Tanzania Bara haitakaa iongozwe na anayetoka familia ya Rais. Huku tunaangalia utendaji sio huruma kulinda familia

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana Jf,

Nimesoma thread mbalimbali zikimwonyesha mtoto wa Rais mstaafu kuwa anaandaliwa kuja kuwa Rais wa JMT baada ya kustaafu Magufuri 2025, Rais Magufuri Urais ameupigania kuanzia pale alipochukua form kugimbea ubunge, kwani ndiko alijiandaa mwenyewe kupitia kazi zake alizokuwa anatumwa na wananchi na viobgozi wake kwa kuzifanye zionekane za utendaji safi na usmamizi usio na shaka. Hapa alijihimalisha kwa wananchi na kuleta ushawishi mkubwa kwao.

Kumekuwa na mawazo ya kufanya Urais kama taasis za familia Fulani. Hayo yanawezekana Zanzibar na Kenya tu. Hapa bara hatuna tabia hiyo kwani urais ni nguvu zako mwenyewe hauhitaji mbeleko. Mbeleko tulifanyiwa kwa Ben tu , unaweza kusema Mwlm alikosea lakini yashapita. Urais wa wakati ule ulikuwa wa Mrema ambaye naye aliutengneza kupitia wananchi .
 
Kwenye siasa zetu hizi lolote linaweza kutokea, ushauri utabaki kuwa ushauri.ila wasimamizi wa haya mambo wanayakwao.wanaamua nani awe wapi na yupi awe nani.
 
Kwenye siasa zetu hizi lolote linaweza kutokea, ushauri utabaki kuwa ushauri.ila wasimamizi wa haya mambo wanayakwao.wanaamua nani awe wapi na yupi awe nani.
safari ya 2025 hakuna kuchagua familia ya §mtu, mtu ajitume kufuatana na uwezo wake atii
 
Rais Magufuri Urais ameupigania kuanzia pale alipochukua form kugimbea ubunge, kwani ndiko alijiandaa mwenyewe kupitia kazi zake alizokuwa anatumwa na wananchi na viobgozi wake kwa kuzifanye zionekane za utendaji safi na usmamizi usio na shaka. Hapa alijihimalisha kwa wananchi na kuleta ushawishi mkubwa kwao.
Hii ni kweli kabisa. Magufuli alikuwa smart sana tangu alipokuwa naibu waziri kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya serikali ya awamu ya tatu. Baada ya kuonekana anafanya kazi akapandishwa kuwa waziri kamili tangu mwaka 2000 mpaka 2015 alipogombea na kushinda urais. Japokuwa miaka mitano yake imekuwa na ugumu lakini kuna vitu ambavyo amaevifanya na vinaonekana na anastahili kupewa sifa kwa hilo. Nimechagiza haya kuonesha kwamba Tanzania Bara hatutaki favour ila tunaangalia kazi na output hayo ya famila hatutaki kabisa kuyasikia
 
2025 ndipo lilipo anguko la CCM iwapo wapinzani wakitengeneza msingi October 25 2020
Unaonekana kama utabiri lakini ndio uhalisia wenyewe. CHADEMA walifanikiwa sana uchaguzi wa mwaka 2015 kutokana na msingi walioutengeneza mwaka 2010 Dkt Slaa alipogombea urais na kumtingisha vilivyo Dkt Kikwete
 
Unaonekana kama utabiri lakini ndio uhalisia wenyewe. CHADEMA walifanikiwa sana uchaguzi wa mwaka 2015 kutokana na msingi walioutengeneza mwaka 2010 Dkt Slaa alipogombea urais na kumtingisha vilivyo Dkt Kikwete
ilikuwa patashika JK hakushinda kwa kishindo. kidogo ateleze aliokolewa na kuwa na vyombo vya usalama
 
Back
Top Bottom