txyz
Member
- Apr 3, 2014
- 89
- 48
Kwa muda sasa nimekuwa nikifanya utafiti usio wa kimaandishi kuhusiana na wanasiasa wa Tanzania.
Nilichobaini ni kuwa katika vyama vyetu vya siasa,asilimia kubwa ni wale ambao hata ukiwapa mwezi kudefine siasa ni nini wataambulia patupu.
Watu hawa wanaongoza kwa propaganda chafu zenye kujenga chuki na zilizojaa tabia ya kujisifu na kujiinua.
Utawasikia wengine wakitamba mimi ndo kiboko ya,fulani ni rafiki yangu,tutawashinda hadi wakimbie mji na kauli nyingine nyingi.
Kinachonisikitisha wananchi nao wamewapa mashiko katika jamii zetu,wananchi wako tayari kuchekeshwa na upuuzi.Kwa kifupi hawa ni wasakatonge katika medani ya siasa.
Wengine wako tayari kujeruhi wengine wanaoonekana kwenda kinyume na itikadi zao.Wapo vyama vya upinzani ,wapo chama dola.
Namshauri msajili wa vyama vya siasa atoe agizo kwa vyama vya siasa kuhakikisha wanachama wao wanapewa elimu ya uraia kama sheria inavyosema na izuie wafuasi na wakereketwa wasio na maadili wasipande katika majukwaa ya vyama vyao.
Kama tutapuuza,naiona hatari kwa nchi yetu kutokana na wavamizi hawa wa siasa.