hueleweki mkuu. Kinachofanya aonekane msaliti ni kuchapishwa kwa picha hiyo au ni yeye kucheka na mh rais? Maana picha au gazeti linareport event tu!
Lakini kubwa ni kwa nini unaamini si sawa kwa zitto kuongea na kucheka na rais. Tuliona karibu viongozi wote wa cdm walipoenda pale magogoni na kupewa chai wote walionesha tabasabu/kufurahi tu. Sasa hili la zitto ni kwa nini lionekane kuwa ni tatizo? Na kwa gazeti kuchapisha picha hiyo ni kwa nini unaona vibaya...mimi naona kama vile inamjenga zitto kisiasa kwa sababu inaonesha anavyokubalika hata na wapinzani wake (ccm).
Kama utakumbuka hili la kukubalika na wapinzani liliwapa taabu sana washabiki wa jk pale ilipokuwa inaonekana kama vile dr slaa hamkubali, anamkwepa etc. Ilivyotokea mwanya wa dr slaa na jk kukutana sote tunajua picha hizo zilivyopewa umuhimu hata na magazeti ya ccm au pro ccm. Well hili la zitto pengine lipo tofauti kidogo lakini kimsingi sioni tatizo kwa picha hizo kuchapishwa gazeting kama kweli hiyo event ilitokea.
Kama unadhani kuna hoja/agenda nyingine labda utuambie.
yale maneno yamekaa kimbeya kimbeya tu
Hiyo picha haina shida yoyote.Mbona gazeti ninalo na imeandikwa MARAFIKI WA KWELI.Kuna ubaya gani? Mbona sisi huku mtaani CCM na CDM tunaazimana chumvi? Mleta mada analeta uchochezi wa kipumbavu usiyo na maana yoyote.
upo arumeru mkuu? visu, mapnga mshayatupa?
No, kuna kitu hapa hakipo sawa. Si zambi kukutana na na Rais lakini kuna mipaka yake. Hasa ukiwa ni mwanasiasa. David na Ed (both Milband and Balls ) huwa wanakutana kila mara ila sijawahi ona wamepiga picha pamoja (labda washamba na sio wastaarabu). Kuna mpipaka yake kwenye siasa.
Picha ya Zitto na kikwete ina ujumbe ufuatao nao ni kwamba Zitto anamkubari sana Raisi ila watendaji wake ndiyo anaona wana matatizo. Swali kama unaona hivyo na wewe unaipenda nchi kwa nini usiende kumumsaidia?
Najua CDM wanajua kuwa tatizo la nchi hii chanzo ni kikwete na zitto anasema hapana kwa mawazo, maneno na matendo.
Zitto kwa ufupi tu akaokoe jahazi la Raisi ampendaye!
Leo uk wa mbele kuna Picha ya Mh JK akifurahi na Zitto.
Katika picha hiyo Tanzania daima lajidai "Marafiki wa kufa na kufaana"
Malaria Sugu @ WORK
Huyu lazima atakuwa Tuntemeke maandishi yake yamekaa ki ukuda ukuda tu kutaka kuchonganisha watu.