RIPOTI: Tanzania yashuka nafasi 12 kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Taarifa ya mwaka 2017 iliyotolewa na Reporters Without Borders(RST) kuhusu World Press Freedom Index inaonyesha Tanzania bado inaongoza katika uhuru wa vyombo vya habari ukilinganisha na nchi nyingine tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki ingawa imeporomoka vibaya kwa nafasi kumi na mbili(12).

Tanzania imeshika nafasi ya 83 na kwa Afrika Mashariki inafuatiwa na Kenya inayoshika nafasi ya 95, Uganda ikishika nafasi ya 112, South Sudan 145, Rwanda inashika nafasi ya 159 huku Burundi ikishika nafasi ya mwisho katika EAC kwa kuwa katika nafasi ya 160 ambayo inajulikana kama black zone/very bad.

Awali, Tanzania ilikuwa katika nafasi hizi:
2016 - nafasi ya 71, 2015 - nafasi ya 75, 2014 - nafasi ya 69, 2013 - nafsi ya 70, 2012 - nafasi ya 34 na 2011 - nafasi ya 41

Screen Shot 2017-06-03 at 10.45.18.png


Kwa Afrika, nchi ya Namibia inaongoza kwa kushika nafasi ya 24 ikifuatiwa na Ghana katika nafasi ya 26 huku South Afrika ikishika nafasi ya 31.

Kwa dunia, nchi ya Norway inaongoza ikifuatiwa na Sweden katika nafasi ya 2, Uingereza inashika nafasi ya 40 huku Marekani ikishika nafasi ya 43. Kwa maana nyingine, nchi za Namibia, Ghana na Afrika Kusini zina uhuru wa kujieleza zaidi ya Uingereza na Marekani.

Kwa maelezo zaidi gonga na usome hapa World Press Freedom Index 2017

reporters.jpg

Reporters Without Borders (RSF) has released the 2017 World Press Freedom Index that shows an increase in the number of countries where media freedom has declined.

A statement from RSF says the World Press Freedom map is getting darker and media freedom is under threat now more than ever. A total of 21 countries are now colored black on the press freedom map because the situation there is classified as “very bad.” Of these, Burundi,s ranked 160th out of 180 in the 2017 Index has been added to the black zone.

In 2015 President Pierre Nkurunziza launched a fierce crackdown against media outlets that covered a coup attempt after his decision to run for a third term. RSF reports that Burundi is now locked in a crisis and media freedom is dying. Charged with supporting the coup, dozens of journalists have fled into exile. For those that remain, the report says, working is almost impossible without toeing the government line.

Another East African country, Tanzania, also saw a decline in media freedoms in 2016. The 2017 index places it in 83rd place, down 12 points from the previous year. This decline is attributed to frequent threats, attacks and arrests of journalists and the heavy hand of President John Magufuli, who according to the report, “tolerates no criticism of himself or his programme”. Additionally, newly passed laws like the Cyber Security Act, the Media Services Act and the Statistics Act criminalise the dissemination of information.

Uganda’s position in the Index has also dropped considerably. It went from 102nd place in 2016 to 112 in the 2017 Index. The RSF report blames this on regular intimidation and violence against journalists, and serious media freedom violations in the 2016 general election.

Neighbouring Kenya remained in 95th place on the Index, but there are concerns about the slow erosion of media freedoms there. The RSF report found that as Kenya prepares for general elections in August 2017, many independent journalists have been the targets of threats and attacks by both the public and the authorities.

Rwanda is the only East African country that had an improvement in its World Press Freedom Index rankings, moving up two points to the 159th place. However censorship and self-censorship are commonplace in Rwanda despite a new media law that was passed in 2010.

SOURCE: Africa Centre for Media Excellence
 
Ukizisikia kelele za ''wanasiasa'' wetu unaweza ukadhani Tanzania niya mwisho katika Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki kwenye eneo la uhuru wa kujieleza kumbe bado ‘’tunapeta’’ pamoja na kudondoka kidogo kutokana na kupitishwa mwaka 2015/2016 kwa sheria za Cybercrimes Act, the Media Services Act and the Statistics Act.

Unamsikia ''mwanasiasa'' anakuambia ‘’Kenya wako mbele kwenye uhuru wa kujieleza ukilinganisha na Tanzania''. ''Tanzania hakuna freedom of expression’’. Blah, blah, blah

Kuna wanasiasa na wanaharakati wako Instagram wanapiga kelele wakidai uhuru wa kujieleza lakini cha kushangaza ukitoa hoja tofauti na mitazamo yao wanakupiga ban kwenye account zao kwa sababu wanadhani uhuru wa kujieleza ni one way traffic.

Kwa repoti hii haishangazi kuona nchi za Magharibi haziwasikilizi wanasiasa wetu kwa sababu zinaufahamu ukweli halisi kuhusu nafasi ya Tanzania katika world press index.

Ama kweli, ukweli hupanda ngazi wakati uwongo hutumia lifti!
 
