‘Tanzania haiko kiwango kizuri usalama mtandao’

‘Tanzania haiko kiwango kizuri usalama mtandao’

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
WATAALAMU wa ukaguzi na usimamizi wa mitandao nchini wameshauriwa kujenga uelewa wa kutosha kwa jamii ili kuweza kujua maana halisi ya usalama wa mtandao na hata kuwa na mfumo wa kulinda mifumo mingine ya kimtandao.

Hata hivyo, imeelezwa Tanzania haiko katika kiwango kizuri cha usalama katika mtandao, hivyo kuna uhitaji wa kuboresha mifumo na kuwa ni jambo endelevu litakalowezesha mitandao kuwa salama.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Rais wa Chama cha watalaamu wabobezi wa mitandao (ISACA Tanzania), Neemayani Kaduma katika warsha ya kujenga ufahamu wa namna ya kutumia mitandao katika njia sahihi na yenye usalama.

Warsha hiyo inawakutanisha wataalamu hao wa mitandao, ili kuangalia jinsi hata kwa watumiaji wa mtandao wasiokuwa na teknolojia kuweza kupata elimu kuhusu usalama katika mtandao.

Akiwasilisha mada katika warsha hiyo kuhusu usalama katika mtandao, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi alisema kwa ujumla suala la mtandao linahusiana kwa karibu na maisha, uchumi na hata maendeleo nchini.

Aidha alisema kwa vile nchi inajielekeza katika uchumi wa viwanda na kipato cha kati, usalama katika mtandao ni muhimu. Kuhusu kiwango cha usalama wa mtandao nchini, alinukuu takwimu za Shirikisho la Teknolojia la Ulimwengu (ITU) kwamba Tanzania ifanye jitihada ili kuinukia katika kiwango cha juu cha usalama ambapo kwa sasa Mauritius inaongoza na Tanzania ikiwa na alama 0.317.

Makamu wa Rais wa ISACA Tanzania, Venance Mwolo alisema kujenga uelewa kwa jamii ni jambo muhimu kwa kuwa wahalifu wa mitandaoni wanazidi kujifunza mbinu mpya mara kwa mara.


CHANZO: Habari Leo
 
Back
Top Bottom