Yombayomba
JF-Expert Member
- Aug 23, 2006
- 818
- 214
Nonda kwa kweli mimi siioni Tanganyika. Hiyo power of Attorney labda alipewa Nyerere as a natural person and not a legal person. Hayo mambo yasiyo ya Muungano ambayo unasema ni ya TAnganyika yanaamuliwa na Bunge gani au na Baraza gani la Mawaziri? Mbona wakati wa kujadili hotuba za Wizara ambazo si za muungano wabunge toka Zanzibar hawatoki nje ili mambo yasiyo ya muungano yajadiliwe na Watanganyika peke yao? Huwa nashangaa ati wabunge toka Zanzibar wanakuwa kwenye kamati za Bunge za Nishati na Madini, Utalii, Ujenzi na Miundombinu na wanapiga kelele kwelikweli wakati haya Mambo si ya Muungano kwa Mujibu wa Katiba. Ni bora wasingekuwa wanashiriki katika mambo hayo ningeamini kuwa japo kwa mbaaali Watanganyika wanaaamua mambo yao kivyao, lakini loooo Wazanbibar Baraza la Wawakilishi LAO Bunge la Muungano LAO imekaaaje? Paomoja na hayo mchakato wa Kutunga Katiba Mpya/Kurekebisha Katiba unatupa nafasi mujarabu ya kuuangalia Muungano wetu kwa jicho la pili ili tuachane na mazonge yanayouzunguka huu Muungano ambao kwangu ni tata.
Makaimati,
Hivi una habari mjomba wenu Bakhersa anadai eti mama yake Mnyamwezi na baba yeke Mpemba? nyinyi ni ndumila kuwili, mnatikisa kiberiti tukija juu mnafyata, hivi nani anawadanganya kuwa bara inaitaka Zanzibar? kama si nyinyi wenyewe kutaka muungane?
Kilichotokea Zbr siku tatu zilizopita ktk mijadala ya kukusanya maoni kuhusu Mapitio ya Muswada wa Katiba, 2011 wote tumejionea. Nadhani hapa the best way kwa kuwa tukiulizwa sisi wenye nchi iwapo tunautaka muungano au la jibu litakuwa - hatuutaki! Labda hao viongozi ambao nadhani ni uoga na unafiki wa kutotaka kuonekana muungano umewafia mikononi mwao ndio wanaukumbatia muungano. Tuanze kujadili the best way ya kila upande kuanza kivyake! Tujadili ni namna gani ya kupeana talaka, na namna gani tunaweka mahusiano yetu ya kidiplomasia, kijamii, kiuchumi n.k.
Hakukuwa hata na sababu ya kutuma ujumbe wa kina mzee Sitta Zbr, for what? kwa kuwa kama maoni ya katiba kutoka upande wa Zanzibar yangeweza kupatikana thru Wizara inayoshughulikia Muungano, Wabunge zaidi ya 70 kutoka Zbr ktk Bunge la Tanzania, Wabunge 5 kutoka BLW Zbr waliopo ktk Bunge la Tanzania etc. Tunajikomba nini hadi kuraruriwa Muswada mbele ya macho ya watu wazima kama kina Sitta???? Viongozi wetu wasikie, pleeeease JK na timu yako vunjeni huu muungano hakuna atakayewalaumu. Hata mapenzi yakianza ni matamu sana lakini mkishachokana hufikia mwisho hata mbinu gani zikitumika, mapenzi yakiisha - yameisha! Ndoa yetu ktk muungano imefikia tamati, lets break the knots. We need back our beloved Tanganyika!
Hilo la Bakhresa halina uhusiano na matakwa ya Wazanzibari> Bakhresa ana hiyari yake nanyi mnahiyari yenu juu yake. Nafikiri hamna uwezo wa kumfanya chochote kwani anaweza kuondosha miradi yake au akawa kama mwekezaji. Mna wawekezaji wa kiwango cha Wachina wakiuza vikombe mtamdharau Bakhresa anaeekupeni karibu nusu ya mapato ya kodi kuliko wafanya biashara wenu.
Hivyo wewe unashangaa kuwepo Mnyamwezi na Mzanzibari? Kamuulize Abuod Jumbe, Ali Hassan Mwinyi, Hassan Nassoro Moyo, Marehemu Saidi Natepe, Seif Bakari na wengi.
Hata hivyo ishu hapa ni kuwa kama ni Muungano basi uwe wa haki na usawa kama hamuwezi basi na tuuuvunje.
Mojawapo ya mambo yaliyonichefua kwenye muswada wa katiba ni pamoja na Part III hasa section 5 na 6. S.6 inasema kuwa wajumbe wa tume watatoka pande zote za muungano kwa idadi sawa (yaani kama wajumbe ni kumi basi Zanzibar watoke 5 na Bara watoke 5), ukienda mbele zaidi unaona kuwa maamuzi ya watu wa Bara yanaamuliwa na Wazanzibari.
Bunge letu lina wabunge takribani 360, kati ya hao zaidi ya 75 wanatoka Zanzibar (kama asilimia 20 hivi) sasa hili suala la katiba kwa nini tusitumie uwiano wa wabunge au hata uwiano wa watu, je kwa nini serikali yetu inabembeleza sana huu muungano?
Nadhani inabidi hii ipingwe kwa nguvu zote na wabunge wa bara maana huku si kuimarisha muungano bali kuendekeza upendeleo ambao nisingependa kuutaja hapa
Ukweli ni kwamba population ya wazanzibari including wapemba haijafika hata 1.5m. Iloikatiba mpya itende haki kwa muuungano, representation bungeni lazima iwe ya ki-uwiano. 1.5/43 x 100 = 3.5%. Wao walipaswa kuwa 3.5% tu hata hivyo natambua kuwa kuna factor nyingine za kisiasa zinazofanya wawe karibia asilimia 20; siasa hizo si za haki kwani inwezekana mbungo mmoja kule Zennji akawa anawakilisa watu wasiozidi elfu 30. This is bad. Katiba lzima iliangalie hili suala la muungano upya.
Hivi unajua hicho kipande chenu cha ardhi(Zanzibar) miaka 20 ijayo kitazama kutokana na tabia nchi ambayo itasababisha maji kuongezeka na chote kuzama,jaribu kuwaheshmu watanganyika wanaowatunza na kuwapa ardhi,cdhan kama muungano ukivunjika mtatosha huko kwenu..ee Mungu 2letee Tanganyika ye2..
Ukweli ni kwamba population ya wazanzibari including wapemba haijafika hata 1.5m. Iloikatiba mpya itende haki kwa muuungano, representation bungeni lazima iwe ya ki-uwiano. 1.5/43 x 100 = 3.5%. Wao walipaswa kuwa 3.5% tu hata hivyo natambua kuwa kuna factor nyingine za kisiasa zinazofanya wawe karibia asilimia 20; siasa hizo si za haki kwani inwezekana mbungo mmoja kule Zennji akawa anawakilisa watu wasiozidi elfu 30. This is bad. Katiba lzima iliangalie hili suala la muungano upya.