Tanzania bila ushirikina inawezekana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania bila ushirikina inawezekana?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tausi Mzalendo, Feb 12, 2012.

 1. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tanzania tunashika namba katika ushirikina ( utafiti uliwahi kuonyesha na kuletwa JF) Tanzania imo katika tatu bora Afrika tukiwafuatia Benin!
  Ushirikina - kwenda kwa waganga kusafisha nyota, kutafuta dawa za kjupata mali na vyeo, ngekewa, kutabiriwa n.k. ni "moja ya nyenzo" zinazotumiwa na watu mbalimbali katika ngazi zote kusaka mafanikio, ukiacha kufanya kazi kwa bidii na kujituma.

  Kuna viongozi wanasifika kwa kupenda huduma hizo za wataalam.Wakati wa michakato ya kusaka nafasi za uongozi ndio utaona safari za kwenda vituo mbalimbali hasa Bagamoyo zikiongezeka!Cha ajabu, mganga anamsaidia mtu awe tajiri, apate madaraka na mafanikio, ilhali yeye hali yake ni ya kusikitisha kwa jinsi umaskini ulivyomfunika gubi-gubi!

  Maofisini watu wanakamatana na kuhisiana uchawi na hata jambo hilin la aibu liliwahi kutokea bungeni!

  Ni jambo la kusikitisha sana kwamba siku hizi hata wasaidizi wa majumbani ( wasichana wanaolea watoto au kusaidia kazi nao wanatuhumiwa kwa ulozi na ushirikina.Juzi kati, Clouds FM kwenye leo tena walimhoji binti mdogo kutoka Morogoro akaelezea jinsi anavyofanya ushirikina katika nyumba ya mwajiri wake, na jinsi anavyosafiri usiku na mtoto mdogo wa mwajiri hadi Morogoro kushiriki "mikutano ya kichawi"!

  Mara nyingi tunasikia pesa kiasi kikubwa zilitumika katika "kamati za ufundi" - hasa kwenye michezo.Wasanii wa kizazi kipya nao wanatuhumiwa kwa ushirikina. Binti mrembo Aunty Ezekiel anayetuhumiwa kwa kuendekeza uchawi na ushirikina kwenye tasnia ya filamu hakumjung'unya maneno.Alipowekwa ‘mtukati’ , Aunt alimwagia ‘upupu’ wote ambapo alikuwa na haya ya kusema:
  “Kila mtu ana maisha yake hapa duniani ya namna ya kufanikiwa ambayo hayaingiliani na mwezake, yaani kwa mganga waende wao tu, tukienda sisi kwa sababu ni wasanii, basi inakuwa ni ishu?”( soma gazeti la Amani tarehe 2-8 February 2012)

  Watu wanatafuta dawa za kuwazibiti wapenzi wao au hata kuvuta wapenzi!
  Ushahidi wa kutia fora kwa USHIRIKINA ni kuongezeka kwa matangazo ya waganga wakienyeji wakijigamba wanatoka SUMBAWANGA, NIGERIA na kwengineko kwenye kusifika kwa ushirikina!
  Wanafunzi na watu wengine nao wameanza kutegemea ushirikina kushinda.

  Ni wazi kwamba taifa la washirikina litabakia nyuma daima dumu! Ushirikina hupunguza umakini na kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii na kushindanisha vipaji.Watu wengine wanatawaliwa na hofu hata ya kupambana na vinara wa ushirikina na matokeo yake tunajikuta tunabaki na watu wasiotufaa - iwe ni kazini, majumbani, jamii pana n.k.

  Tujiulize, kama USHIRIKINA NI NYENZO kwanini tumeendelea kubaki mikia kwenye kila kitu.
   
 2. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa ushirikina upo sana kwenye ofisi za serikali,unakuta mtu msomi mzuri lakini hafanyi kazi bila kwenda kwa sangoma,
   
 3. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ofisi zinazoongoza kwa ushirikina Bandari,Trc,Idara ya Mahakama,wizara ya maji,Halmashauri zote,
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  talking of a pandora box....
  this is it.......
   
 5. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ushirikina ni kujilazimisha kumuamini mtu atakae toa jibu kwa maswali yalio kosa jibu...
  watu wakielimika watapunguza ushirikina
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni special case aisee kwenye ushirikina..
  mtu ni msomi wa Harvard na ni mshiriikina...
  wasomi wa TZ ni wa aina yake....
  hivi ushirikina unasababisha umasikini au umasikini unapelekea watu kuwa washirikina?????
   
