Bushesha jr
JF-Expert Member
- Apr 26, 2020
- 674
- 690
Ndugu Wana jamvi nimetafakari sana hatma ya nchi yetu endapo CCM itashindwa kusimamia majukumu yake hususani rasilimali za nchi yetu,hii ni kutokana na ukweli kwamba vyama vya upinzani naona havina sera ya ulinzi wa rasilimali wala havijali kabisa.
Aidha sababu nyingine ni kwamba vyama vyetu vya upinzani ni dhaifu mno na havina maono toka aondoke nguli wa siasa na mzalendo wa kweli Dkt. W. Slaa vyama hivi havijawahi kuwa na agenda tena.Vyama hivi vimekisa dira na mbaya zaidi vyama hivi havina agenda ya ulinzi wa rasilimali za nchi yetu.
Wapinzani wamekuwa wakibeza ulinzi wa rasilimali zetu na wanaonekana wazi kuwa kwao ulinzi wa rasilimali za Taifa siyo kipaumbele,tunahitaji na tunaomba wanasiasa wa nchi hii mlete chama mbadala wa CCM na kiwe Cha kizalendo Kama kile cha EFF Cha Julius Malema huko Afrika Kusini.
Tusipofanya hivi Kama Taifa ipo siku tutajikuta katika mtanziko mkubwa tusijue pa kwenda.
Nawatakia tafakuri njema