Tanzania haikuhitaji Rais mkorofi, ilihitaji Rais mwenye msimamo thabiti

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Ndugu zangu wadanganyika nawasalimu wote salam za heri ya mwaka mpya.

Kwanza niweke tu wazi kwamba, mimi sijawahi kukubaliana na Mh Raisi tangu kipindi cha kampeni na hata alipoapishwa na kuanza wajibu wake. Sio kwasababu ya maumbile yake la. Kipindi cha kampeni nilimchukia kwa kauli na matendo yake aliyokua akiyafanya maana yaliashiria kitu kibaya mbeleni, lakini Wadanganyika wengi hawakuelewa waliendelea kupiga makofi na hatima kumchagua.

Tendo la kupiga push-ups mbele za watu ukiwa na ordinary thinking unaweza ukadhani ni tendo la kawaida au la kufurahisha watazamaji lakini mimi nasema tangu alipopiga push-ups nilipata somo anaenda kuwa mtu wa aina gani. Somo nililolipata ni kwamba alikua akiwaambia watanzania kwa vitendo kwamba mimi sitaongoza nchi kwa kufwata kanuni na taratibu bali nitaiongoza kwa kutumia nguvu na mabavu. "ukitaka kuwa bouncer moja ya mazoezi ni kupiga push-ups''

Kitendo cha kuwaambia wananchi kwamba endapo wakishinda watu wa upinzani nchi itageuka kuwa libya kilimaanisha kwamba endapo angeshindwa asingekubali kushindwa na angesababisha vurugu ambazo zingeleta machafuko.

Tangu amekua Raisi amekua akifanya mambo mengi lakini mengi yanathibisha kile kitendo cha kupiga push-ups, na ndo maana hata kutumbua haifwati taratibu na wanaotumbuliwa ni wale ambao hata kama wako chama kimoja ila wana mtazamo tofauti na yeye "utumbuaji wa visasi" kwanini nasema hivyo kwasabu, kama kweli angetumbua waliotumia vibaya madaraka na mali za umma leo hii Chenge hangekua mwenyekiti wa bunge, Mwigulu asingekua waziri ma mambo ya ndani, Mwakiyembe asingekua waziri wa katiba sheria maana, hawa wote ni mapapa wa wale dagaa wote waliotumbuliwa bandari na TRA.

Tanzania ilihitaji mtu mwenye "msimamo thabiti" namaanisha nini? namaanisha mtu mwenye ufahamu na mambo ya kijamii, kisiasa, kiitikadi, kiuchumi, kitamaduni na kisayansi, ambaye anauwezo wa kusimamia jambo analolijua kwa weledi na kwa kufwata katiba na kanuni.

Anachofanya huyu bwana ni sawa na familia ina watoto wawili, mmoja mkorofi na mwingine ana msimamo na mambo ya msingi ya maendeleo. Mtoto mkorofi akiamua kuchara bakora kila mtu nyumbani awe baba, mama, kaka, dada, anafanya hivyo bila uoga na bila kujihoji endapo yuko sahihi au la. lakini mtoto mwenye msimamo ana uwezo wa kumwambia baba, mama, mjomba,shangazi, kaka , dada, jambo hili halitafanyika mnavyotaka na mlivyozoea litafanyika kwa utaratibu ntakao wapa mimi, akiwapa sababu za msingi za kufanya anachokifanya na akatekeleza adhma yake na kuiletea familia maendeleo.

Tanzania haikuhita mtu mnafiki, wala muoga bali ilihitaji mtu mwenye ufahamu wa uchumi, elimu, afya, siasa na mambo ya kijamii na avisimamie hivyo kwa weledi bila kujali itikadi, tofauti za kisiasa wala kijamii. Lakini bahati mbaya sana tumempata mtu ambaye hana chembe ya ufahamu wa hayo mambo bali mkorofi ambaye ukimgusa kidogo tu lazima utumbuliwe hadharani.

Hii sio afya kwa nchi kubwa kama Tanzania kuongozwa na mtu ambaye anaweza kuwaambia wanananchi mkiitegemea serikali 'mwafwa' alafu tunasema tumepata kiongozi tuliyemtakaa!!!
kiongozi bora hapimwi kwa uawezo wa kutumia muda mwingi kuongelea vitisho na mabavu bali hupimwa kwa uwezo wa kutumia ufahamu wake kuwatoa watu sehemu flani kuwapeleka sehemu flani ya maendeleo hata kama ni mpole kiasi gani huyo ndiye kiongozi.