 8. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
 9. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mtu akiwa msomi ila walio mzunguuka wote ni washirikina
  influence yao inakua kubwa na akiwa na personality ndogo anaishia kuamini.
  Nikiongelea kiwango cha education nadhani ni watu wengi sana
  watoke kwenye negative kwenda positive kwa pamoja,
  then in 10, 20 or 30 years utaona tofauti.
  Umasikini unaongeza ushirikina.
  Kuna scientific study ilionesha kua watu wakitoka katika umasikini
  wanapoteza ushirikina na udini sababu wanajitegemea kuliko wanavo tegemea spirits
  (Study ilisema kua Mungu is merely a higher spirit)
  Na ikasema kua uchamungu wa wamarekani unatokana na tofauti kubwa kati ya the rich and poor.
  So mtu kama hajiamini kua anaweza anageukia Mungu au miungu, au mizimu na warozi ili wamuwezeshe.
  Of course I don't agree with them wanapo mlinganisha Mungu na miungu
  ila niliona kuna kaukweli upande wa factors zinazo peleka mtu kua mshirikina.
  Ukitaka nikutumie link niPM. :eyebrows:
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  weka hiyo link hapa itakuwa usefull na uzi huu
   
 11. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hutaki PM? haya... Don't change your mind baadae tena.
  Hapa utapata kitabu chote on Amazon, you will need to buy it in order to read it. Nililazimishwa kusoma part of it.

  Na hii ni summary ndogo ya kitabu by the Shinynickel's review:

  My book is by two social scientists called Pippa Norris and Ronald Inglehart. It's called "Sacred and Secular: Religion and Politics Worldwide". It was published in 2004 and is meticulous and powerful in its interpretation of an enormous range of data. What they're looking at are the data on religious practices in the world today and the extent to which they can be correlated, country by country, with various socioeconomic variables. Now, many books and articles on the state of religion are remarkably data-free, or get muddled in their account of the data, and this one is the antidote.
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  unaweza ni pm kwa mengine lol
  asante kwa link....
   
 13. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  The Boss, kigeu geu. lol
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kigeu geu?
  sio gentleman? lol
   
 15. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Jamani mimi naona uchawi na ushirikina upo kiimani zaidi,yaani kuna watu ambao wanamtegemea mungu na ambao wamechagua kumtegemea shetani (miungu,matambiko na ushirikina). Kila mtu anachagua imani yake ya kuifuata na mara nyingi watu tunapenda majibu ya haraka ya shida zetu hivyo wengi wanaamini ushirikina sababu wanapata majibu ya shida zao haraka ingawa sio moja kwa moja.
  Kwahiyo hoja ya usomi, utajiri au umasikini sioni kama inanguvu hapa ila ni imani ya mtu, ni sawa kama two sides of the same coin kwamba kama unaamini mungu yupo basi na shetani pia yupo.
  Kama watu wanaenda makanisani na misikitini basi pia kuna watu wanaenda kwa waganga, kutambika na kuamini katika ushirikina na pia wao wanaona wanafanikiwa katika maisha yao ya kila siku kama hawa wengine wanaomcha mungu.
   
 16. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama ni hivo mbona sasa (according to TM source) ushirikina ni mkubwa Tanzania na Benin kuliko Rwanda na Kenya (mfano)? ingekua hivo ingeonesha proportions zimefanana duniani kote
  Ila huo utafiti nilinukuu hapo juu unasema kwamba mtu akiwa masikini na hajasoma, kuna uwezekano mkubwa wa kua mshirikina.
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kuna members wengi waliwahi leta research hapa jf
  TZ inaongoza Africa na labda duniani..
   
 18. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Link tafadhali... :A S-coffee:
   
 19. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Kwahiyo study inasema kama mtu anajiamini hawezi kuamini katika mungu wala shetani?

   
 20. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Binadamu tunapokuwa na shida tunageukia imani zetu,sasa na mara nyingi majibu ya mungu yanachelewa ila ushirikina unaona majibu haraka ingawa price yake ni kubwa (makafara na mambo ya ajabu ajabu) sasa haya mataifa yanaamini katika ushirikina kutokana wanaona watu wengi kwenye jamii zao wamefanikiwa kwa njia hizo (wanasiasa na wasomi).
   
Loading...