Tanzania izuie uingizwaji wa maziwa ya Kenya

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
63,466
88,825
Kenya Kuzuia Gesi ya Tanzania: Tanzania ichukue hatua dhidi ya Kenya

Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo. Tamko la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya linasema ' ndani ya siku 7 kuanzia juzi tarehe 24 Aprili 2017, itakuwa ni marufuku Kwa Kenya kuagiza Gesi ya kupikia kutoka Tanzania '. Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.

Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa.

Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.

Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.

Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania. Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.

Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo Kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma mjini
26/4/2017
 
Majamaa wa kulialia. Alafu bado utasikia mtu akikwambia Tanzania haitaji Kenya vile Kenya inahitaji Tanzania. Hahaha!!
 
Msipotezee muda na Kenya.. As long as hiyo mitungi ni cheap I guarantee you itawafikia wakenya tu.
 
Wakenya nao ni washenzi muda mwingine ,mlianza hivi KQ wakapigwa pini mkaanza kulia lia sasa nyie endeleeni tu njaa ikiwakamata hata punje haivuki boda mtaenda Sudan kuchukua

Halafu mlivyo mapongo mnasahau ishu tu kama ya maziwa mnayotuuzia yakizuiwa yatawaumiza Wakenya wengi
 
Hahahaha, hii habari anko hajaisikia nadhani akiipata anaweza mpa Ambassador 24hrs awe keshatua Nai:D:D
 
Teh teh.....Kenya nao akili zimewaruka!!!
Wakenya wataamua la kufanya..... na uchaguzi ndio huo upo mlangoni.....
 
Ningependa kusikia msuli wa serekali ukijitokeza katika hili sakata.

Mosi, Zuia KQ

Pili,Zuia maziwa yote ya Kenya kuingia soko la Tanzania

Tatu,fukuza waKenya wote wanaofanya kazi Tanzania wakiwemo wale wa EAC

Nne, Fukuza Balozi wa Kenya mara moja

Tano,Bidhaa zote za Kenya zipandishiwe ushuru 100%

Sita,Zuia bidhaa za chakula kwenda Kenya hasa Mahindi

Serekali kupitia wizara mbali mbali kuangalia namna ya kuzidisha mbinyo hadi yule jamaa anayetumia yale majani atuombe radhi.
 
Kenya Kuzuia Gesi ya Tanzania: Tanzania ichukue hatua dhidi ya Kenya

Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo. Tamko la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya linasema ' ndani ya siku 7 kuanzia juzi tarehe 24 Aprili 2017, itakuwa ni marufuku Kwa Kenya kuagiza Gesi ya kupikia kutoka Tanzania '. Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.

Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa.

Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.

Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.

Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania. Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.

Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo Kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma mjini
26/4/2017
Yaani magu mpaka leo upo kimya katika hili? Ningelikuwa mm saivi uhuru angekuwa anajuta kwa huo ubianfsi wake. Nyang'au.
 
Watanzania fungukeni. Walichokataa ni kupitia njia za panya ambazo hupeleka mitungi. Mingi halipiwi ushuru wale kukaguliwa ubora. Mombasa kuna bulk process hivyo ni fursa kwa makampuni yetu kupeleka bulk natural gas. Ila kwa kuwa sisi ni walalamishi hatulioni hili.
 
Ningependa kusikia msuli wa serekali ukijitokeza katika hili sakata.

Mosi, Zuia KQ

Pili,Zuia maziwa yote ya Kenya kuingia soko la Tanzania

Tatu,fukuza waKenya wote wanaofanya kazi Tanzania wakiwemo wale wa EAC

Nne, Fukuza Balozi wa Kenya mara moja

Tano,Bidhaa zote za Kenya zipandishiwe ushuru 100%

Sita,Zuia bidhaa za chakula kwenda Kenya hasa Mahindi

Serekali kupitia wizara mbali mbali kuangalia namna ya kuzidisha mbinyo hadi yule jamaa anayetumia yale majani atuombe radhi.
Duuh huo utakuwa ni ukatili wa hali ya juu. Watakuja mpaka kina MOI kuomba maridhiano.
 
Back
Top Bottom