Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa " If J.K managed to be a president, anyone can be".
Kwa kweli yale maneno niliyapuuzia mwanzoni lakini sasa naanza kuyatafakari kwa kina. Hivi unaweza kuamini kuwa CCM wakiongozwa na J.K mwenyewe walikuwa mstari wa mbele kupinga serikali tatu kwa kigezo cha gharama za uendeshaji, sasa cha kuchangaza eti wanafanya sherehe ya kukabidhi rasimu "inayopendekezwa".
Daily news limeandika ukurasa wa mbele," Heads of state from different countries are among the invited guests to the proposed constitution handover celebrations at Jamhuri stadium tomorrow ". Hivi kweli kwa akili ya kawaida, J.K ana cha kujivunia hata kupoteza pesa za walipa kodi kufanya sherehe ya rasimu? Huo ukereketwa wa gharama kwa mlipa kodi umeenda wapi? Hivi wanajuaje kuwa watanzania wataipigia kura ya NDIYO, au kwa sababu wanajua haitaji kura za ndiyo bali wanahitaji "system" ya kutangaza kuwa ndiyo wameshinda.
Mimi huwa nawaonea huruma wasomi wetu, walioamua kuziba fikra zao kwa njaa zao, Profesa hawawezi kujitofautisha na mwimba taarabu, hana uchambuzi zaidi ya propaganda ya siasa. Kama kweli J.K anayo guts, kwa nini anangangania kuzungumza na "wazee" wa DOdoma na wala hajawahi kukutana na intelectuals ( think tank) ili wambane kwa hoja. Siku nchi hii itakapobadili siasa za kutegemea ignorance ya watu kupitisha mambo, na kuruhusu fikra chanya kufanya kazi, ndipo vita yetu ya umaskini tutaweza kuishinda. Watakachofanya Dodoma ni propaganda kuonyesha kuwa rasimu inakubalika kwa watu.
Haya basi baada ya usanii wenu Dodoma, tukutane kwenye midahalo ya wasomi mtuambie nini mlifanya Dodoma.