Leslie Mbena
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 207
- 678
TANZANIA ITAENDELEA KUWA BABA LAO AFRIKA MASHARIKI NA KUSINI KWA MIAKA MINGI IJAYO,THE UNFORGETTABLE TANZANIA,HOME FOR EVERY AFRICAN.
Leo 14:15pm 17/05/2020
Tanzania daima inaongozwa na imani ya Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere,Sisi sote ni ndugu,Enzi zake Mwalimu Julius Nyerere alisema Tanzania haiwezi kuwa huru kama nchi nyingine za Afrika haziko huru, Tanzania itaendelea kutoa chakula kwa wote waliojipiga lokidauni pindi watakaposikia njaa.
Daima Tanzania ni nyumbani kwa kila Mwafrika,kamwe Tanzania kama Mama,hatutafunga mpaka kwa Mwafrika yeyote yule awae yote,kwa nchi yeyote ile ya kiafrika iwe kwa magonjwa,dhiki,au faraja,Tanzania ni nyumbani kwa kila Mwafrika.
Historia ya Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ina vipindi vingi vya historia vinavyoanzia nchini Tanzania,hasa katika harakati za Ukombozi wa nchi za Afrika, Tanzania ni nyumbani kwa nchi zote za Afrika.
Tanzania kupitia Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa kinara wa harakati zote za kulikomboa bara la Afrika,Julius Nyerere alijitoa mwili na roho kuhakikisha Tanzania haiwi huru peke yake,
Mafanikio ya Uhuru kwa nchi zote za Afrika ni ishara tosha kuwa alichokitamani Mwalimu Julius Nyerere na Wanamapinduzi wenzake ,imezaa matunda yanayopaswa kulindwa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo,
Kamwe Covid 19 haitayumbisha ushirikiano wa kikanda katika Afrika,SADC itaendelea kuwa imara na yenye amani,utulivu, Maendeleo na ustawi bora wa maisha ya Wananchi wake,
-Coalition of the Willing CoW.
Tumeona maadui wa ndani na nje ya Tanzania wakifurahia Kenya kufunga mpaka wake na Tanzania eti inaogopa Covid 19,Tumeona propaganda nyingi za Madereva wa Kitanzania wakinyanyaswa mpakani na kupimwa kinguvu na majibu yao yakitoka na Covid 19,hii ni njia ya kuchafuana kwa sababu ya ushindani wa biashara na Utalii,
Nimeona maadui wa ndani na nje ya Tanzania wakifurahia Rwanda kutumia Bandari kavu ya Naivasha nchini Kenya,niwaambie tu Kwanza hiyo option ya Rwanda kutumia Bandari kavu ya Naivasha ni temporary,
Niwaambie pia maadui wote wa Tanzania,msimjumuishe Museven kwenye uoga wa sasa,Msilolijua Museven ni Mtanzania wa Mpandangindo na kamwe hawezi kwa vyovyote vile kuiasi Tanzania.
-Kigali-Uganda-Naivasha-Mombasa.
Nimeona ikisemwa kuwa Bandari ya Naivasha itapunguza gharama ya uagizaji bidhaa nchini Rwanda kupitia Mombasa na pia ushindani wa usafirishaji wa bidhaa za nje nchini Rwanda kwani gharama za kazi zinapungua.
Kukamilika kwa bandari hiyo ya nchi kavu kutafanya mizigo mingi ya awali eti iliyokuwa ikipitishwa njia ya Dar-es salaam kupitia Barabara kuu itapungua kwa idadi kubwa,
Ndugu zangu Shule ni muhimu sana jamani,nimeona hata Diaspora wa Marekani wanafurahia Rwanda kuchukua Bandari kavu ya Naivasha na kuiacha Bandari ya Dar es Salaam,
Nimegundua diaspora wengi wa Marekani akina Dullayo,Hajji,Liberatus waliishia form four wakapata division zero kwa Ufisadi wa baba zao wakaenda Marekani na Sasa wameukana uraia wa Tanzania wanamuita Trump cousin yao,looh utumwa huu,Kasumba mbaya,Watu hata maana ya dry port hawajui wanaangalia picha tu za mtandaoni wanajiona wako Japan.