Ukizisikia kelele za ''wanasiasa'' wetu unaweza ukadhani Tanzania niya mwisho katika Jumuiya ya nchi za Afrika Mahariki kwenye eneo la uhuru wa kujieleza kumbe bado ‘’tunapeta’’ pamoja na kudondoka kidogo kutokana na kupitishwa mwaka 2015/2016 kwa sheria za Cybercrimes Act, the Media Services Act and the Statistics Act.

Unamsikia mwanasiasa anakuambia ‘’Kenya wako mbele kwenye uhuru wa kujieleza ukilinganisha na Tanzania. Tanzania hakuna freedom of expression’’.

Kwa repoti hii haishangazi kuona nchi za Magharibi haziwasikilizi wanasiasa wetu kwa sababu zinaufahamu ukweli halisi kuhusu nafasi ya Tanzania katika world press index.

Ama kweli, ukweli hupanda ngazi wakati uwongo hutumia lifti!
Hasa Tindu Lissu ndo anaongoza kwa Tabia yake mbaya ya kutufanya wajinga kwa kutupa takwimu za umbeya umbeya.
Sijui huwa analenga nini kwa kweli.
 
Hasa Tindu Lissu ndo anaongoza kwa Tabia yake mbaya ya kutufanya wajinga kwa kutupa takwimu za umbeya umbeya.
Sijui huwa analenga nini kwa kweli.
Tundu Lissu ni mwanaharakati.

Moja ya sifa ya mwanaharakati ni kujua kukosoa bila kuwa na solutions.
 
Huwezi kupingananna tafiti, kwa hiyo ripoti tunatakiwa kujisahihisha, sio kisa imeonekana tunaizidi kenya basi tubweteke, angalia, pamoja na kwamba tunaizidi kenya ila kwa mwaka jana tu tumeshuka nafasi 12, huku kenya wakishuka nafasi 2. Hadi mwaka huu unaisha twa mtiririko huo tutakua tumeshuka zaidi ya nafasi 24, kenya watakua na 4, sasa hapo unaweza kuona nani atakua anapoteza zaidi.
 
Huwezi kupingananna tafiti, kwa hiyo ripoti tunatakiwa kujisahihisha, sio kisa imeonekana tunaizidi kenya basi tubweteke, angalia, pamoja na kwamba tunaizidi kenya ila kwa mwaka jana tu tumeshuka nafasi 12, huku kenya wakishuka nafasi 2. Hadi mwaka huu unaisha twa mtiririko huo tutakua tumeshuka zaidi ya nafasi 24, kenya watakua na 4, sasa hapo unaweza kuona nani atakua anapoteza zaidi.
Mkuu;
Ulichokiandika hapa ni logical fallacy!

Huwezi kujenga hoja za kisiasa kama unafanya mahesabu ya namba kwamba 1+1=2 kwa maana hiyo, 1+2 itakuwa ni 3.

Kumbuka Kenya wanaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ambao historia inaonyesha huwa haumaliziki kwa amani kutokana na mgawanyiko wa kikabila.

Tanzania tunaweza kujirekebisha kwa haraka sababu tatizo letu linarekebika kisheria wakati Kenya wana tatizo la kijamii ambalo halimalizwi na sheria pekee.
 
Tatizo kuna baadhi ya watu wameshajitolea tafsiri yao ya UHURU WA KUJIELEZA........

Wao kwao uhuru wa kujieleza ni kukashifu na kutusi watu wengine bila ya kubughudhiwa....huku wao wenyewe wakiwa hawako tayari kusikia maoni ya wengine dhidi yao isipokuwa yale yanayofanana na ya kwao.....
 
Labda Tanzania ya Kusadikika,Kenya kuna mbunge alimtukana Uhuru hadharani na hajafanywa chochote,Ben watch eight kamkosoa Uncle tu lakini mpaka sasa yupo na chatu wa chattle.
Unapingana na utafiti kwa kutumia dhana ya fikra zako pekee?

Kumtukana Rais hadharani haiwezi kubeba taswira nzima ya hali halisi kuhusu uhuru wa kujieleza.

Tukio moja au matatu hayawezi kutoa taswira nzima ya hali halisi.

Hata kwenye ligi ya mpira, timu inayoongoza kwenye ligi ikishindwa mechi moja haina maama kuwa itashuka na kuwa ya mwisho, vivyo hivyo timu inayoshika mkia ikishinda mechi moja haina maana kuwa itapanda na kuongoza ligi.
 
Labda Tanzania ya Kusadikika,Kenya kuna mbunge alimtukana Uhuru hadharani na hajafanywa chochote,Ben watch eight kamkosoa Uncle tu lakini mpaka sasa yupo na chatu wa chattle.
Ah kumbe mnataka uhuru wa kutukana sio kujieleza. Ingekuwa inawezekana bavicha wote wangepelekwa Burundi wakae wiki mbili tu, wakirudi huko wangekuwa na heshima
 
Amefanyia wapi huo utafiti ? Ametumia sample gani ? Amehoji watu wangapi, wa aina ,gani wa umri upi amezingatia gender balance vp ? ,amehoji mikoa mingapi ?
 
Back
Top Bottom