"Samahani sana Mh Magufuli lakini umekua ukisema msema kweli ni mpenzi wa Mungu basi, na wewe ukubali ukweli huu kama ulivyo maana mimi nimpenzi wa Mungu" TUNAHITAJI KIONGOZI MWENYE MSIMAMO THABITI SIO MKOROFI.
 
Sasa kama hujawai kukubaliana nae unadhani itaona ata jema lake? We endelea na misimamo yako hiyo hiyo ila kumbuka na kubali kua huyu ndio rais wako hadi 2020 na 2025 Mungu akijalia tutampa tena maana katengeneza nchi... keep it up mkuu
 
Matamko yake mimi yananiacha hoi kabisa, kauli zake kwa wananchi wanyonge zinatofautiana kila kukicha, kila mtu atabeba mzigo wake, mkiitegemea Serikali mwafwaa, hakuna Serikali inayowajengea wananchi wake nyumba waliopatwa na majanga ya asili, hapa kwa kweli ccm walichemka sana, uzuri inakula na upande wa ccm
 
Sasa kama hujawai kukubaliana nae unadhani itaona ata jema lake? We endelea na misimamo yako hiyo hiyo ila kumbuka na kubali kua huyu ndio rais wako hadi 2020 na 2025 Mungu akijalia tutampa tena maana katengeneza nchi... keep it up mkuu

Yaani napishana na huyu bwana kila siku. sasa undhani hili la kuwaambia wananchi mwafwa si ndo anazidi kunipa maswali juu ya uwezo wake wa kufikiri.
 
mtanena sana kwa lugha na kutoa njozi na utabiri sana, saanaaa.

Tafsiri ya kunena kwa lugha na utabiri unaijua? Au umeona siku ispite kabla hujaandika chochote? basi mara mojamoja ruhusu na ubongo ufanye kazi.
 
Yaani napishana na huyu bwana kila siku. sasa undhani hili la kuwaambia wananchi mwafwa si ndo anazidi kunipa maswali juu ya uwezo wake wa kufikiri.
Nchi TANZANIA.
Rais ni JOHN POMBE MAGUFULI.
Chama tawala ni CCM.
NB:Km hupendi ama kufa au hama nchi.
 
Site clean up ni muhimu sana, hii miaka mitano usitegemee zaidi bali 2020 site itakuwa safi kwa kuanza ujenzi!
 
Nchi ilibiendelee lazima wananchi wake waelimike sio kwa eimu ya darasani tu hatakupambanua mambo.wacha tuisome namaba nadhani uchaguzi ujao tutafanya vzr na kuchagua kiongozi makini kama huyu maana watz wameelimika sasa
 
tunahitaji rais mwenye utu. sijasema kama huyu hana utu, najua ana utu.
 
jiwe lililo mponda john ni lile tu na lililompiga moses tofauti ni mda na nguvu za urushaji wa hayo mawe
 
Kwakweli tuombe tu tufike salama yani jpm amalize muda wake na kutuacha salama.Kwani bila maombi nchi hii itazama sababu ni ngumu nchi kwenda kwa kutegemea mawazo ya chuki na visasi
 
Wana wa Israel walipokuwa jangwani kuelekea kanaani walimshutumu Moses na kukufuru kuwa bora hata utumwani misri, hebu tujibidiishe na mambo yetu tuachane na misisimko ya siasa
 
Ndugu zangu wadanganyika nawasalimu wote salam za heri ya mwaka mpya.

Kwanza niweke tu wazi kwamba, mimi sijawahi kukubaliana na Mh Raisi tangu kipindi cha kampeni na hata alipoapishwa na kuanza wajibu wake. Sio kwasababu ya maumbile yake la. Kipindi cha kampeni nilimchukia kwa kauli na matendo yake aliyokua akiyafanya maana yaliashiria kitu kibaya mbeleni, lakini Wadanganyika wengi hawakuelewa waliendelea kupiga makofi na hatima kumchagua.

