Hao waliolipa na kurudi chuoni wametoka wapi? Je wao sio watanzania? Unapaswa kelewa kuwa kuna watanzania wa uwezo tofauti tofauti na msimamo wa serikali ni kuwasaidia wale wanaoshindwa, kama wewe ulivyoshindwa na ikakusaidia. Ninachopinga mimi ni kulazimishana kuamini kuwa watanzania wote hawawezi kujlipia.
Tupende tusipende elimu ya bure ilikwisha na utawala wa Mwalimu, wakati huo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu walikuwa hawajai kiganjanjani.Leo vyuo vikuu tele, na wanafunzi tele na wote wanataka kusomeshwa na kodi ya wananchi.
Sioni hilo likitendeka leo au kesho.
Tatizo la serikali ni kutolifafanua hili kuwa kuwasomesha watu bure kumefikia mwisho, wawe ni watoto wa wa mkulima ,mafanyakazi au kibopa.
Sasa hivi kinachofanyika ni ujanja ujanja tu wa wanafunzi wengine wapewe mikopo na wengine wakose.Sera ya kuwa kila mwanafunzi lazima alipie karo ianzishwe na muundo wa mikopo usioeleweka sasa usitishwe.Nchi nyingine kuna mtindo wa scholarship kwa category fulani ya wanafunzi waliofanya vizuri sana na ambao serikali inaona umuhimu wa kuwa retain kwa kuwalipia ili wawe wataalam/viongozi wa nchi.
Hapa criteria ni performance tu na hii inaongeza ushindani katika elimu.
Ndugu yangu, watanzania walio wengi wanamaisha duni, kipato chini ya dola moja...ukiangalia kwa makini suala hili tunataka kujenga tabaka la masikini na wenye nacho, serikali haishindwi kuwalipia hao wasio na uwezo, angalia ni kiasi gani tunateketeza pato la taifa kwa mambo yasiyo na msingi? Ufisadi ? chaguzi? the list is very wrong...wenye uwezo sawa wachangie wale akina Kayumba nao???
Kichwangumu unaongea theory nyngi lakini practice iko tofauti na hizo theory. Ukimleta mwanafunzi aliyepeleka hati ya nyumba bodi ya mikopo mlete hapa. Hakuna mtu anayelazimishwa kupeleka hati ya nyumba ili apewe mkopo. wala hakuna collateral yoyote inayohitajika ili kuidhinisha mkopo.
Wanafunzi hawa hawapingi utekelezaji, wanapinga sera. wao wanataka flat rate 100% kwa wanafunzi wote na sera haisemi hivyo.
Hao waliolipa na kurudi chuoni wametoka wapi? Je wao sio watanzania? Unapaswa kelewa kuwa kuna watanzania wa uwezo tofauti tofauti na msimamo wa serikali ni kuwasaidia wale wanaoshindwa, kama wewe ulivyoshindwa na ikakusaidia. Ninachopinga mimi ni kulazimishana kuamini kuwa watanzania wote hawawezi kujlipia.
Exactly my sentiments!!!! Na ndio mfumo uliokuwa unatumika miaka yote mpaka ilipokuja hii bodi ya mikopo na mambo shaghalabaghala ya 40%, 60% and 100%.
Criteria ya kutoa udhamini kwa mwanafunzi dunia nzima ni moja tu, kufaulu vizuri! Serikali itoe mikopo na udhamini kwa wanafunzi waliofaulu vizuri bila kujali mtoto wa mkulima au wa tajiri. Haiingii akilini eti kwa sababu mimi baba yangu ana uwezo wa kifedha halafu nimefaulu vizuri ninyimwe mkopo kisa nilisoma Academy.
Serikali isomeshe wanafunzi kwa 100% kwa kuzingati viwango vyao vya kufaulu mpaka pale uwezo wake unapoishia!
Kwahiyo ambao hawajalipa ni masikini na ambao wamelipa wanauwezo hivyo basi serikali itawapa asilimia 100% hawa ambao hawajalipa?
Umesahau kuwa kabla ya kuja kwa Bodi ya mikopo wanafunzi waliosoma kwenye vyuo binafsi kama Tumaini na vingine hawakupewa msaada wowote na serikali.Unadhani ni sahihi kwa serikali kutowasaidia wanafunzi wa Tumaini, SAUT, MUM, IMTU, Kairuki etc. ? Au unadhani walioenroll kwenye hivyo vyuo hawajafaulu???
Hoja yangu ya hapa ni kufaulu na kupata admission kwenye Chuo chochote kile kinachotambilika, kiwe cha serikali ya cha binafsi. Ila viwango vya kufaulu ndicho kiwe kigezo cha kumpa mwanafunzi mkopo na si kipato chake! Hayo mambo ya kutathmini uwezo wa kifedha wa mzazi/mlezi wa mwanafunzi ili kujua anaweza kuchangia kiasi gani yanatuletea matatizo makubwa.
Hilo limeelezewa wazi na waziri. Wale wote walioshindwa kulipa wapeleke appeal wizarani for reassessment. Assessment hiyo ndio itatoa jibu kama walipiwe 100% au la. Sera kama ilivyo inamconsider kila mtanzania. wanaofanya utekelezaji uwe mgumu ni wanafunzi wanaotoa taarifa zisizo sahihi. Hivyo basi adui wa mwanafunzi masikini ni mwanafunzi mwenye uwezo aliyedanganya kuwa hana uwezo.Tatizo si sera.
Yes, serikali uwezo wake mdogo sana.
Mashangingi ya bei mbaya 700 kwa mwaka mmoja. Kukodisha ndege mbovu za ATCL, zilizopelekwa Kiwira kimya kimya, za safari, za vikao, washa, seminar, kongamano................ Kweli serikali uwezo wake mdogo, AMEN!!
Hilo limeelezewa wazi na waziri. Wale wote walioshindwa kulipa wapeleke appeal wizarani for reassessment. Assessment hiyo ndio itatoa jibu kama walipiwe 100% au la. Sera kama ilivyo inamconsider kila mtanzania. wanaofanya utekelezaji uwe mgumu ni wanafunzi wanaotoa taarifa zisizo sahihi. Hivyo basi adui wa mwanafunzi masikini ni mwanafunzi mwenye uwezo aliyedanganya kuwa hana uwezo.Tatizo si sera.
Nani mwenye wajibu wa kusema huyu kadanganya au hajadanganya? Mimi au wewe au serikali(bodi)?
Mkopo sio zawadi. Lengo la mkopo ni kuwawezesha wale wasiafford kujilia waweze kusoma. Unaposema mkopo utolewe based on exams results utakuwa sahihi iwapo tu waliofaulu wote watashindwa kujilipia. Iwapo mtu amefaulu na anauwezo wa kujilipia kwa nini umkopeshe. Kumbuka huu ni mkopo sio zawadi.
Serikali na Chuo wanatumia vigezo gani kujua kina nani wana uwezo na kina nani hawana uwezo?
Board ya mikopo pia inashindwa kujua nani tajiri nani maskini kwa sababu watanzania hawawezi ku-be-identified.. yaaani hawana vitambulisho vya kitaifa (National Identity Card) ambavyo vinginetunza database, ingekuwa rahisi kujua baba yako anafanya kazi gani? analipa kodi kiasi gani, na pato lake la mwaka kiasi gani? Bila hilo hata board ya mikopo inalaumia kijinga tu.