Tanzania kufungua ubalozi wake nchini Qatar

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410

Balozi%20wa%20Qatar%20Magufuli.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 16 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi.

Pamoja na kutangaza kuufungua Ubalozi wake nchini Qatar Dkt. Magufuli amemuomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Qatar kwamba zipo fursa nyingi za ushirikiano zinayoweza kufanyiwa kazi, huku akibainisha uwepo wa gesi asilia zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 na mpango wa kufufua shirika la ndege la taifa (ATCL).

"Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" Amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi amemshukuru Rais Magufuli kwa nia yake ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano na nchi hiyo, na amemuahidi kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar na Jumuiya ya wafanyabiashara wa nchi hiyo ili waje kuwekeza Tanzania.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Makinda amesema mazungumzo yao yameuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kwamba amemhakikishia kuwa amejipanga kuhakikisha mfuko huo uliobeba matumaini ya huduma za matibabu ya watanzania unaboreshwa zaidi na dosari zinazolalamikiwa na wanachama zinafanyiwa kazi

Chanzo: EATV
 
Muna mpango wa kurejesha Watz 500,000 Kutoka katika moja ya nchi ya Qatar na bado munawaza kufungua Ubalozi utakuwa na faida gani? Balozi zetu mahsusi zinatakiwa zisaidie Watz walioko nje ya nchi kama hakuna Watz kazi yake asubiriwe muarabu kuja Tz miaka 10 kwa watu 2 ni ufujaji wa kodi.
 
Kama kumbux2 zangu ziko sahihi, nchi hii ya Qatar ilihusika na utoroshwaji wa twiga na wanyama wetu wengine kwa kutumia ndege ya kijeshi, leo inakuwaje tunawakaribisha kiulaini hivi bila ya kuwapa kwanza sharti la kurejesha viumbe waliotupora?
Kiungwana, Balozi huyo wa Qatar walau angeonyesha kukerwa na kitendo kile japo kwa kuomba msamaha wa kinafiki, lkn, duh!
Haijakaa vizuri hii!
 
Back
Top Bottom