Tendo la kupiga push-ups mbele za watu ukiwa na ordinary thinking unaweza ukadhani ni tendo la kawaida au la kufurahisha watazamaji lakini mimi nasema tangu alipopiga push-ups nilipata somo anaenda kuwa mtu wa aina gani. Somo nililolipata ni kwamba alikua akiwaambia watanzania kwa vitendo kwamba mimi sitaongoza nchi kwa kufwata kanuni na taratibu bali nitaiongoza kwa kutumia nguvu na mabavu. "ukitaka kuwa bouncer moja ya mazoezi ni kupiga push-ups''

Kitendo cha kuwaambia wananchi kwamba endapo wakishinda watu wa upinzani nchi itageuka kuwa libya kilimaanisha kwamba endapo angeshindwa asingekubali kushindwa na angesababisha vurugu ambazo zingeleta machafuko.

Tangu amekua Raisi amekua akifanya mambo mengi lakini mengi yanathibisha kile kitendo cha kupiga push-ups, na ndo maana hata kutumbua haifwati taratibu na wanaotumbuliwa ni wale ambao hata kama wako chama kimoja ila wana mtazamo tofauti na yeye "utumbuaji wa visasi" kwanini nasema hivyo kwasabu, kama kweli angetumbua waliotumia vibaya madaraka na mali za umma leo hii Chenge hangekua mwenyekiti wa bunge, Mwigulu asingekua waziri ma mambo ya ndani, Mwakiyembe asingekua waziri wa katiba sheria maana, hawa wote ni mapapa wa wale dagaa wote waliotumbuliwa bandari na TRA.

Tanzania ilihitaji mtu mwenye "msimamo thabiti" namaanisha nini? namaanisha mtu mwenye ufahamu na mambo ya kijamii, kisiasa, kiitikadi, kiuchumi, kitamaduni na kisayansi, ambaye anauwezo wa kusimamia jambo analolijua kwa weledi na kwa kufwata katiba na kanuni.

Anachofanya huyu bwana ni sawa na familia ina watoto wawili, mmoja mkorofi na mwingine ana msimamo na mambo ya msingi ya maendeleo. Mtoto mkorofi akiamua kuchara bakora kila mtu nyumbani awe baba, mama, kaka, dada, anafanya hivyo bila uoga na bila kujihoji endapo yuko sahihi au la. lakini mtoto mwenye msimamo ana uwezo wa kumwambia baba, mama, mjomba,shangazi, kaka , dada, jambo hili halitafanyika mnavyotaka na mlivyozoea litafanyika kwa utaratibu ntakao wapa mimi, akiwapa sababu za msingi za kufanya anachokifanya na akatekeleza adhma yake na kuiletea familia maendeleo.

Tanzania haikuhita mtu mnafiki, wala muoga bali ilihitaji mtu mwenye ufahamu wa uchumi, elimu, afya, siasa na mambo ya kijamii na avisimamie hivyo kwa weledi bila kujali itikadi, tofauti za kisiasa wala kijamii. Lakini bahati mbaya sana tumempata mtu ambaye hana chembe ya ufahamu wa hayo mambo bali mkorofi ambaye ukimgusa kidogo tu lazima utumbuliwe hadharani.

Hii sio afya kwa nchi kubwa kama Tanzania kuongozwa na mtu ambaye anaweza kuwaambia wanananchi mkiitegemea serikali 'mwafwa' alafu tunasema tumepata kiongozi tuliyemtakaa!!!
kiongozi bora hapimwi kwa uawezo wa kutumia muda mwingi kuongelea vitisho na mabavu bali hupimwa kwa uwezo wa kutumia ufahamu wake kuwatoa watu sehemu flani kuwapeleka sehemu flani ya maendeleo hata kama ni mpole kiasi gani huyo ndiye kiongozi.

"Samahani sana Mh Magufuli lakini umekua ukisema msema kweli ni mpenzi wa Mungu basi, na wewe ukubali ukweli huu kama ulivyo maana mimi nimpenzi wa Mungu" TUNAHITAJI KIONGOZI MWENYE MSIMAMO THABITI SIO MKOROFI.

tuliitaji raisi anayefuata katiba nasheria
 
Kwa sababu bado tunaye miaka mitatu na ushee, mbele tumuombee apate hekima na busara
 
Back
Top Bottom