Tanzania imechafuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania imechafuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tikerra, Sep 17, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati mbaya watanzania wengi hawataki kujisomea. Lakini niseme jambo moja wazi,nalo ni kwamba, wale tunaoamini wanatusaidia, ndio wanaotumaliza.Kuna ushahidi wa kutosha kwa wale wanapenda kujisomea, kwamba wale, tunaowaita wafadhili wakisaidiwa na Marekani, ndio wanaosaidia katika kusambaratisha nchi yetu.Hawa ni pamoja na World Bank na IMF.Kisichoingia akilini mwangu, ni kwamba,kwanini tunaendelea kuwakumbatia wauaji hawa,wakati nchi yetu ina rasilimali za kutosha za kuweza kujiendesha yenyewe?Viongozi wetu wamepewa usembe au vipi?
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Raisi wetu anaongea mengi, lakini hili nalo limenitia mashaka.Eti anasema malumbanao yanayoendele sasa nchini, yanaonyesha ukomavu wa demokrasia.Mmm!Jamani kweli?Mimi binafsi sioni hivyo.Kwangu mimi hizi ni dalili za nchi kusambaratika,'disconnection' kati ya wananchi na uongozi,na kwa ujumla nchi kushindikana kutawalika.Na matamshi ya Rais Kikwete pia yanaonyesha hali ya yeye mwenyewe kukata tamaa,na kutokuwa na nia ya kweli ya kuitoa nchi mahali ilipo sasa.Ieleweke wazi kwamba wanachi wamekata tamaa kupindukia na hatua za makusudi kabisa zipochukuliwa kuondoa hali hii, nchi yetu itasambaratika kabisa.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Nchi imechafuka

  Mwandishi Wetu Septemba 17, 2008
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  Ni vitisho, vitimbi, ufisadi

  KUNA kila dalili kwamba hali ya Tanzania kama Taifa imechafuka karibu katika kila nyanja na sasa vitisho, tuhuma, vitimbi na ukiukwaji mkubwa wa maadili ni mambo yanayoonekana kuanza kuzoeleka bila kujali athari zake kwa jamii.

  Matukio ya hivi karibuni na hata miaka michache iliyopita, yanadhihirisha kuwapo kwa ombwe (vacuum) kubwa katika uongozi unaosababisha kila kundi kufanya mambo bila kujali athari zake kwa jamii.

  Vitisho dhidi ya baadhi ya wanasiasa na wanahabari, mkanganyiko ndani ya vyama vya siasa kikiwamo chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM) na vyama vya upinzani yameelezwa kuwa ni matokea ya kuchafuka kwa hali ya kisiasa nchini, hali iliyoanza kwa takriban miaka mitano sasa.

  Kiongozi mmoja wa dini ameliambia Raia Mwema kwamba, hali ya sasa si shwari na kwamba nchi inaelekea katika machafuko iwapo viongozi wa kisiasa na kidini hawatachukua hatua za haraka kurekebisha hali hiyo.

  "Kwa sasa sitaki kujitokeza kuliweka hili wazi, lakini nakwambia kijana, nchi inaelekea kwenye machafuko na kwamba ni lazima sisi viongozi wa dini, wazee na viongozi wa kisiasa wenye nia njema na nchi hii tufanye uamuzi wa haraka wa kukabiliana na hali hii," alisema kiongozi huyo wa kanisa moja linaloheshimika nchini na kuongeza;

  "Nitajitokeza siku si nyingi na kubainisha haya, lakini haiwezekani sasa watu wanakurupuka na kutishia watu maisha, si kawaida hata kidogo maana mtu anatishia na baadaye mutazoea na kusema ni vitisho ili utekelezaji uwakute mukiwa mmelala."

  Katika siku za hivi karibuni kumekuwapo taarifa za kutishiwa kwa viongozi wa kisiasa akiwamo Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Wabunge wawili wa CCM, Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela) na Anne Kilango Malecela wa Same Mashariki pamoja, wanahabari Saed Kubenea na mfanyabiashara anayemiliki vyombo vya habari, Reginald Mengi.


  Habari zilizothibitishwa na baadhi ya wahusika akiwamo Sitta, zinaeleza kuwapo kwa taarifa za vitisho vikilenga kuwatahadharisha kuwapo kwa sumu kali iliyoingizwa nchini kutoka mashariki ya kati, taarifa zilizofikishwa kwenye vyombo vya dola.

  Mbali ya vitisho hivyo, Mwanasiasa asiyetabirika, Christopher Mtikila, ameibuka na kuwatuhumu viongozi wa chama cha upinzani wa Chadema akidai kwamba wanahusika na mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Tarime kupitia chama hicho, Chacha Zakayo Wangwe, ambaye alifariki katika ajali ya gari eneo la Pandambili, mkoani Dodoma.

