Tanzania imekataa masharti ya uingereza!

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alitoa msimamo huo leo Jijini Dar es Salaam akisema huko ni kwenda kinyume na sheria na utamaduni wa nchi yetu inayotambua ndoa ya mme na mke kama kiini cha familia.Membe alisema hayo alipokuwa akizungumzia mkutano wa Jumuia ya Madola uliofanyika wiki iliyopita Perth, Australia.Alitoa msimamo huo kufuatia kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuwa wana mpango wa kusitisha misaada kwa nchi ambazo katiba na sheria zake hazitambui mashoga na ndoa zao. “Nchi yetu inaheshimu sheria na utamaduni wake hivyo hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti kama hayo ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja, hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nje”, Waziri Membe aliwaambia waandishi wa habari.Alisema tamko hilo ni msimamo wa chama cha Conservative na kibaya zaidi linatoka Uingereza ambako ndio wenye Jumuia ya Madola hivyo linaweza kusababisha kuvunjika kwake na Cameroun na nchi hiyo ndio watawajibika jumuia hiyo ikivunjika.Alisema miongoni mwa nchi 54 za Jumuia ya Madola kati yake nchi 13 ushoga ni sehemu ya katiba yao wakati 41 hazina utamaduni huo hivyo msimamo wa Tanzania ni kuwa na ndoa za jinsi mbili tofauti, kinyume na hapo unafungwa kifungo miaka 30.Alisema kuendelea kukumbatia ushoga si jambo zuri na si la kulishabikia hata kidogo vinginevyo wanaweza kujuta nchi ikijihusisha na ushoga na kuukubali kupata misaada ya maendeleo. ”Tanzania hatuwezi kuyumbishwa kwa masharti ya kipuuzi bora tuitunze nchi yetu.Tanzania ni nchi maskini lakini kamwe haturuhusu kuingiliwa na nchi nyingine.Kama ndio hivyo basi wakae na hela zao,” alisema Waziri Membe wizarani kwake.Alisema katika mkutano wa Madola, walijadili mabadiliko ya hali ya hewa ambapo walibainisha nchi zinazotegemea mvua zichukue hatua gani kuishi bila kuathiri hali hali ya hewa.Pia alisema walijadili kuhusu hatua za kuchukua ili kuvisaidia visiwa vidogo kama Maldives vinavyoliwa na maji ya bahari yanayojaa kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa.Alisema watakuwa na mkutano London Aprili mwakani kujadili mikakati hiyo.

Source: TANZANIA IMEKATAA MASHARTI YA UINGEREZA YANAYOTAKA NCHI ZINAZOTAKA MISAADA YAKE ZIRUHUSU VITENDO VYA USHOGA « Strictly Gospel
 
Kwa hiyo kuna "Plan B" misaada ikipungua au kuondolewa kabisa au Membe anachojua ni "hatuyumbishwi" tu?
 
kwenye miaka ya 1960, wakubwa walituonya kuhusu ongezeko kubwa la watu kwa nchi maskini. Walipendekeza njia mbali mbali za jinsi ya kupanga uzazi (birth control). Siku hizo ilikuwa ni dhambi kubwa kwa waafrika kuzungumzia suala la mpango wa uzazi.Ilibidi hata "mashirika" ya kutoa huduma za uzazi zipewe majina ya kificho kama "UMATI" ambayo kazi yake ilikuwa ni tofauti kabisa ya maana ya neno la shirika hilo. Hakuna gazeti wala radio ambayo ingeweza kutumia neno kondomu kwenye taarifa zake. Sasa baada ya kupigwa msasa na vyombo vya ugaibuni, 'elimu ya uzazi" imeanzishwa hata kwenye shule za msingi.

Nadhani na hili la mahusiano ya njisia moja ni suala la muda tu. Bora hata baadhi ya makanisa yameona kwamba la Mungu halina kosa, na hawa mashonga wameumbwa na Mungu huyo huyo, wala hawakuomba wawe hivyo, ni muda tu hata wanasiasa wa bongo wataona ukweli wa suala hili na kwanza, kunyamazia tu likiendelea kabla ya kushabikia kama ilivyo kwa kutowabagua wagonjwa wa ukimwi, au kushabikia matumizi ya kondomu.

Watako kuwepu miaka kumi ijayo wataona ushoga ukipigiwa debe kama ukimwi.

macinkus
 
hata mwanzo alikataaa kuutambua uongozi wa waasi wa libya
chakushangaza baada ya wiki wakakubali!
 
Hapa iuingereza imetafuta kigezo cha kuacha kutoa misaada, nadhani imezidiwa hiyo ni mbinu tu, na sisi tuache utegemezi jamani unaona madhara yake?
 
Back
Top Bottom