lil wayne
JF-Expert Member
- Apr 15, 2016
- 992
- 904
Tukianza kwa kuzungumzia hali ha Taifa hili miaka 10 iliyopita, utagundua kuwa nchi ilikuwa Mahututi kupita kiasi. Hata wananchi wake walifika hatua ya kukata tamaa na Taifa lao. Ghafla mapenzi na taifa lao yalipotelea pasipo julikana.
Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kama ungepata bahati ya kuingia kwenye mioyo ya watanzania mmoja baada ya mmoja ungeliona kiu ya uhitaji wa ujio wa kiongozi ambaye angeweza badilisha hali.
Ni kweli watanzania walihitaji kiongozi imara zaidi ya yule wa awamu iliyopita. Wengi waliaminishwa kuwa huyu mpya ndiye "mwenyewe", hata wakatolea mifani CHANYA ya jinsi alivyokuwa akiongoza wizara yake, ambako nako kulikuwa na madudu ya ajabu.
Ila ukweli ni kwamba huyu anafanana na yule ambaye watanzania wengi waliomtegemea, na wala si kiongozi halisi aliyengojewa. Kuna baadhi ya watu waligundua mapema kuwa huyu sie lakini wakapiga mioyo yao konde na kusema hebu ngoja tuone kipi kitatokea.
Ukweli ni kwamba watanzania wengi tulimngoja yule mwenye uwezo wa kusimamia misingi na kanuni za kiuongozi ambazo zingemsaidia kufikia "Tanzania mpya" bila kuyumbisha taratibu na misingi ya kiuongozi. Watanzania Hawakutegemea kiongozi "ANAYEPWAYA" kiasi hiki kama huyu wa sasa. Ila kwa kuwa alochaguliwa na wachache, tunaona ngoja tuone mwisho wake.
Tunasikitika kupoteza miaka mingine kwa kufanya majaribio ya kiongozi kama ilivyokuwa awamu iliyopita.