TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,674
- 28,789
mkuu wakati mwingine swali hili huwa najiuliza mara kwa mara kwamba, hivi wahusika wa mipango miji hawa wanopitisha vibali vya ujenzi wa majengo haya kweli hawajaligundua tatizo hili?Tena hivi vioo vinaongeza joto hata nje ya jengo lenyewe. Ukipita pale Quality Plaza, njia panda ya Chan'gombe wakati wa jua kali utahisi joto linaongezeka.
Tena hivi vioo vinaongeza joto hata nje ya jengo lenyewe. Ukipita pale Quality Plaza, njia panda ya Chan'gombe wakati wa jua kali utahisi joto linaongezeka.
Inaonyesha kuwa vinafanya kazi yake, vina reflect jua hivyo kuzuia ndani ya jengo kupata joto hii inapunguza gharama za AC.
Tena hivi vioo vinaongeza joto hata nje ya jengo lenyewe. Ukipita pale Quality Plaza, njia panda ya Chan'gombe wakati wa jua kali utahisi joto linaongezeka.
Mkuu, ni kweli vinafanya kazi yake, vina reflect jua. Lakini kazi vinayoifanya ni ya kuamisha tatizo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Kwa hiyo majengo ambayo hayana reflectors za miale ya jua ambayo yako karibu na jengo hilo la vioo yatalazimika kutumia AC maradufu.
ERB wenyewe wamejaa Civil and Structural Engineers, hawajui kutofautisha kati ya Computer Engineer na Electrical Engineer yaani ni kazi kweli kweli. Anyway, bado tuna changamoto nyingi na bahati mbaya baada ya mradi kuisha sijui kama huwa tunarudi kuangalia kama jengo halisababishi usumbufu wowote ndani au nje tofauti na ilivyokusudiwa.@ WA-UKENYENGE: Kweli kabisa ishu imekaa kitaalamu kabisa, kwa jinsi ulivyofafanua.
Nimewalenga hasa madesigner kuhusu hili kwa sababu wao ndio wanajua kabisa kuwa bidhaa wanayomwandalia mteja ina ubora kiasi gani kwa kuzingatia matumizi ya nishati. Pamoja na matakwa ya mteja mimi nadhani designers wetu wanayonafasi ya kumshauri mteja vyema, juu ya bidhaa anayohitaji kwa manufaa ya mteja mwenyewe na afya ya uchumi wa taifa.
Pia Bodi ya wahandisi-ERB (nikiamini iko karibu na designers wetu) inalojukumu la kuhamasisha washikadau wote katika sekta ya Ujenzi wa majengo hapa nchini namna bora ya kujenga majengo yenye ufanisi katika matumizi ya nishati ya umeme.
ERB wenyewe wamejaa Civil and Structural Engineers, hawajui kutofautisha kati ya Computer Engineer na Electrical Engineer yaani ni kazi kweli kweli. Anyway, bado tuna changamoto nyingi na bahati mbaya baada ya mradi kuisha sijui kama huwa tunarudi kuangalia kama jengo halisababishi usumbufu wowote ndani au nje tofauti na ilivyokusudiwa.
Inshu imekaa kitaalamu kidogo!! Msanifu jengo ni msanifu jengo, Lighting A/c designer ni kitu kingine kabisa. Na mlaji/mteja naye ni mwingine!
Tukianza kwa msanifu wa jengo: Anadesign kulingana na requirements za mteja wake kwa kufuata nini mteja anataka na nini hataki kutokana na matumizi ya jengo husika na uwezo wa mteja, tukija kwa mtu wa umeme! atapewa michoro iliyokamilika kutoka kwa msanifu jengo na kila sehemu ikiwa imeshaainishwa matumizi yake na kazi yake inakuwa inaanzia hapo na kuikamilisha kutokana na uhitaji unaotakiwa.
Sasa tukija kwenye inshu ya matumizi ya A/C, hapa ni sera za kampuni/serikali husika kuhusu matumizi ya umeme majumbani. Kuna baadhi ya nchi vitu kama A/C vinakuwa controlled na utility company mfano: wanawasha na kuzima kwa kila baada ya nusu saa au dakika 45 on, 30 minutes off, hivyo inakuwa rahisi kupunguza matumizi ya umeme yasiyo yalazima na mteja hawezi kuhisi anaonewa au kupunjwa au vinginevyo, lakini kwetu sisi hata kama ndani ilishakuwa kero, bado A/C limewashwa utadhani mtu kalazimishwa.