Mbalamwezi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2007
- 800
- 171
Nipe muda ntakupa actual prices...mid of next week. Ila, Kwani Augusta alinunua wapi mafuta yale ya January? Halafu si kweli kwamba Addax ilununua magazeti. Kwani nani asiyejua jinsi tunavyoyapeleka mambo TZ. Anayesema ukweli ndo anaambiwa mzushi na muongo ili mradi watu walinde maslahi yao!
Na kaka naamini sote tuna nia njema na Tanzania. Augusta kwani ni ya nani? Sio yule muitaliano aliyekuwa AGIP au Tiper hapa hapa Tanzania anayewakilishwa na ex Addax(Mgoa)?
Halafu standard zetu za kukataa tender ni namna ya kufunga tender document kwenye bahasha???? Well, time will prove us right or wrong. What I suspect ni kuwa hatujui tunachofanya. Tuendelee kushupaa na kujenga haya makampuni makubwa ya nje. Tutakaojililia ni sisi maana hela za kwetu na uwezo wa kujenga kampuni zikawa kubwa pia tunao.Tunaposhindwa ni tamaa zetu na njaa ndogo ndogo tu, however clean we try to convince people that we are.
Mkuu duh, umejuaje kama mimi ni kaka?
Sijui hasa Augusta inamilikiwa na nani. Ila ukiangalia ina anuani ya Swiss, japo unayemtaja anaweza kuwa mwakilishi au shareholder. Sijui alinunua wapi mkuu yale mafuta. Ila ni kweli kuna malalamiko yanachunguzwa, dizaini jamaa kama wanachakachua na ethanol. Next week labda watatoa matokeo ya sampuli zinazopimwa. Ila iliendeshwa kampeni kubwa sana na magazeti mkuu, najua unaifahamu.
Kuonyesha kuwa walikuwa wanafitini, sources za malalamiko zilikuwa zinajificha...na magazeti zaidi ya sita yaliandika stori inayofanana kila kitu. najua uliziona zile mkuu. Unajua ile ni business worth over $100 million a month wakati walipokuwa wanajiagizia wenyewe, sishangai wanatoana macho.
Kuhusu criteria, hayo ni masharti ya tender nyingi tu, na unaweza kuangalia hata kwenye other sources. Ubaya wa tender mkuu, ni kuwa ukikosea masharti hata kiduchu halafu ukapewa tu, upo uwezekano wa wenzako kwenda kublock ushindi mahakamani, na process nzima ikasimamishwa. lazima tukumbuke hilo pia.
La mwisho, cha maana makampuni yalichoomba ni kufungua second window ya prequalification criteria, ambayo itawawezesha hata wenye mitaji midogo hasa wa ndani kushiriki. Kwa sasa requirement ya kuingiza mzigo wa kutosha miezi miwili inawatoa jasho kwa kuwa ni pesa nyingi. Serikali imeanza process ya kulifanya hilo liwezekane soon. Hii ina maana washiriki wa zabuni watakuwa wengi zaidi na premiums zitazidi kushuka na hata pengine kuifikia za Mozambique ($25).