  Mtikila ambaye habari zake zimechapishwa sana katika gazeti moja litolewalo kila siku, anakwenda mbali zaidi kwa kuelezea hata jinsi wauaji wa Wangwe walivyotekeleza mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kudai kwamba walitumia nyundo kummaliza katika maelezo ambayo baadhi ya wanahabari walisema yanaweza kutolewa na mtu aliyekuwapo eneo la tukio pekee.

  Kifo cha Wangwe kilizua tafrani za kisiasa na vyama vya siasa vilitumia msiba huo ama kujijenga ama kudhibiti wapinzani wake, ikiwa ni pamoja na vyama vya upinzani kusigana na kwa upande mwingine CCM kujizatiti kutaka kulitwaa jimbo hilo.

  Matukio hayo yanakuja wakati kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, nchi imekumbwa na mitikisiko kadhaa ya mfululizo inayoathiri hata mshikamano wa kitaifa, masuala ya maendeleo na hata kuyumbisha uchumi na kuathiri huduma za jamii.

  Mbali misigano hiyo inayowagusa wapinzani pekee, ndani ya CCM nako kumekuwa na mivutano kuanzia ndani ya vikao vyama chama hicho tawala, ndani ya Bunge, ndani ya jumuiya zake na sasa hata katika vyombo vya habari ambako wanasiasa wa chama hicho wamekuwa wakilumbana kudhihirisha kuendelea kuyumba kwa hali ya kisiasa nchini.

  Mwanasiasa mmoja ndani ya CCM ameielezea hali hii kuwa ni viashiria vya hali ilivyo ndani ya mfumo wa kitaifa wa siasa na kwamba umesababishwa kwa kiasi kikubwa na matumizi makubwa ya fedha katika siasa bila kujali zinakotoka fedha hizo.

  "Huwezi kuwa na viongozi ambao wamenunua nafasi zao kuanzia ngazi ya chini halafu utarajie kuwa na uongozi bora ama utarajie kuwapo na hali ya kuelewana! Hapana. Siasa sasa zinaangalia nani anapata nini na si nani anatumikiaje umma. Huwezi kuwa na wanasiasa ambao kabla ya kuzungumza anawasiliana kwanza na mtu ambaye hata siasa hajui maana yake nini! Hii ni hatari sana," anasema mwanasiasa huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

  Mwanasiasa huyo ambaye anatokea Zanzibar, anasema sehemu kubwa ya wajumbe wa NEC na hata viongozi wa juu wa chama wamekuwa wakisikiliza zaidi maelekezo kutoka kwa watu waliowafadhili katika chaguzi zilizowaingiza katika nafasi zao na hata katika vikao vyao mtu akisimama unajua kabisa atazungumza nini.


  "Kwa kweli tumefika mahali pabaya, hata hapa Dodoma tuko kila mtu ana maelekezo ya nini cha kuchangia aliyoyapata anakojua mwenyewe. Ndiyo maana siku hizi hunisikii nimeamua kukaa kimya kwa kuwa siwezi kuelekezwa na mtu ambaye hata siasa hajui eti kwa sababu tu ana fedha," anasema.

  Kauli ya mwana CCM huyo inaungwa mkono na wanasiasa kadhaa hususan vijana ambao baadhi wanasema kwa hali ilivyo vijana wenye msimamo hawana nafasi katika siasa za sasa ambazo wenye fedha ndio huamua nani anastahili kuwa kiongozi.

  "Sisi vijana tunapaswa kupambana sana, maana umeona mfano wa Nape (Nnauye) ambaye kusema kwake ukweli kuhusiana mradi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) amesumbuliwa sana kwa sababu tu anagusa maslahi ya watu ndani na nje ya siasa ambao wana uwezo mkubwa kifedha. Kama huna fedha na hutaki kusikiliza wenye fedha wanachotaka ujue watakudhibiti tu," anasema mwanasiasa kijana ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka mkoani Tanga.


  Hata hivyo kijana huyo anasema vijana na wanasiasa wenye msimamo hawapaswi kukata tamaa kwa hali ilivyo na badala yake ni kupambana kubadili mfumo kandamizi unaobebwa na fedha chafu, kazi ambayo anakiri kuwa ni hatari katika mazingira mapya ya utandawazi na soko huria.

  Kabla ya kuibuka hadharani kwa misigano ndani ya siasa, Serikali ya Kikwete ilikumbwa na mfululizo wa tuhuma mbalimbali za ufisadi dhidi ya wanasiasa ndani ya serikali yake na baadhi ya wastaafu, tuhuma ambazo hadi sasa hakuna hata moja iliyofikishwa mahakamani zaidi ya kuendelea kuzungumzwa katika majukwaa ya kisiasa, bungeni na katika vyombo vya habari.

