Tanzania invyoinufaisha uganda kiuchumi

Tanzania invyoinufaisha uganda kiuchumi

KITAHYA

Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
25
Reaction score
13
Sijui kama na kwa majirani wengine ndivyo ilivyo, ila mie kwa hapa niaona niitumie Uganda Kama kielelezo maana mimi ni Mkazi wa Kagera Mkoa unapakana na Nchi ya Uganda. Nimeleta uzi huu kwa kuanagalia mazao mawili muhimu ya Kahawa na Samaki. Kahawa ya Kagera karibu asilimia 30 inavuka mpaka na kuelekea Uganda kwa njia ya ziwa na hata barabara. Jambo hili limekuwa la Muda mrefu. Hivi kwa nini watu wanapendelea kuuza kahawa Uganda? Jibu ni kuwa hivi sasa bei ya kilo moja ya kahawa isiyosagwa kwa Tanzania ni Tshs.1000/= wakati Mganda ananunua kwa Tshs1500/= tena kwa kuifuata mwenyewe. Wakulima wanajiuliza hivi Uganda wanapeleka kahawa soko la wapi ambako Tanzania hawajui? Inawashangaza watu kuona Uganda ili wafikie soko inabidi wapitie Tanzania au Kenya na kulipa ushuru kadha wa kadha, iweje wawe na bei ya juu kwa mkulima kuliko Tanzania ambayo hailipi ushuru kwa nchi yoyote?

Kwa upande wa samaki, hapo ndipo mgogoro kabisa, viwanda vya Tanzania vinanunua kilo ya samaki kwa bei ya Shilingi elfu 4000/= wakati kwa Uganda inaenda hadi Tshs 6000/= hivyo wavuvi wa Tanzania wanapata faida kwa kuuza samaki Uganda kuliko wanunuzi wa ndani? Kwa njia hii Uganda inasafirisha samaki kwa Wingi kuliko Tanzania wakati Tanzania inamiliki sehemu kubwa ya ziwa Victoria kuliko Uganda.

Najua wapo watakaosema wanaouza Uganda Kahawa na Samaki si wazalendo, hawajui kuwa kodi ya mazao hayo ndizo barabara, sawa, lakini naomba wewe ujibadirishe kwa muda tu uwe mukulima au mvuvi, upate suruba zote wanazopata baada ya hapo uje na jibu. Ni nani mhujumu wa uchumi wa Tanzania?

Jamani watu hawako tayari kupunjwa kwa makato rukuki yasiyokuwa na tija kwao. Ukweli ni kuwa ushuru unaopatikana kutokana na mazao hayo ni mdogo kuliko thamani ya Kahawa na Samaki zinazovuka mipaka.

Sina uzoefu na mipaka mingine lakini nadhani kote ni hivyo hivyo, jamani nani ataisadia Tanzania?
 
Inashangaza kuona namna ambavyo, wakulima na hao wavuvi wanavyochukuliwa kama wao ndo wakosa uzalendo namba moja, lakini ni wazi kwamba wanajaribu kuboresha maisha japo si kwa njia ambayo ni halali. Serikali nilazima iboreshe bei za mazao ghafi kwani nao wanahitaji maisha bora.
 
Dah mkuu Tanzania katika mambo ya biashara za kimataifa na mbinu za ukusanyaji kodi ni sufuri kabisa
 
Dah mkuu Tanzania katika mambo ya biashara za kimataifa na mbinu za ukusanyaji kodi ni sufuri kabisa

Mkuu,kwenye ukusanyaji kodi nadhani Tizi-"TANGANYIKA" tumezama zaidi ya sifuri,tuna mifumo mingine ya kinyonyaji isiyotofautiana sana na ile ya mkoloni mweupe japo waweza kusikia ndimi zikitoa maneno laini,matam na enye tumaini tele,vitisho na dharau pia kwa mtu wa chini yaani mlalahoi-mkulima na mfanyakazi na sasa tunasikia hata matajiri wanalia!teh,teh,'the rich do not cry' KWA PAMOJA TUSEME 'YATOSHA'!!!
 
wanakosa uzalendo kwasababu ya sh.500 ambazo seerkali ya tz haitaki kutoa badala yake inawataka walipie uzalendo wao . uliwahi kuona wapi duniani?
 
kwani tanzania wanajua biashara, wanajua bahasha tu acha waliwe
 
Kwenye uzi kama huu hutawaona vijana wa mtaa wa Lumumba.

Nape, Mwigulu, Taswira et al njooni hapa mtuambie!
 
Back
Top Bottom