Dakika kumi zijazo mechi hiyo ya CECAFA (kati ya Tanzania na Kenya) itaanza kuchezwa uwanja wa Taifa wa zamani. Tutawaletea live show (via texts) hapa hapa.
Timu zote sasa ziko kwenye uwanja tayari kukaguliwa. Kenya wakiwa na jezi zao nyeupe ambazo kwa namna moja ama nyingine naweza kuzifananisha na zile za Senegal. Uzi wa Stars ni ule ule tuliouzoea
Umemalizwa kupigwa wimbo wa taifa wa Kenya na sasa unaanza kupigwa wa Tanzania. Wachezaji wa Kenya wanaonekana kuwa na mori wa mchezo. Inashanghaza wa kwetu wamenuna; yawezekana ndiko kuikamia mechi yenyewe
Vilabu vya Tanzania kwa kiwango cha soka kwenye ranks za Afrika Mashariki vinaonekana kuwa juu. Ajabu ni kuwa Taifa Stars ndiyo inalega lega kwenye ranks za Afrika Mashariki.
PENALTI!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.