Tanzania awards $500 mln oil supply deal to Swiss firm Augusta; GVT hope will lower prices... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania awards $500 mln oil supply deal to Swiss firm Augusta; GVT hope will lower prices...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wed Nov 30, 2011 7:08am GMT


  * Augusta Energy to supply 540,000 tonnes of oil

  * Govt hopes bulk oil procurement will lower prices

  DAR ES SALAAM Nov 30 (Reuters) - Tanzania has awarded a $500 million contract to a Swiss company, Augusta Energy, to supply 540,000 metric tonnes of oil to the country for the first two months of 2012, a senior official said on Wednesday.


  "The contract awarded to Augusta Energy yesterday marks the introduction in Tanzania of a new bulk procurement system for oil imports," Mansoor Shanif, chairman of state-run oil company, Petroleum Importation Coordinator (PIC), told Reuters.


  Augusta beat bids from four other Swiss-based companies, including Trafigura and Addax & Oryx Group for the contract.


  "The oil that will be imported under this contract covers a period of two months (Jan-Feb 2012). Most of the oil will be sold in Tanzania, while some of it will be for transit purposes," he said.


  Shanif said the state-run oil company would invite fresh bids after the expiry of the two-month contract awarded to the Swiss firm.


  The bulk oil procurement is aimed at lowering fuel prices, which have been partly to blame for a rising inflation rate in the country.


  The year-on-year inflation rate in east Africa's second-biggest economy accelerated for the twelfth straight month in October to 17.9 percent from 16.8 percent a month earlier on rising food and fuel prices.


  Tanzania's energy regulator, EWURA, which imposes fuel cap prices on fuel retailers in the country, said it would introduce a new formula for calculating pump prices after the commencement of the bulk oil procurement.


  Oil importers are the biggest drivers of demand for U.S dollars, putting pressure on the shilling.


  The government said it hopes bulk procurement of oil would ease demand on foreign currency and help to stabilise the local currency.


  Oil imports soared 36.2 percent to $2.6 billion in the year to August 2011, with volumes rising to 3.4 million tonnes from 3.2 million, according to a latest central Bank of Tanzania report.


   
 2. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  What credentials? all purchases are made by special oil supply contracts. Specifications on quality, quantity, tests and measures are all that is required. Payments are released by banks (guarantors) if quality and quantity is met. Quality and quantity are measured by arrangements agreed and on acceptable standards by all involved, seller, buyer, guarantor qualified inspectors and representatives of retailers and end users.
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Huu ni utapeli oil iko kwenye soko la dunia na kufanya Bulk imports haitapunguza bei!!!. Tanzania ina magari yasio zidi million 1 sasa Bulk imports ni kiasi gani?. Vilevile kwasababu soko ni la dunia nzima ni kwanini wauzaji watoe unafuu wakati India, China, USA, Brazil wananunua oil 1000% zaidi ya sisi? kwanini wasiwape discount hao!!. Kitu kingine kwasababu serikali inafanya Bulk imports inasababisha oligopy kwa hiyo kampuni kwasababu haina ushindani? sasa bei itashuka vipi wakati mwingizaji ni mmoja anaweza kutafuta sababu yeyote ya kupandisha bei. Hizi kama tulivyosema mwanzo ni 10% za watu wa serikali tu. Biashara zote za oil na kampuni zipo hapa Houston, TX kwa wasiojua hapa ndiyo Head Qtr ya oil business in the World!!. Huu ni upuuzi tu   
 5. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  @Ribosome...Please. Augusta Energy is a shell company created specifically for earning a commission for the people awarding the contract... lets put it this way. Why not deal with me? I will create a vessel to supply.
   
 6. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  You may have a very important point here Baba Sangara: even a cursory look of their web history goes a long way to show that Augusta Energy is a recent (and possibly fraudulent) start-up, and a virtually unknown entity, in the sense that the company has nothing to show by way of previous, transparent records of activities in other countries in their line of business.
   