  Tuhuma hizo ni pamoja na zile za utata katika mradi wa umeme wa dharura ambao ulisababisha kujiuzulu kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, ambao wote waliwahi kushika nyadhifa za uwaziri wa Nishati na Madini kabla ya sakata hilo.

  Siku chache baada ya kujiuzulu kwa mawaziri hao, serikali ya Kikwete ilipata mtikisiko mwingine baada ya Waziri ambaye alimrudisha katika baraza lake la mawaziri na kumpa wizara nyeti ya Miundombinu, Andrew Chenge kujiuzulu akituhumiwa kuhusishwa na sakata la ununuzi wa rada ya kijeshi, yeye akiwa miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na rushwa iliyotolewa na kampuni ya BaE System ya Uingereza.

  Baada ya kujizulu kwa Chenge, kukaibuka sakata lingine likimgusa tena aliyekuwa Waziri Mkuu, Lowassa na kwa sasa likiwa linaihusisha jumuiya ya CCM (UVCCM), hadi kusababisha malumbano yaliyosababisha umoja huo kumsimamisha uanachama wa jumuiya hiyo mwanasiasa kijana Nape Nnauye.

  Baada ya kusimamishwa kwa Nape, Kamati Kuu ya CCM ikaingilia kati na kupooza joto lakini tena Kikwete akiwa Mwenyekiti wa CCM, amejikuta akimpa Chenge jukumu la kupitia mkataba wa jengo la UVCCM ulioleta utata, uamuzi ambao ulipigiwa kelele tena na wananchi wakiwamo baadhi ya wana CCM wenzake. Pamoja na Chenge wajumbe wengine wa timu hiyo ni Dk. Abdalah Kigoda na Pindi Chana, wote wakiwa wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM na watu wenye taaluma ya uhasibu.

  Sakata lingine ambalo linaendelea kuitikisa serikali ya Kikwete ni kuhusiana na wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyokuwa ikisimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sakata ambalo hadi sasa wahusika wamekuwa wakijikanganya kuhusiana na utekelezaji wa sheria kuhusiana na watu waliohusika na wizi huo.

  Wachambuzi wanasema Rais Kikwete amelegeza msimamo katika suala hilo na inaelekea anapingana na maagizo yake mwenyewe ya awali ya kutaka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria, baada ya kulihutubia Bunge na kutoa muda wa hadi Oktoba 31 kwa wahusika kulipa fedha walizoiba "vinginevyo" watafikishwa mahakamani. Rais ameonyesha kwamba kwa watakaolipa hawatachukuliwa hatua, jambo ambalo limepingwa na wengi.

  Wiki hii katika kile walichokiita maadhimisho ya mwaka mmoja wa mapambano dhidi ya ufisadi, Chadema wamedai kwamba fedha za EPA zilizoibwa zimetumika kuisaidia CCM katika uchaguzi wa mwaka 2005, na hivyo wameelezea wasiwasi wao kama kweli serikali ya CCM inaweza kuwachukulia hatua wahusika wa wizi huo.

  Madai hayo ya Chadema yemeelekea kuaminiwa na wananchi wengi kutokana na kusuasua kwa hatua dhidi ya wahusika hata baada ya kikosi kazi (task force) iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kukabidhi kazi yake ya awali bila ya kutangazwa kwa hatua zozote dhidi ya wahusika.
   
 4. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  masikini tanzania yangu!
   
 5. M

  MKUDE WA MGETA Member

  #5
  Sep 18, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mimi nauliza wana jf mnafikiri tufanyeje ili kuondokana na hili sekeseke kwani inasemekana kuwa hii nchi inaendeshwa na kundi moja la mafisadi lenye nguvu sana na inasemekana hata 2010 jk atachukua nchi kwani ameweza kuwalinda mafisadi.
   
 6. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tanzania tumeiharibu wenyewe
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna ukweli ndani yake na ni obvious kuwa kuna leadership Vacuum na nchi iko mikononi mwa mafisadi. Lakini, huyu mwandishi ameandika kwa lengo gani? Ameandika kutufahamisha tunachofahamu? ameandika kutuma message kutuonesha need for change, au ametuandikia kutuambia kuwa whatever we do mafisadi wataendelea kupeta 2010? Ni vigumu kuelewa. Labda ametuandikia ili tuweze kufahamu kuwa kuna sumu zaidi imeletwa kutoka Mashariki ya kati.
   
 8. r

  rpg JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 3,516
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sijakuelewa, una maana gani?? Hebu tufafanulie. Kwamba hujaelewa alichoandika, ama kiswahili si sanifu.....
   
Loading...