Nimeiona hii kwenye gazeti la Mwanachi la leo linalohusu 'Dua ya kuombea Bunge inayosomwa kama kasuku.
Dua hii inasema kama hivi:
Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu,Muumba wa Mbingu na Dunia,umeweka katika dunia Serikali za Wanadamu na Mabunge ya Mataifa ili haki ya itendeke.Twakuomba uibariki nchi yetu idumishe uhuru,umoja.haki na amani,umjalie rais wetu hekima,afya njema,na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri,wadumishe utawala bora.Utuongezee hekima na busara sisi wabunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utupe uwezo wa jujadili kwa dhati mambo yatakayoletwa mbele yetu leo,ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na utsawi wa nchi yetu.Amina"
Kwenye sala/dua hii ni nzuri siwezi kukataa wala kupinga,lakini nina maswali kadhaa kuhusu hili:
1.Je Bunge letu linaitendea haki sala au dua hii.
2.Kwanini dua hii isisomwe na wabunge wote ili kila mmoja aweze kuifanyia tafakuri ya kina pale anapoomba au kusali dua/sala hii asubuhi wafunguapo Bunge.
3.Na kwanini sala/dua hii husomwa kwa haraka sana kama vile kuna muda unapotea,yaani kwanini dua hii sifanywe kwa tafakuri ya kina pale inaposaliwa?
Inawezekana hoja hii ilishawahi kuletwa hapa na sikuiona basi naomba mnisamehe,ila ningependa tuitafakari dua hii na kuiomba serikali yetu au Bunge letu liichulie DUA hii kwa moyo na kila mtu ndani ya Bunge awe anaisoma na kuitafakari,ninadhani itabadilisha dhana nzima ya uchangiaji usiona tija,uchangiaji wa mipasho na matusi kwa wabunge wa pande zote mbili.
Karibuni nyote tuijadili.