Tanzania hakuishi vituko

Tanzania hakuishi vituko

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,247
Reaction score
888
Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa " If J.K managed to be a president, anyone can be".

Kwa kweli yale maneno niliyapuuzia mwanzoni lakini sasa naanza kuyatafakari kwa kina. Hivi unaweza kuamini kuwa CCM wakiongozwa na J.K mwenyewe walikuwa mstari wa mbele kupinga serikali tatu kwa kigezo cha gharama za uendeshaji, sasa cha kuchangaza eti wanafanya sherehe ya kukabidhi rasimu "inayopendekezwa".

Daily news limeandika ukurasa wa mbele," Heads of state from different countries are among the invited guests to the proposed constitution handover celebrations at Jamhuri stadium tomorrow ". Hivi kweli kwa akili ya kawaida, J.K ana cha kujivunia hata kupoteza pesa za walipa kodi kufanya sherehe ya rasimu? Huo ukereketwa wa gharama kwa mlipa kodi umeenda wapi? Hivi wanajuaje kuwa watanzania wataipigia kura ya NDIYO, au kwa sababu wanajua haitaji kura za ndiyo bali wanahitaji "system" ya kutangaza kuwa ndiyo wameshinda.

Mimi huwa nawaonea huruma wasomi wetu, walioamua kuziba fikra zao kwa njaa zao, Profesa hawawezi kujitofautisha na mwimba taarabu, hana uchambuzi zaidi ya propaganda ya siasa. Kama kweli J.K anayo guts, kwa nini anangangania kuzungumza na "wazee" wa DOdoma na wala hajawahi kukutana na intelectuals ( think tank) ili wambane kwa hoja. Siku nchi hii itakapobadili siasa za kutegemea ignorance ya watu kupitisha mambo, na kuruhusu fikra chanya kufanya kazi, ndipo vita yetu ya umaskini tutaweza kuishinda. Watakachofanya Dodoma ni propaganda kuonyesha kuwa rasimu inakubalika kwa watu.

Haya basi baada ya usanii wenu Dodoma, tukutane kwenye midahalo ya wasomi mtuambie nini mlifanya Dodoma.
 
Maajabu kwakweli, walau wangesubiri kwanza matokeo ya kura ya maoni ndio wajue mbivu na mbichi. wanaanza kufanya sherehe kabla ya siku ya harusi?
 
Ushetwani aliotumia JK kupata madaraka utatuletea matatizo, yale mashetani sasa yanataka kulipwa, yanataka damu, ndio maana JK haishiwi matendo ya ku incite wananchi kughazibika ili apate sababu ya kuwatandika risasi kutuliza majini.

Mtaona mambo ya hovyo sana kutoka kwa huyu Jamaa katika siku hizi chache za mwisho, kitu ambacho hawezi kukubari ni kutoa mwanafamilia wake kafara kwa hao majini hivyo ni lazima wasio wake wafe, na hao ni lazima wafe kwa wingi.

Ndio maana kila siku nasema

My Country Tanzania, My God protect thee.
 
Tutaendelea kudai katiba ya wananchi hata kama hii ya sitta itatangazwa imepita.ngoma bado mbichi kabisa.
 
hiyo inadhibitisha kuwa mipango yote hata ya kutafuta 2/3 rais anahusika ,hata kuchakachua katiba nayo anahusika,kwasababu uwezi kuwanza kushangilia kabla wananchi hajapiga kula, inaamaana hata hizo kula washajipanga jinsi ya kuchakachua.
 
Mkuu hata mimi niliwahi kuelezwa na Diwani mmoja rafiki sana na JK. kuwa, siku moja akiwa na JK. JK. kama vile akashtuka hivi kama vile haamini kama kweli yeye ni Rais! JK. akamwambia kuwa," siamini kama kweli mimi ndye Rais wa Tanzania" Diwani akamuuliza kwa nini Mh.? JK. hakujibu kitu.

Lakini mm sishangai sana maana naamini kuwa watanzania wengi ni vilaza, sasa unategemea nn kama idadi kubwa ya vilaza ikamchagua mwenzao? ni sawa na hapa Mirembe wakachaguana kuwa mmoja ni mwenyekiti na mwingine katibu, unadhani mwenyekiti ataamini kuwa kashinda? ni mpaka a-exercise powers zake!
 
Mkuu samahani lakini

Milembe siku hizi mnatumia mpaka computer/simu?
 
Naona kuna maandalizi kabambe huko Dodoma ya CCM kusherehekea kupitishwa katiba inayopendekezwa. Nasikia wamealikwa wageni mbalimbali ndani na nje ya nchi na sherehe inafanyikia uwanja wa Jamuhuri. Sijaelewa hasa nini wanasherehekea maana katiba bado haijapatikana!

Je ni kweli CCM wanafurahia uzuri wa hii katiba inayopendekezwa au wanafurahia kufanikiwa kuchomoa vipengele vilivyokuwa mwiba kwao kwenye rasimu ya Warioba? Ni nini hasa kiko nyuma ya CCM kushangilia na kujipongeza kabla mtoto hajazaliwa? Ni kweli wameguswa na katiba kujibu kero na matakwa ya wananchi? Je ikitokea katiba hii isipopita zanzibar watasema nini? Au haya wanayafanya kama mbinu ya kuipigia kampeni hiyo katiba yao?