 7. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  You may have a very important point here Baba Sangara: even a cursory look at their web history goes a long way to show that Augusta Energy SA is a relatively recent (and possibly fraudulent) start-up, and a virtually unknown entity, in the sense that the company has nothing to show by way of previous, etablished business activities and/or dealings in other countries. Bottomline is, Augusta Energy SA doesn't fit the profile of a company worth winning a $500 million dollar contract.
   
 8. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Wakuu Njabu na Kamundu, heshima kwenu!

  Mfumo huu wa ununuzi si kama serikali "imewazawadia" tu Augusta zabuni ya kuiuzia mafuta Tanzania, bali ni kutokana na kushinda zabuni hiyo ya kimataifa ambamo makampuni mengi yameshiriki lakini yamebwagwa kwa kuwa na bei ya juu. Augusta imeshinda jana kwa mara ya tatu baada ya kuonyesha itaiuzia nchi mafuta kwa wastani wa dola 48.88 kwa tani, wakati mshindi wa pili Addax SA Energy $ 52.85, wa tatu Vito SA $ 53.92, wa nne Trafigura PTE $57.56, wa tano TOTSA $ 57.72, wa sita Reliance Industries $58.82 na wa saba Swiss Singapore $ 67.44.

  Zaidi ya yote, si serikali inayoagiza mafuta haya, bali ni mfumo ulioasisiwa kwa pamoja kati ya serikali na wauza mafuta ili kuwezesha kupatikana kwa mizania bora ya kiuchumi badala ya kila mtu kuagiza mafuta yake kidogo kidogo, wote wanaagiza kwa pamoja kila mtu analipa na mzigo unakuja kwa pamoja.

  Faida kuu ya mfumo huu ni kuwa wenye shida ya mafuta (Tanzania) wanaitangazia dunia kuwa yeyote anayeweza kuwauzia mafuta kwa bei nzuri basi na afanye hivyo...si kweli kwamba ni kutengeneza ukiritimba...tunakokwenda, tutafika mahali ushindani ukikolea tutapata mafuta kwa bei nzuri, maana ushahidi ni ushindani unavyoongezeka sana. Mathalan, kwenye zabuni ya jana, mshindi ameshusha bei toka $67 aliyoiuzia nchi zabuni iliyopita, hadi $48.88. Wengine pia wamejitahidi kushusha lakini si kama Augusta.

  Nawasilisha.
   
 9. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kuangalia idadi ya magari peke yake ili kujua nchi ina mahitaji kiasi gani ya mafuta haitoshi. Angalia gharama za kila mwezi kwenye mtandao wa BoT ili ujue, na pia ikiwa Huko uliko ndo wauza mafuta wa dunia, basi wataweza kushiriki kwenye zabuni ya wazi inayotangazwa Tanzania.

  MKuu, ni vema ukaeleza kinagaubaga namna gani hii haitawezekana, badala ya kutueleza kijumla jumla tuu, nina hamu ya kujua hii inatupeleka wapi.
   
 10. N

  Njaare JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  All in all, tulichotegemea ni mafuta kushuka. Ila toka haya mambo ya bulk procurement yameanza, bei ya mafuta inapaa! Kuna faida gani? Ni afadhali kila kampuni ya mafuta iagize inavyoona inafaa. Kazi ya serikali iwe kudhibiti ubora.
   
 11. I

  Isaiah 54 Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  JAMANI, na mimi nineona vyema kuwaelewesha wenzangu juu ya hii. Mosi historila ya Mfumo wa Uingizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Bulk Oil Procurement) unatokea kwenye Sheria ya Petroli ya Mwaka 2008, Kifungu cha 33 (1) na (2), inasema hakuna mtu yeyote anayeweza kuingiza mafuta hapa nchini ispokuwa : through effecient Procurement. Hivyo basi ukiangalia ununuzi wa huko nyuma ulikuwa ni kinyume cha Sheria kutokana na mambo mengi yaliyokuwamo kama vile kuhamisha gharama (transfrer of pricing) kutoka makampuni mama, ukwepati wa kodi na hata kuingizwa kwa mafuta machafu.
  Tangu January hadi sasa Watanzania wameshuhudia kuongezeka kwa kodi kutokana na kuongezeka kwa mafuta ambayo yanakuja pamoja.

