanywa na maabara za Kimarekani kwa kuwa Tanzania haina mashine zenye uwezo huo wa juu katika kuchunguza virusi kwa undani.

  Ugunduzi wa kuwa VVU wana gamba lenye sukari linalowafanyia kinga ya kutogundulika kuwa ni adui ndani ya mwili wa binadamu, iliainishwa na wataalamu nchini Marekani.

  Kuhusu mpango wa kutengeneza chanjo hiyo, nguli huyo alisema utafanyika nchini Marekani, lakini KCMC itakuwa moja ya vituo vya kuendeleza utafiti huo duniani hadi kupatikana kwa chanjo kamili.

  Baadhi ya wataalamu wa Tanzania waliohusika katika utafiti huo ni Profesa Noel Sam, Profesa Saidi Kapiga na Sarah Chiduo.Wanasayansi wengine walioshiriki kwenye utafiti huo kutoka nje ya nchi ni Profesa John Bartlelt na Profesa John Crump.

   
 2. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Good news, ila bado inabidi tuedelee kujikinga kwa njia zetu tunazotumia kila siku.
  Maana kauli ya NOT LESS THAN 5 YRS si mchezo tuanweza tukawa tumepungua sana.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ni Wa TZ au Wa marekani? ukisoma utaona msemaji sana Ni DK wa Maerkani sasa ni collaboration au? Heading inanichanganya
   
 4. i411

  i411 JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Hatujaa zoea kusikiafa habari za ubunifuu Leo hii katika gazeti la mwananchi kuna stori wataalam kcmc wamekamilisha matokeo Yao na watu wamepona na wanasayansi wengine wameaminia. Lakini utafiti na wagonjwa wao wenye vvu nazani wamefanya mda mchache tokea 2006 mpaka 2010 ......
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  ile ya muhimbili waliowachanja ma askari polisi 100 imefikia wapi?
   
 6. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  wameshaanza kutumia ARV
   
 7. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Again!?
   
 8. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ahahahahaaaah!
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Kwanini watumie ARV?!, hunahabari kuwa majaribio yalifanywa kwa placebo?, je, placebo inaweza kuwapo UKIMWI?, wanchekesha.
   
 10. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Sio heading pekee inayochanganya...ona...
  Leon Bahati, Moshi
  WANASAYANSI wa Tanzania
  wameandika historia mpya ya
  kipekee duniani, baada ya
  kufanikisha utafiti
  utakaowezesha upatikanaji wa
  chanjo na tiba ya
  Ukimwi.Utafiti huo
  umeshangaza Ulimwengu
  baada ya wanasayansi hao
  kueleza kuwa wapo baadhi ya
  watu waliobainika
  kushambuliwa na Virusi vya
  Ukimwi (VVU), kwa muda
  fulani na baadaye kujijengea
   
 11. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,646
  Trophy Points: 280
  hizi habari ndio zile za gazeti la mwananchi zilizowahi kusema dawa ya ukimwi imepatikana.waandishi wetu utata mtupu.
   
 12. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Majaribio ya magamba bwana...
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,663
  Trophy Points: 280
  Hiyo chanjo ikoje ikoje vile?au wamegundua kondom za kumeza?
   
 14. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  unaishi wapi? ktk mambo ya aibu yaliyoikumba Tanganyika ktk miaka 50 ya uhuru hili lipo top 10. Matokeo ya njanjo yapo hewani muda mrefu sana na imebaki kuwa ni siri na aibu ya govt. Well sijui govt imefikia wapi kuwalipa fidia waathirika mpaka sasa. Am stand to be correct.

  my take: Kama tungekuwa na utamaduni wa kuwasikiliza wataalam haya yote leo hii yasingetukuta ndugu, warning zilishatolewa na wataalam lkn ubabe wa wenye nchi ukatumika kuukingia kifua utafiti ufanyike na sasa waliopinga wamebaki wanachekelea ushindi dhidi ya wababe
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Well done Tanzanian Scientists...

  Well done... It can be done ... and if successful the Country will make a lot of $$
   
 16. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kazi njema yenye heri katika ardhi yenye dhahabu na almas ambayo viongozi wake wameshindwa kuwaongoza watu kufikia mafanikio ya kiwango cha juu cha kupigiwa mfano kwa nchi za Kiafrika.
   
 17. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kumbe virusi vina gamba kama ccm! Duh sikulijua hilo
   
 18. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Babu wa Loliondo oyeeeeee!
   
 19. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  haha ha ha ha ha ha ha haaaaaaa!Tunaweza kugundua tiba na kinga ya ngoma (UKIMWI) alafu tukabaki vilevile kama hatukuwepo!
   
 20. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ...Ila Tiba Ya Malaria Ipo Lakini Bado Raia Wanafariki...So Hata Ikipatikana hy Ya Ukimwi Sijui Ndo Itakuwaje...But ni Good Step
   
Loading...