Tanzania inatuhitaji wote sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania inatuhitaji wote sasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by emrema, Jun 5, 2011.

 1. e

  emrema JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimefuatilia matukio ya wiki na kuyatafakari kwa undani kabisa. Sasa nakuja na haya. Jamani watanzania tunalazimika kuikomboa hii nchi sasa hakuna mwingine atakaye kuja ikomboa na ile kauli ya mmoja wa wabunge kuwa kizazi kijachi kitayachapa viboko makaburi yetu inaniingia. Haya yamenisukuma hasa.
  1. Kupingwa kwa bajeti inayopendekezwa na Upinzani (Zitto) kwa kutumia jazba na maneno ya kejeli hasa na Viongozi walioshika madaraka makubwa bila kutumia utaalam wowote kumenishtua. Mimi ni mfanyakazi wa Serikali kuna vikao ambavyo ni vya muhimu na ndio msingi wa ufanisi wa taasisi yetu vinavyofanywa katika ngazi ya idara na huchukua muda mrefu mara nyingine masaa 12 havilipwi posho yoyote. Vikao vya ngazi za juu tu au kuanzia level fulani ambavyo vinalaiishiwa na vitengo vya chini ndio vinalipwa hadi 200,000 per day hata kama ni kikao cha saa limoja! Kwa wiki unakuta kuna vikao hivyo 3 au 4 na watu ni wale wale. Posho hizi naunga mkono zifutwe.
  2. Kuna viongozi waliopo madarakani kwa lengo la kupinga hata yale mazuri yanayopendekezwa mfano ni kuingiliwa baadhi ya mawaziri moja kwa moja kwenye utendaji wao wa kazi kama Magufuli.Kauli za viongozi hazilengi matatizo ya wananchi hasa umaskini na suala la umeme.
  3. Ukandamizaji wa Upinzani kwa kutumia jeshi la Polisi. Hapa kuna hatari kubwa sababu wananchi tumeona wanaanza kuchukua sheria hata kuvamia vituo vya polisi. Hii itaendelea sana tu.
  4. Maisha ya wananchi yanaendelea kuwa ya shida serikali imekaa kimya kwenye mahospitali dawa hakuna wakati nimesoma wiki hii kuwa madawa yameharibika msd??
  5. Jeshi la wananchi lipo kwa ajili ya nani mipaka yetu ipo uchi wageni zaidi ya 1000 wanaingia na kupita nchini kila siku bila usimamizi wowote. Polisi wanaua wananchi hapa jeshi linatakiwa litoe msimamo sababu NDILO linatakiwa kulinda wananchi hasa polisi wanaposhindwa.

  NAPENDEKEZA

  Viongozi wenye uchungu bado na Nchi waache unafiki na wasimamie misingi na malengo ya kitaifa hasa katika kuondoa umaskini na kuimarisha uongozi bora. Hapa napendekeza vyombo vya habari viendeshe vipindi maalumu vya wazi kama kile cha Kipima joto ITV kwa kuwaita viongozi hawa. Lowasa aeleze Taifa nini kimetokea na tufanye nini kwani inaonekana anayo mengi ambayo inawezekana akayatoa kwa jazba baada ya kukwanguliwa gamba ambalo yeye mwenyewe anasita bado kujivua na kushindwa kusaidia Taifa. Sitta atoe kwa usahihi mwongozo kwa Spika mpya ambae anaonekana hajui kuwa MBUNGE ana kinga kikatiba na ndio maana huyu anayetajwa kula njama ya kumwua Chageni hajakamatwa bado kama wanavoyburuzwa wale wa upinzani. Bunge na mbunge ni mhimili mmojawapo kati ya ile 3 ya nchi. Lissu awafahamishe wananchi juu ya katiba yetu na imefikia wapi na nini kifanyike na hasa nafasi ya muungano. Wengine wanajf naomba uwaongeze.

  Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Kimsingi mapendekezo yako yako poa na yanamafaa kwa tz mpya!
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,759
  Trophy Points: 280
  mtanzania mpya ndo yupi? we ni mpya au ushachakaa?
   
Loading...