  Kuhusu suala la bei, lazima tuelewe kuwa January mwaka huu pipa lilikuwa likiuzwa dola 100 na sasa hivi tunaenda Aprili, pipa hilo hilo limefika doal 130, lakini usisahahu kushuka kwa thamani ya Shilingi ambako kuanaathiri sana katika upandaji wa bei. Hivyo basi kama mfumo huu usingekuwepo mafuta kwa Dar ingikuwa Sh 2,700/-.
   
 12. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Tatizo letu ni lile lileee....kupenda majibu rahisi rahisi kwa maswali magumu. Unategemea uone bei ya mafuta ishuke wakati soko la dunia yanapanda, hayo mafuta yanatoka Tuyuku?

  Bila shaka, kuna unafuu unaopatikana ukiangalia kiwango ambacho mafuta yanapanda sasa kama ukilinganisha na ambavyo yangepanda kabla ya mfumo huu, wakati kila meli ya mwagizaji ilikuwa inalipa $20,000 kama demmurrage charges wakati kuna foleni ya meli, na meli moja ilikuwa inakaa siku hadi 30, kwa hiyo anayelipia ni mtumiaji wa mwisho.

  Sasa meli moja inapakuwa kwa siku tatu tu...bado huoni unafuu?
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nijuavyo mimi siku zote biashara kubwa za kimataifa kama hii hufanywa kutokana na makubaliano ya kibiashara baina ya serikali yetu (rais) na nchi inayotoa mafuta (rais wao). Kwa mfano tutanunua mafuta Saudia kwa kiasi kadhaa wakati huo huo nao wakinunua mali zetu ktk mabadilishano ya bidhaa na siii mikataba kama hii ya kuzawadia mashirika binafsi. Kazi hiyo itafanywa na Saudia ili kurahisisha na kufuatilia kodi za export ya mafuta yao..

  Nakumbuka vizuri sana wakati wa Nyerere tulikuwa hatuzawadii mashirika binafsi bali ni mikataba baina ya nchi mbili na hii ndio kazi ya IKULU kutafuta uwezekanao wa free trade baina ya nchi mbili.. Haya nayoyaona Bongo ni ya kipekee.. ONLY IN TANZANIA..
   
 14. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkandara mkuu, heshima kwako!

  hii ni zabuni ya kimataifa, ubaya wake uko wapi? unazungumzia wakati wa Nyerere, wakati ule serikali ilikuwa inaendesha uchumi. Tulikuwa na kitu cha ku export ili kuwa na biashara nao kama unavyoeleza. Lakini katika hili, Ni sekta binafsi ndiyo inanunua mafuta kwa wingi, na zabuni inatangazwa kimataifa, unalielewa hili?

  Unapompa Rais madaraka ya kuingia mikataba ya namna hii na suppliers, si ndo tunarudi kule kule? Utawapa nini wenzako ili wakupe mafuta?
   
