Tanzania inazalisha Unga wa meno Ya TEMBO

Tanzania inazalisha Unga wa meno Ya TEMBO

KIROJO

Senior Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
169
Reaction score
21
Akichangia hotuba ya wizara hiyo, Mbowe alisema majangili wamekuja na mbinu hiyo mpya kwa lengo la kukwepa kunaswa na vyombo vya dola.
Alisema hivi sasa meno hayo hayasafirishwi kwa meli kama zamani na badala yake kuna viwanda nchini ambavyo huyasaga meno hayo na kisha kusafirishwa kama unga kupitia viwanja vya ndege.
“Watu hawa wamekuwa wajanja, wameona kupitisha meno kama unga ni rahisi kwani hakuna mashine za kung’amua unga huo,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema Serikali inapaswa kuwa na mikakati ya kukabiliana na biashara hiyo ambayo inaweza kuwamaliza tembo wa Tanzania.
Mbowe alisema kwa sasa kilo moja ya meno ya ndovu inauzwa mpaka Dola 5,000 (Sh7.9 milioni), jambo linalofanya majangili kubuni njia mbalimbali za kufanikisha njama zao.
Alishauri kuwa Serikali inapaswa kuchukua hatua kali dhidi majangili ikiwamo ya kuwanyonga wanapopatikana na hatia.
“Tatizo wahusika wakubwa wa biashara hii ni watu wenye uhusiano mkubwa na viongozi wa Serikali lakini dawa yao ni kunyonga tu,” alisema.
Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku chache baada ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Maliasili, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa kutoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwamba anahusika na biashara ya meno hayo.
 
Si ndio maana mtandao wa jangiri Kinana umeshamili nadhani hata hicho Kiwanda yeye ni muwakilishi
 
KIROJO huo unga unatumika kwa matumizi gani?
 
Last edited by a moderator:
Niliona ole milya akitoka mapovu kumwelekeza mwenyekiti amwulize mbowe alikuwa na hizo taarifa tangu lini na ikibidi achukuliwe hatua kwa kukaa na taarifa ambazo zinaleta hasara kwa taifa bila kuripoti mapema. Wazee wa vitisho kazini, lakini wajue watanzania tunawaangalia kwa makini
 
Nauliza serikali wanalinda nini na kuna haja gani ya kuwa na jeshi la polisi na usalama wa taifa kama rasilimali za nchi hii zinaliwa na watu wachache kwa mwamvuli wa ccm? mimi nawashauri ccm mimi niko tayari kwa kweli kuwaunga mkono kama watafanikiwa kulinda raslimali ya nchi na wananchi kwa maslahi ya taifa, kukemia udini, kubadili mfumo wa elimu na kuwa mfumo wa kumwandaa mhitimu kutokuwa tegemezi na maendeleo ya nchi kusambazwa nchi nzima na siyo dar kama ilivyo hivi sasa. pia viongozi wa serikali kukubali kukosolewa na wananchi kupata huduma bora za jamii kila mahali na wabadhirifu kuwajibishwa bila kuangalia anatoka chama gani. hapo mimi nitaipigania ccm kwa sehemu yote ya maisha yangu iliyobaki
 
Back
Top Bottom