Tanzania kerosine consumers association | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kerosine consumers association

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rimbocho, Jun 30, 2011.

 1. r

  rimbocho Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzania kerosine/parafine consumers association
  tangazo kwa umma

  yah: kukataa uamuzi uliotolewa na ewura wa kupandisha bei ya mafuta ya taa.

  ndugu wananchi chama cha watumiaji mafuta ya taa kina jumla ya wanachama 36,000,000 tanzania nzima. Toka kianzishwe mwaka 1920 hapa tanganyika hakija pata usajili wa kudumu hii ikiwa ni kutokana na kutokuwajibika kwa viongozi wetu wanaosajili vyama hivi vya kijamii.

  Kwa ujumla wetu tumesikitishwa sana na hoja hii ya kupandisha bei ya mafuta ya taa bila sisi watumiaji kuhusishwa kwani katika vikao vya ewura wanshiriki watumiaji wa dieseli na petroli pamoja na wauzaji wa mafuta.

  Kwa takwimu tulizo nazo inaonyesha kabisa uchakachuaji wa mafuta haupo katika dieseli na petroli peke yake bali pia katika mafuta ya taa, kwani miaka ya nyuma kuliwahi kuripotiwa matukio kadhaa ya wanachama wetu kupoteza maisha na mali zao kutokana na kutumia mafuta ya taa yaliyo changanywa na petroli hivyo kulipuka na kuleta madhara hayo. Hivyo kwa kuongeza bei ya mafuta ya taa wanachama wetu wengi watapoteza maisha na mali zao.

  Je ewura walizingatia vigezo vipi kabla ya kupandisha bei ya mafuta ya taa? Au kwa sababu chama chetu hakijasaliliwa ndio maana hakisikilizwi?

  Katika kipindi hiki cha mgao wa umeme usio na kikomo tunategemea kupata wanachama wengi zaidi, je hizi si hujuma za ewura kuwaogopesha wanachama wetu ili wasijiunge kwa wingi?

  imetolewa na mwenyekiti wa kudumu
   
Loading...