Tanzania hii hii


Inkoskaz

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
6,336
Likes
463
Points
180
Inkoskaz

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
6,336 463 180
Thursday, December 5, 2013

HUZUNIII::WAFANYABIASHARA WAJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI NA WATU WANAODAIWA NI ASKARI JIONEE HAPA

Mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Arumeru.
MASKINI! Wafanyabiashara wawili, wakazi wa Tengeru, wilayani Arumeru mkoani hapa, Joel Zephania Mzava (35) na Gidiona Kija Mfuru (43), wamenusurika kuuawa baada ya kupigwa risasi na watu wanaodaiwa ni askari wa usalama barabarani.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo la kusikitisha lilijiri hivi karibuni kati ya eneo la Msitu wa Mbogo na Karangai wilayani Arumeru, majira ya saa 4:10 asubuhi ambapo wafanyabiashara hao wa kiume walijeruhiwa sehemu mbalimbali. watu hao wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Arumeru wakitibiwa majeraha makubwa waliyoyapata.

Mashuhuda hao walisema kuwa, wafanyabiashara hao walikuwa kwenye gari la mizigo aina Nissan Mitsubishi lenye namba T 481 BGF wakitokea wilayani Simanjiro.

Kushoto ni mmoja wa majeruhi baada ya kupatiwa matibabu.
Akizungumza kwa tabu hospitalini hapo, mmoja wa majeruhi hao ambaye amepoteza kipande kwenye sehemu nyeti baada ya kupigwa risasi katikati ya miguu, alisema waliomba lifti katika gari hilo wakitokea Landabani, Simanjiro walikokuwa wamepeleka biashara zao.
Alisema gari hilo lilikuwa na magunia 45 ya mkaa, mali ya dereva wa gari hilo aliyetajwa kwa jina moja la Dismack, mkazi wa Tengeru.
Mzava alisema walipopewa lifti walikaa mbele na dereva hivyo wakawa watatu.
Alisema walipofika eneo la tukio waliwaona askari wawili wamesimama pembeni ya barabara kwenye kichaka wakiwa na pikipiki aina ya Toyo.
Alisimulia kuwa askari hao waliwasimamisha.

Majeruhi akipatiwa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Arumeru.
Baada ya kusisimama waliwatambua askari hao wanaodaiwa ni wa Kituo cha Mbuguni ambao walimtaka dereva kuwapatia kibali cha kusafirisha mkaa.
Dereva alitoa kibali na risiti za malipo lakini askari hao hawakuridhika na kutaka wapatiwe fedha ndiyo waweze kumwachia vinginevyo wangelipeleke gari kituoni.
Baada ya kuona usumbufu, dereva aliondoa gari ndipo askari mmoja aliwamiminia risasi zaidi ya 20 na kusababisha gari hilo kuserereka na kupinduka huku damu zikiwa chapachapa.Katika tukio hilo wasamaria wema walifika na kutoa msaada kwa majeruhi kwa kutafuta gari na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Usa-River ambako walipatiwa hati ya matibabu (PF-3) kisha wakakimbizwa hospitali hiyo ya Wilaya ya Arumeru.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru, OCD Benedict Mapujila alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa tayari ameshapeleke taarifa kwa mkuu wa polisi mkoani hapa, RPC Liberatus Sabas.
CHANZO GPL
 
Inkoskaz

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
6,336
Likes
463
Points
180
Inkoskaz

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
6,336 463 180
tunakwenda wapi watanzania
 
sotojooo

sotojooo

Member
Joined
Sep 10, 2013
Messages
92
Likes
1
Points
15
sotojooo

sotojooo

Member
Joined Sep 10, 2013
92 1 15
Kweli tunakokwenda watanzania sio pazuri kabisa kwa hali hii
 

Forum statistics

Threads 1,250,661
Members 481,436
Posts 29,740,763