comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2013 ya shirika la OECD ambayo 27/7 Wallstreet waliinukuu, Tanzania haionekani katika orodha katika nchi kumi zinazoongoza kuwa na wasomi duniani. Tunapozungumzia wasomi, ni ile idadi ya watu waliomaliza elimu ya vyuo vikuu na walau mtu kua ana digrii moja.
Namba 1:
Russian Federation.
Nchi hii inayoongozwa na Rais Vladimir Putin ina jumla ya watu Milioni 144.1 (2015) kwa mujibu wa Banki ya dunia na ina jumla ya kiwango cha elimu ya chuo kwa asilimia 53.5.
Namba 2:
Canada.
Nchi hii iliyopo Kaskazini Amerika yenye jumla ya watu 35.85 million kwa sensa ya mwaka (2015 ) Kutoka Benki ya dunia , Canada ina kiwango cha elimu ya chuo kwa 51.3%.
Namba 3:
Japan.
Kwa mujibu wa Benki ya dunia kwa mwaka 2015, Japan ina watu wapatao milioni 127, na ni nchi inayoongoza kwa Teknolojia na Sayansi duniani. Japan ina kiwango cha elimu ya chuo kwa 46.4%.
Namba 4:
Israel
Nchi ya Israel ina kiwango cha elimu ya chuo kwa jumla ya 46.4%.
Namba 5:
United States
Nchi hii iliyopo katika bara a Amerika ipo katika nafasi ya tano ikiwa na kiwango cha elimu ya chuo 42.5%.
Namba 6:
Korea
Sensa ya mwaka 2015 chini ya Benki ya dunia ilibainisha uwepo wa watu wapatao milioni 50.62 nchini Korea, ikiwa ina kiwango cha elimu ya chuo 40.4%.
Namba 7:
United Kingdom
Ikiwa ipo chini ya utawala wa Malkia Elizabeth wa pili na Waziri Mkuu Theresa May, Nchi hii yenye wakazi wapatao milioni 65.14 ina kiwango cha elimu ya chuo 39.4%.
Namba 8:
New Zealand
Nchi hii iliyopo kusini mashariki mwa Bahari ya Pacific,imeshika nafasi ya nane ikiwa na wakazi wapatao milioni 4.596. New Zealnd ina kiwango cha elimu ya chuo 39.3%.
Namba 9:
Finland
Nchi hii inapatikana Kaskazini mwa Bara la Ulaya, huku lugha zake zikiwa ki Finishh na Kisweden. Taifa hili lina kiwango cha elimu ya chuo 39.3%.
Namba 10:
Australia
Ikiwa imezungukwa na Bahari ya Hindi pamoja na Pacific, Australia ina wakazi wapatao miloni 23.75 kwa mujibu wa Benki ya Dunia mwaka 2015. Kiwango cha elimu ya chuo ni asilimia 38.3.