Tanzania daima na Tume ya Mwakyembe Kuongezewa muda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania daima na Tume ya Mwakyembe Kuongezewa muda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kingmairo, Sep 19, 2012.

 1. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 659"]
  [TR]
  [TD] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"] Tume ya Mwakyembe sasa yajiongezea ulaji
  na Mwandishi wetu
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"] TUME iliyoundwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuchunguza viongozi wa bandari waliosimamishwa imeelezwa kugeuzwa mradi maalumu baada ya kuomba kuongezewa muda na kuvuka mipaka ya mamlaka iliyonayo.
  Taarifa za ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Wizara ya Uchukuzi, zinaeleza kwamba tume hiyo iliyoundwa Agosti 24, mwaka huu, ilipewa wiki mbili, ikaongezewa siku kumi na baadaye kuomba siku saba za ziada, huku wakipanua wigo kwa kuwahoji wastaafu wa bandari na wajumbe wa bodi ya mamlaka hiyo.
  Kitendo cha kuhoji wastaafu wa bandari wakiwamo waliowahi kuiongoza, kimeelezwa kuwa ni mkakati wa kulazimisha sababu za kuwakandamiza viongozi wa TPA waliosimamishwa na kuhalalisha kujilipa posho zaidi.
  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tume ya Mwakyembe haina mamlaka ya kumhoji Mwenyekiti wa Bodi ya TPA na hata wajumbe wake, lakini imeelezwa kutaka kulazimisha kwa malengo binafsi.
  “Tayari walishampigia simu mmoja wa wajumbe wa bodi na kumtaka awasaidie kupata mambo mabaya waliyofanya viongozi waliosimamishwa lakini akagoma na kuwaambia hawezi kushiriki kuwaonea watu,” anasema mtoa habari wetu.
  Mwenendo na tabia ya tume hiyo kuwahoji watu wasiohusika una nia ya kutafuta mambo yatakayohalalisha kuwazuia viongozi waliokuwapo TPA wasirudi kazini, huku hali ikizidi kuwa mbaya kiutendaji ndani ya bandari.
  Ofisa mmoja mwandamizi ndani ya serikali alisema ya kuwa hata uongozi mpya wa bandari kwa sasa umeshindwa kufanya kazi kutokana na kuendelea kuwapo makundi ndani ya mamlaka hiyo, huku baadhi ya waliochukua nafasi wakiwa hawana uwezo wala uzoefu katika sekta husika.
  Hayo yamethibitishwa na baadhi ya watendaji wapya wa TPA ambao wamechukua nafasi ya uongozi uliosimamishwa kwa muda ambao wengi wamekiri kutokua na uzoefu na bandari.
  “Hapa bandarini tunashindwa kufanya kazi maana wenzetu hawatupi ushirikiano wowote wakati sisi hata hatuna uzoefu na hatuijui vyema bandari. Hii kazi kwa kweli itatushinda, na ni bora tuwe wakweli tusije kuonekana tumeharibu,” alisema mmoja wa viongozi wapya TPA.
  Kabla ya kuunda tume hiyo, Dk. Mwakyembe aliwasimamisha kazi viongozi wote wa TPA, akiwamo Mkurugenzi Mkuu, Ephraim Mgawe, akiwatuhumu kuhujumu uchumi na kukaidi maagizo ya Ikulu, tuhuma ambazo tume inahaha kuzichimba kila kona, ikiwa ni pamoja na kurubuni baadhi ya watu.
  Baadhi ya tuhuma zilizoelekezwa kwa viongozi waliosimamishwa zimeelezwa kutowahusu kabisa, ikiwa ni pamoja na wizi wa makontena uliotokea katika kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binafsi cha TICTS. Kitengo hicho kimekodishwa na kinashindana kibiashara na TPA ambao sasa wanapokea makontena katika eneo lao.
  Tuhuma nyingine ambazo hadi sasa zinaonekana kama kiini macho, ni tuhuma za wizi wa mafuta, katika eneo la kuingizia mafuta la Kurasini (KOJ), tuhuma ambazo hata polisi wameelezea kutokuwapo wizi kutokana na kutokuwapo kampuni ya mafuta iliyoonyesha kuibiwa.
  Pamoja na kuhusisha bodi ya TPA, imelezwa kwamba baadhi ya wajumbe wa bodi hawaridhishwi na jinsi Dk. Mwakyembe anavyochukua maamuzi yanayoathiri utendaji wa bandari.
  Pamoja na Mgawe, wengine waliosimamishwa kazi ni naibu wakurugenzi wakuu wawili wa TPA waliotajwa kwa majina moja moja ya Mfuko na Koshuma.
  Pia yumo Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng’amilo, Meneja wa Kurasini Oil Jet, Meneja wa KOJ na Terminal Oil Engineer ambao hawakutajwa majina.
  Mwakyembe alimteua Madeni Kipande ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi kukaimu nafasi ya Mgawe
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Source: Tanzania Daima, 19/9/2012
  My take:
  Msisitizo wa Mwandishi huyu ni kamaameshachukua upande Fulani! Kwa kuomba kuongezewa muda kuna tatizo gani? Nikipi bora, tume ifanye kazi bora au ilimradi kazi ifanyike bila kujali ubora? Ameshatoahitimisho kuwa waliosimamishwa tume inatafuta sababu za kuwakandamiza/kuwaonea, yeye amefikiaje hitimisho hilo?Je ni hoja gani alizo nazo kuonyesha kuwa hawana kosa hivyo wataonewa? Kwa kweli media zinahitaji kufahamu nafasi yao katika jamii.
   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Heshima kwako

  Zoezi zima na maamuzi ya Serikali/Mwakyembe ni upuuzi unaodhihirisha udhaifu wa utawala. Kila kitu cha kibiashara kna taratibu zake; kuingia mkenge ni lazima mtu unapoingiza siasa za maji taka kwenye utaalamu. Wamechamba na vidole vyenye kucha lazima wakate kucha kujisafisha.
   
Loading...