Kwanza Niwaambie wale maadui wa Tanzania ndani na nje ya Tanzania,hii move wala haihusiani na korona. Ni mikakati ya kibiashara tu.Rwanda walikuwa tayari wanatumia bandari ya Mombasa. Ila ilikuwa inawakosti sana kwa kutumia malori.
Wanachofanya sasa, ni kuwaachia Wakenya bandari ya Mombasa pengine hii Bandari ya Mombasa ni ya Wachina maana mkataba wa ujenzi wa SGR ya Kenya ulihusisha Bandari ya Mombasa,
Sasa Rwanda imeacha kusafirisha malori toka Mombasa hadi Naivasha na badala yake Treni ya wachina itasafirisha mizigo kwa reli kutoka Mombasa mpaka Naivasha ambako kuna hiyo bandari ya nchi kavu. Wanyarwanda na milori yao watakuwa wanasubiri Mchina ashushe mzigo Naivasha,
Nao wataenda kuchukua mizigo Naivasha badala ya kuburuza milori yao mpaka Mombasa,utumwa wa madeni kwa ndugu zetu Kenya ni mbaya sana,watafanya chochote hata wasichotaka watafanyishwa
Zoezi halikatazi mizigo ya Rwanda kuendelea kupitia bandari ya Dar es salaam ambayo ndiyo baba lao.
-Cost analysis,Uchambuzi wa gharama za Rwanda hadi Naivasha.
Usafirishaji utakuwa wa gharama za juu,it will be more expensive, look here, labda kama hujui biashara,Vijana wa CBE na IFM mtasaidia kuwajulisha maadui wa Tanzania.
-Kipengele Cha muda nacho tutakiweka kwa maana ya ucheleweshwaji wa usafirishwaji wa Mizigo,the time from Mombasa,Naivasha by rail that will cost some money & time. Dry port at Naivasha needs to be built, many people to be hired, equipments to be bought eg craines, plus electricity costs, maintanance, all costs goes up to Rwanda,Nimeongea lugha ya beberu ili Rwanda msikie kama hamjui Kiswahili,
Rwanda hadi Naivasha ni gharama kubwa sana sijui kama mnaelewa, Naivasha to Kigali about 900km by road, that is long distance too,Hakuna kitu kikubwa Rwanda umeokoa hapo, Haya wakiamua kwenda hadi Uganda kupitia Ziwa Victoria huo ni mzunguko mkubwa sana,
Yaani mzigo unatoka Mombasa unauleta Naivasha kwa barabara 200km,halafu unashusha tena unaweka katiks meli hadi Uganda unashusha,
Uganda hadi Rwanda,unapakia tena kwa lorries, hizo gharama na muda wa kupoteza na uharibifu wa mzigo,logistics ni nyingi sana na gharama kubwa sana hiyo, Hapo kibiashara ni gharama kubwa sana kwa Utaratibu mzima kwa maana ya process yote,Nadhani business people Vijana wa CBE enzi hizo Chino,Kabaro,Saidi,Langwene,Chozi mnaelewa,
-Dar es Salaam to Kigali,the best option,
Umbali ama Distance from Dar es Salam to Kigali is 1,450 km by road. Kwa akili ya kawaida tu hata bila kupita CBE au IFM Mizigo ikitoka Dar to Kigali hausimami kokote hadi Kigali, yaani siku 2 mzigo uko Kigali, bila kusimama kokote kule, Hapo gharama ni ndogo sana, na Rwanda hana gharama zingine zozote hapa,
Reli ya umeme ikianza kazi, mzigo unaweza kwenda hadi Isaka-Mwanza yaani mizigo ya Rwanda wanaweza chukulia Mwanza that is 320km tu,hapa unaweza kuona treni ya umeme ikikamilika ya mizigo tunapiga bao wote hata Uganda mizigo yao yote watachukulia Mwanza then wanasafirisha kwa meli Ziwa Victoria hadi Uganda.
So Reli ya umeme ikiwa tayari, Mwanza na Kigoma inaweza kuwa Dry Ports kubwa sana kwa ajili ya DRC Congo, Burundi, Rwanda na Uganda. Wakenya tunawapiga bao sana
Strategically bado Tanzania ni best option ya Rwanda, Mombasa ni kujiongezea gharama,Ukitumia Dar to Kigali haupiti nchi ya tatu Uganda tofauti na Mombasa-Naivasha-Uganda-Rwanda,Hata kama hawatajenga SGR ya Kigali to Isaka, bado umbali wa barabara kutoka Rwanda-Kahama-Mwanza ni mfupi sana, km 500 tu.
