Tanzania haitabadilika katika karne hii au ijayo

marine 1

Member
Jul 29, 2015
60
67
Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR limekamilika, tena kwa mafanikio makubwa.

Pamoja na wananchi kutahadharishwa kutunza kadi zao za kupiga kura, Tahadhari hiyo imekuwa kama kumpigia mbuzi jitaa.

Jana baada ya kutoka kazini niliamua kupita sehemu mbalimbali kuongelea vugu vugu la kisiasa. Katika stori likzjitokeza swala la wajumbe wa nyumba kumi kukusanya kadi za kupiga kura.

Kwamba eti wajumbe wanapita kukusanya kadi na kama sio kadi basi wanaandikisha majina na namba za kadi kwa siri. Nikauliza wanazichukua kadi ili iweje? sikupata majibu.

Ajabu ni kwamba hata baadhi ya walizotoa namba hizo za kadi ni wasomi tu. Wanajitetea eti wao wanajua ni mchezo mchafu na kwamba wajumbe watalipwa kwa kukusanya namba hizo, ila wao haliwajalishi kwani walijiandikisha ili kupata kitambulisho kwaajili ya shughuli zao nyingine na HAWATAPIGA KURA.

Kwa kweli nimechoka na kupoteza imani na watanzania wenzangu
 
Watanzania sisi ni majinga sana!!,na yote hiyo ni kwasababu hatukupata Uhuru wetu kwa mtutu wa bunduki,Angali wenzetu Burundi kanchi kadogo na maskini walivyo makini,Sisi ngoja tuendelee kupigika maana ujinga ni wetu na Tutaangamia sana kwa kukosa maarifa.
 
Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR limekamilika, tena kwa mafanikio makubwa.

Pamoja na wananchi kutahadharishwa kutunza kadi zao za kupiga kura, Tahadhari hiyo imekuwa kama kumpigia mbuzi jitaa.

Jana baada ya kutoka kazini niliamua kupita sehemu mbalimbali kuongelea vugu vugu la kisiasa. Katika stori likzjitokeza swala la wajumbe wa nyumba kumi kukusanya kadi za kupiga kura.

Kwamba eti wajumbe wanapita kukusanya kadi na kama sio kadi basi wanaandikisha majina na namba za kadi kwa siri. Nikauliza wanazichukua kadi ili iweje? sikupata majibu.

Ajabu ni kwamba hata baadhi ya wzliotoa namba hizo za kadi ni wasomi tu. Wanajitetea eti wao wanajua ni mchezo mchafu na kwamba wajumbe watalipwa kwa kukusanya namba hizo, ila wao haliwajalishi kwani walijiandikisha ili kupata kitambulisho kwaajili ya shughuli zao nyingine na HAWATAPIGA KURA.

Kwa kweli nimechoka na kupoteza imani na watanzania wenzangu.

Ni wapi huko mkuu???.
 
Back
Top Bottom