Nia aibu katiba iliyopatikana kwa mizengwe na kulazimisha bado inaendelea kulazimishwa kuonekana inaungwa mkono wakti kiuhalsia ni HAPANA.

Nini kilichopo nyuma ya shamrashmara za CCM kabla shuguhuli haijakamilika?
 
Inaonekana ccm wamejihakikishia kura za wananchi hata kabla hizo kura hazijapigwa................maajabu hayakomi nchi hii.
 
Unaona anachofanya kiNANA anapita kule ambako bado wanaabubu Bendera ya CCM mimi labda niseme jambo moja ccm wanauhakika nawanachofanya tupo hapa tunapeana MOYO lkn nawahakikishia labda JK aamue kuizima hiyo RSIMU baada ya kelele nyingi.za wadau lkn akiweka mtaani itapita kwa kiSHINDO wenyewe wanaitaga nasema hivyo kwa sababu gani Watu wanaojitambua cku yakupiga KURA hawaendi wapo nyuma ya Keyboard na Tv,,,,!
 
msituvuruge akili hapa hakuna cha ccm wala ukawa wanaojali hela ya mlipa kodi. Hao ukawa wanaolalamikia gharama ndio waliopendekeza kura ya maoni ifanyike baada ya uchaguzi wa rais. Hii inamaana uchaguzi wa rais ufanyike mara mbili ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Kura ya maoni haina tofauti na kura ya kumchagua rais. Kila mtanzania alijiandikisha kupiga kura lazima apige kura. Gharama ya kura ya maoni haina tofauti na gharama ya kura ya kumchagua rais.

Kwahiyo wapinzani wasitudanganye wanajali gharama. Wanapiga kelele pale jambo linalotaka kufanyika hawalitaki.
 
Naona kuna maandalizi kabambe huko Dodoma ya CCM kusherehekea kupitishwa katiba inayopendekezwa. Nasikia wamealikwa wageni mbalimbali ndani na nje ya nchi na sherehe inafanyikia uwanja wa Jamuhuri. Sijaelewa hasa nini wanasherehekea maana katiba bado haijapatikana!

Je ni kweli CCM wanafurahia uzuri wa hii katiba inayopendekezwa au wanafurahia kufanikiwa kuchomoa vipengele vilivyokuwa mwiba kwao kwenye rasimu ya Warioba? Ni nini hasa kiko nyuma ya CCM kushangilia na kujipongeza kabla mtoto hajazaliwa? Ni kweli wameguswa na katiba kujibu kero na matakwa ya wananchi? Je ikitokea katiba hii isipopita zanzibar watasema nini? Au haya wanayafanya kama mbinu ya kuipigia kampeni hiyo katiba yao?

Nia aibu katiba iliyopatikana kwa mizengwe na kulazimisha bado inaendelea kulazimishwa kuonekana inaungwa mkono wakti kiuhalsia ni HAPANA.

Nini kilichopo nyuma ya shamrashmara za CCM kabla shuguhuli haijakamilika?

mkuu sasa kesho ndio utashuhudia uzuzu wa watanzania,uwanja utajaa hadi kutapika na watakuwa wanashangilia kama mazuzu!!!
_we utashangaa kesho nakumbia utashangaa watz wakishangilia katiba ya kifo chao na umasikini wao na wa vizazi vyao!!!
_ kwanini hatujasomaaaaa
 
wanafanya sherehe katiba hatujaipitisha kuna haja gani ya kuipitisha. Hapo ni kiini macho,

Fikiria sikuwatakaposema sasa imepitisha tayari kwa matumizi what will happen !
 
Kwa mtazamo wako ulitaka kura ya maoni ifanyike siku moja na Uchaguzi wa Rais siyo? You are not serious, ndivyo sheria ya mabadiliko ya katiba inavyosema?
msituvuruge akili hapa hakuna cha ccm wala ukawa wanaojali hela ya mlipa kodi. Hao ukawa wanaolalamikia gharama ndio waliopendekeza kura ya maoni ifanyike baada ya uchaguzi wa rais. Hii inamaana uchaguzi wa rais ufanyike mara mbili ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Kura ya maoni haina tofauti na kura ya kumchagua rais. Kila mtanzania alijiandikisha kupiga kura lazima apige kura. Gharama ya kura ya maoni haina tofauti na gharama ya kura ya kumchagua rais.

Kwahiyo wapinzani wasitudanganye wanajali gharama. Wanapiga kelele pale jambo linalotaka kufanyika hawalitaki.
 
Rais dhaifu anatengeneza serikali legheleghe. Lkn waliomchagua yaani watz ni dhaaifu zaidi coz ni waongeaji Vila vitendo
 
Rais dhaifu anatengeneza serikali legheleghe. Lkn waliomchagua yaani watz ni dhaaifu zaidi coz ni waongeaji Vila vitendo
Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa JK na wabunge wa ccm huu upuuzi wa ccm hauvumiliki tena lazima tujiandae kuzunguka nchi nzima kuwapa wananchi elimu ya kuipigia kura ya HAPANA hiyo rasimu ya ccm
 
Back
Top Bottom