Swali tu ni SGR ya Tanzania itafika lini Isaka toka Rwanda kuunganisha hadi Mwanza itayokutana na SGR ya Mwanza-Tabora-Dodoma-Morogoro-Dar es Salaam,very soon Tanzania itakuwa Taifa kubwa maana miundo mbinu yake tayari Rais Magufuli ameshaitekeleza na inaendelea kumaliziwa.
-Bandari ya Dar es Salaam lango kuu la biashara kwa nchi za Jumuiya ya SADC.
Bandari ya Dar es Salaam,Tanga na Mtwara ni lango kuu la biashara kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC za Malawi,Zambia,Kongo(DRC),Msumbiji na Zimbabwe.
Bandari ya Dar es Salaam,Tanga na Mtwara zimejengwa kabla ya Uhuru wa Tanzania,zimekuwa zikisaidia biashara katika nchi za Malawi,Zambia,Kongo,Burundi,Rwanda,Uganda na Zimbabwe.
-Ufanisi na Gharama Nafuu.
Utoaji wa mizigo wa gharama nafuu kabisa tofauti na bandari ya Beira ambapo Zambia itaamua kuitumia endapo itafunga mpaka wake na Tanzania,utoaji wa mizigo na usafirishaji ni wa haraka zaidi,suala la kuhakikisha gharama zinakuwa ahueni kwa mteja linaangaliwa kwa umakini mkubwa.
-Faida ya mchanganuo wa Gharama.
Ukitumia Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania,unapewa mchanganuo wote wa gharama zikiwemo za usafirishaji kutoka bandarini hadi kwako(total road analysis).
-Malipo kwa njia ya Tehama(Mtandao).
Katika kuwapunguzia usumbufu wateja wanaweza kufanya malipo kwa njia ya Mtandao (online) kwa muda muafaka na haraka,
Kwa upande wa teknolojia ya habari na Mawasiliano (Tehama) si kwenye usalama tu bali inatumika pia vilivyo katika kurahisisha shughuli bandarini,
-Ofisi za Mamlaka ya Bandari katika nchi zinazohudumiwa na Tanzania.
Tanzania imefungua ofisi katika nchi zinazotumia bandari ya Dar es Salaam,Bandari ya Tanga,Bandari ya Mtwara kupitia ofisi hizo,Wafanyabiashara wa nchi hizo hawana sababu ya kusafiri hadi Dar es Salaam,
Ofisi zipo katika jiji la Lusaka nchini Zambia,Kigali nchini Rwanda,Lubumbashi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Bujumbura nchini Burundi,na nchini Comoro.
-Mawakala wa Mamlaka ya Bandari
Mawakala wa Mamlaka ya Bandari wapo hadi kwenye miji ya Bukavu na Goma ndani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Kampala nchini Uganda,wateja wanaweza kufikisha malalamiko yao kwa mawakala na kuyapatia ufumbuzi kwa wakati,
Nimalizie kwa kusema Tanzania inaongoza kwa kuwa na vivutio bora vya utalii barani Afrika,utafiti uliondeshwa na mitandao mbalimbali duniani mfano safaribookings.com,
Jitihada za Serikali za kulinda rasilimali za nchi na ushirikiano kutoka kwa wananchi zimesababisha ongezeko kubwa la idadi ya wanyama pori, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye wanyama wengi barani Afrika.
Vivutio 50 bora Barani Afrika, vivutio 10 kati ya hivyo viko Tanzaniani,Ruaha,Mahale,Gombe,Katavi,Tarangire,ziwa Manyara na Arusha,Vingine ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pori la akiba la selous,Vivutio hivyo vinaongeza pato la Taifa.
Tunapojifunza kuishi na corona kama tulivyoishi na surua,Ukimwi kwa kuchukua tahadhari,Rais Magufuli leo amesema hadi ndege za mwisho wa Mwaka zimejaa,Watalii wakigombania kuja Serengeti,Ngorongoro,Manyara,Mikumi na kuja kupanda Mlima Kilimanjaro,fahari ya Tanzania.
Mungu ibariki Jumuiya ya SADC,Mungu ibariki Jumuiya ya Afrika Mashariki,Mungu mbariki Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Ndugu John Pombe Magufuli.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854