Tanzania DSE VS Kenya NSE

Tanzania DSE VS Kenya NSE

Bwege2030

Member
Joined
May 10, 2025
Posts
82
Reaction score
152
Tanzania DSE na Kenya NSE .

🎯Uchumi Jumla nchi zote mbili zinaonesha ustahimilivu wa kiuchumi lakini kwa mitazamo tofauti.Tanzania inaonesha misingi imara zaidi ya ukuaji (Strong Fundamentals) ikiwa na makadirio ya ukuaji wa 5.5% - 6.0% na mfumuko wa bei wa chini sana wa 3.1%, jambo linalotoa mazingira tulivu kwa uwekezaji wa muda mrefu. Kwa upande mwingine, Kenya imekumbwa na changamoto za kiuchumi zilizopelekea ukuaji kupungua hadi 4.9% kutokana na ukame na misukosuko ya kisiasa huku mfumuko wa bei ukiwa juu zaidi (4.5%) kuliko Tanzania. Hii inaifanya Tanzania kuwa safe haven kwa wawekezaji wanaokimbia vihatarishi vya kuyumba kwa uchumi.

🎯Sekta ya Fedha

Sekta ya benki nchini Tanzania imepata mabadiliko ya kihistoria kwa kushusha kiwango cha mikopo chechefu (NPL) kutoka 9.3% (2021) hadi 3.3% mwaka 2025, kiwango ambacho ni bora zaidi katika kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara. Sekta hii nchini Tanzania ina ukwasi mkubwa (Liquidity ratio ya 27.7%) na mtaji wa kutosha (Tier 1 ya 18.8%), ikiongozwa na CRDB na NMB ambazo zinadhibiti zaidi ya nusu ya soko.Wakati huo huo, sekta ya benki nchini Kenya inapitia kipindi cha mpito cha kisheria ambapo benki ndogo 10 zinapambana kufikia mtaji wa chini wa KSh 3 Bilioni. Hii inaashiria kuwa wakati sekta ya benki ya Tanzania imetulia na inazalisha faida(ROE ya 25%), sekta ya Kenya inatarajiwa kuingia kwenye mchakato wa kuunganishwa kwa benki ili kunusuru mabenki madogo.

🎯Utendaji wa Masoko ya Mitaji (NSE vs. DSE)

Katika soko la hisa, kuna tofauti kubwa ya tabia ya soko,Soko la Kenya (NSE) limekuwa na "Bull Run" ya ajabu ya 51.1%, ikisukumwa na ongezeko kubwa la thamani ya makampuni makubwa kama Safaricom na KCB, pamoja na mabadiliko ya kimkakati ya kibiashara ni ukuaji wa "Aggressive" ambao unavutia wafanyabiashara wa muda mfupi. Kwa upande wa Tanzania, DSE imekua kwa 29.08%, ukuaji ambao ni wa "Organic" na wa kweli (Value-driven) unaoakisi faida halisi za makampuni bila uvumi mwingi.DSE inategemea zaidi sekta za uzalishaji na benki ambazo hutoa gawio (dividends) la uhakika,tofauti na NSE ambayo inaongozwa zaidi na sekta ya huduma na nishati.

🎯Uchambuzi unaonesha kuwa NSE (Kenya) ni soko la fursa za haraka na ukuaji wa bei (Capital Gains) kwa sasa, lakini lina vihatarishi vikubwa vya kiuchumi na kisiasa lakini DSE ni soko la kimkakati kwa mwekezaji anayetafuta usalama wa mtaji, utulivu wa sarafu, na kipato thabiti cha gawio kutokana na mfumo imara wa benki na udhibiti mzuri wa mfumuko wa bei. Kwa mwekezaji mwenye busara,Tanzania inatoa picha ya soko lenye afya ya muda mrefu (Sustainable Growth), huku Kenya ikitoa picha ya soko lililoamka kwa kasi (Recovery Growth) baada ya kipindi kirefu cha mdororo.
 
Ahsante japo me huaga skeptical na taarfa za kiuchum za bot has ongezeko la mfumuko wa bei. Nawaonaga kama wanafanya siasa tu
 
Back
Top Bottom