Tanzania imekufa, tunasubiri 2015 angalau kama tutapata wa kufufua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania imekufa, tunasubiri 2015 angalau kama tutapata wa kufufua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Jul 11, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ndio Tanzania imekufa kiuchumi na kijamii na kisiasa.

  Ufisadi umeshamiri na mafisadi wametamalaki.

  Kiongozi mkuu wa nchi hana habari na watanzania?

  Hakuna wa kumuuliza au kumhoji Raisi, Bunge limetekwa na mafisadi

  Viongozi wa vyama vya upinzani wananunuliwa!

  Watanzania hawana sauti, nchi yao inauzwa, watanzania wanateseka na ni waoga sana.

  Hata viongozi wastaafu na wanaoheshimika kama akina Cleopa Msuya, Jaji Bomani, SAS,SUMAYE,MKAPA,MZee Ruksa, na Taasisi ya MWalimu Nyerere wamekaa kimya kabisa, wanaona nchi inaangamia.

  Watanzania wenyewe tumekaa kimya, tunaparangana na shughuli za kupata chakula au malazi tu wakati R 1 anajenga mahoteli, U track na ma Transporter na ma real estates apartments na ma viwanja kama Burka.

  OOh Watanzania amka, ingia barabarani tumtoe huyu nduli anaelea mafisadi. angalia wanatunyonya kupitia kodi, halafu mafisadi wanakula kodi zetu -- ooh tAnzania. Rada, NDege ya raisi, KAgoda agriculture, meremeta,buzagwi, IPTL,Dowans.

  Watanzania mnalipa kodi kupitia bei ghali za diesel/petrol/ na wanyonge wananyongewa baharini na bei za mafuta taa.

  OOh VAT kwa kila Mtanzania, ukinunua hata pipi tu tayari umelipa VAT. OO mfanyakazi lipa PAYE na VAT


  Ushahidi uko wazi RADA chenge
   
Loading...