Ukifikiria hali kama hii ambayo inatokea Uwanja wa Fisi ambako si mbali toka ikulu, inatisha kufikiria nini kinaendelea kwingine kule wapiga picha wasikofika.
Inafikia wakati mambo kama haya yamguse hata Kikwete mwenyewe.
Does government operate using JF comments?!
Makahaba 63 Dar mbaroni
2008-06-21 21:24:43
Na Mwanaidi Swedi Jijini
Watu 63 wanaodhaniwa kuwa hufanya biashara chafu ya kujiuza miili yao almaarufu kama makahaba wamenaswa na polisi Jijini na kutiwa mbaroni, huku saba kati yao wakitajwa kuwa ni wanaume.
Watu hao wamekamatwa wakati polisi wakiendesha msako dhidi yao katika maeneo mbalimbali Jijini.
Akizungumza na Alasiri
leo asubuhi, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limetokea jana, majira ya saa 4:00 na saa 6:00 usiku huko
Manzese Uzuri, Manzese Darajani na eneo maarufu kwa shughuli hiyo chafu la Manzese Uwanja wa Fisi.
Kamanda Kalunguyeye amesema kuwa makahaba hao ni wale ambao wanaishi kwenye nyumba zao kama watu wengine wa kawiada, lakini shughuli yao kubwa imebainika kuwa ni kujiuza miili yao.
Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Wakati huohuo, mwanamke mmoja aitwaye Anna Mkate, 28, amefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi cha mchanga wakati akichimba kokoto.
Kamanda Kalunguyeye amesema tukio hilo limetokea jana katika eneo la Bunju A.
Amesema Kamanda Kalunguyeye kuwa mwanamke huyo amekutwa na umauti huo wakati akiwa kazini akichimba kokoto na wenzake wawili, ambao wao walinusurika.
Amesema kuwa ahdi sasa, mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala.