Kalalee. Hatuwezi kusovu matatizo ya EWURA kwa post katika JF saa 9 hizi za usiku!
Mkuu wangu kama huna cha Kuuza hbasi huna sababu ya kwenda nje kuomba misaada..Na kiongozi mwenye kuelewa siasa lazima angeenda nje kuomba msingi au niseme mtaji hivyo akijua atawekeza kwenye Umeme na Maji ambao ndio utamwezesha kuzalisha.Mkandara,
uko sahihi, lakini unadhani JK akienda nje kutengeneza masoko, kwa bidhaa zipi? kwa ubora gani? kwa mazingira gani ya production ilhali umeme hakuna? Je, si bora tunge concentrate kuinua viwanda vyetu kwanza, kwa kuhimiza uzalishaji competitive ili bidhaa hizi ziweze kushindana na masoko ya nje?
Chukulia mfano cement tu hapa...production yake inaathiriwa sana na suala la umeme, udhaifu wa shilingi na transport system, kiasi kwamba ikipambana na cement toka nchi za COMESA (hata itoke Egypt) hii yetu inapoteza soko kwa kuwa production costs ni juu.
Ninakubaliana na wewe kila kitu hapo, lakini kuna basic things ilikuwa tuanze navyo then tuvutie wawekezaji au hata kutafuta masoko ya nje. Mimi ninafuatilia sana foreign reserves, ambazo kwa kiwango kikubwa inakuwa boosted na what we export. Mathalan, wakati Mkapa anaondoka 2005, FR ilifikia ya kutosha imports za miezi 8.5, lakini kuna wakati ilishuka hadi miezi 3, why?
Neno uamuzi linachukua maana ndefu zaidi na nitakueleza kwa nini. Aamuzi wa kuingia Ubepari ulikuwa wa maana kwa sababu uchumi wa nchi unatakiwa kuendeshwa na watu binafsi sio serikali isipokuwa huduma za kijamii ambazo serikali inaweka mikataba ya makubaliano na mashirika binafsi ktk utekelezaji wake -Tender.Kwa mawazo yako Mkandara, miaka 20 baada ya ubinafsishaji, je ulikuwa uamuzi wa maana? Na utekelrzaji wake ni wa maana? Nini social welfare ya wafanya kazi na wakulima kwenye ubinafsishaji? Umewanufaisha?
mimi ningeshauri hata viwanda na mashirika yaliyotaifishwa ambayo yameshindwa kufanya kazi yataifishwe tena na safari hii wapewe watu wenye nia na uwezo wa kufanya kazi...
Hivyo basi utaona tatizo lipo kimfumo zaidi, sisi tumewekewa vikwazo vya kupitia walanguzi wa nje kuuza mali zetu na sasa tunapitia tena walanguzi hata kununua mafuta toka nje
Haya Wakuu Mkandara na AK48 Mafuta yamepanda ni Petrol,Diezel na Mafuta ya Taa.Mbalamwezi na utetezi wake EWURA na Project mpya ndio kusema kuwa Jawabu lao imekula kwetu!!!!Maisha ya watu wazima !!!!!!!!!!!!!!!!