 15. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mbalamwezi,

  Naona umekuwa hodari wa kujieleza lakini unayosema sio kwenye kwenye biashara ya Mafuta. Record za Tanzania kwa mwaka 2010 est za CIA Factbook Tanzania inatumia 38,000 bbl/day kwa siku wakati USA inatumia 19.15m bbl/day kwa siku kwa mwaka 2010. Sasa kwasababu wauzaji wa mafuta ni walewale hawana sababu ya kuwauzia mafuta kwa bei nafuu hiyo kampuni wakati wauzaji hao hao wana wateja kama USA, China, India na Brazil. Bei yote duniani ya oil ni sawa na inabadilika kila siku. Kitu kingine ni kwamba Tanzania ikianza kuweka Tender ndiyo inaibiwa zaidi maana hakuna mtu anayejua bei itakuwaje mfano mwezi ujao hivyo kampuni zinazofanya biashara za udalali zinafanya kitu kinachoitwa kitaalamu "Hedge" hivyo kama mfano kampuni yangu nafikiri bei haitakuwa zaidi ya $100 kwa bbl naweka bei ya $105 hivyo nategemea kupata faida ya $5 kwa bbl.
  Kama huelewi hivi vitu navyosema hapa ni kwasababu unafahamu biashara ya mafuta ya Tanzania ambayo ni ya kitapeli lakini kwenye soko la dunia kampuni ikukupa bei inamaana wana "Hedge" na bei ya "Hedge" mara nyingi ni ya juu zaidi. Tanzania ingeweza kwenda kwenye soko la dunia na kununua mafuta peke yao kwa bei rahisi kuliko wanazopewa na hizi kampuni huu ni wizi na hizo biashara mnazosema zinafanyika soko gani wakati kampuni zote za mafuta ziko hapa Houston!. Commodity market ambayo inapanga bei ya mafuta ipo Chicago!!   
 16. I

  Isaiah 54 Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndugu yangu, unapotoa data huna haja ya kwenda CIA sasa hebu tukupe uone tunatumia lita ngapi kwa siku hapa nchini excluding transit fuel. Dieseli lita milioni tatu (3,000,000), Petroli lita laki nane na sabini na tano (875,000), Mafuta ya Taa lita laki sita na nusu (650,000). Inaonekana unajua kidogo biashara ya Petroli, kwa kuwa umetumia neno Hedging lakini matumizi yake hayafanyiki katika biashara hiyo hapa nchini na kukuonesha kuna ushindani angalia jinsi kampuni zilivyoshinda jana kwa mujibu wa Petroleum Importation Cordinator (PIC) jana.
  Company Diesel Petrol Jet/Kero Weighted Average
  Total 59.82 54.33 51.38 57.7182
  Reliance 60.47 54.52 65.38 58.82
  Addax 58.08 41.41 56.53 56.43
  Swiss Sing. 67.75 65.93 73.21 67.44
  Vitol 59.75 40.45 62.95 53.924
  Augusta 54.68 36.18 53.18 48.886
  Trafiggura 57.55 50.90 75.75 56.327

  Compared to thepremium that we are currently having, that were quoted by Augusta in the secondTender (Diesel 64.97, Petrol 74.67 and Jet 59.67 : Weighted average 67.58). Mjadala wote huu ni kutokana na kutoelewa hali halisi ya jambo lenyewe, tatizo ni SHILINGI YENU KUPOROMOKA pambana kujenga uchumi.
   
 17. I

  Isaiah 54 Member

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MANUFAA YALIYOPATIKANA KWA KUANZISHA MFUMO WA UAGIZAJI MAFUTA KWA PAMOJA

  Manufaa ambayo yameanza kupatikana kutokana na mfumo ambayoyamethibitika katika kipindi cha miezi miwili ya uagizaji mafuta wa pamoja na:

  1.
  Kupunguakwa Msongamano wa Meli Bandarini

  Siku za ucheleweshaji wameli katika Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kutoka siku kati ya 40 na 60zilizokuwa zinadaiwa na makampuni na hata siku15 ambazo ziliruhusiwa kwenye kanuniya ukokotoaji wa bei ya mafuta hadi kufikia wastani wa siku 4 kutokana nautaratibu maalum wa kuingiza meli bandarini tofauti na zamani kabla ya mfumohuu. Hii ni sawa na asilimia 74 ya ongezeko la ufanisi katika kupokea mafuta.

  2.
  Takwimusahihi za ujazo wa mafuta yanayoingizwa nchini

  Serikali inaweza kujua kiasisahihi kinachoingizwa nchini au kiasi kinachotarajiwa kuingizwa nchini kwa sikuza usoni, na hivyo kuweza kupanga mipango sahihi ya kiuchumi kwa faida ya nchikwa ujumla. Aidha, mfumo umerahisisha katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.Takwimu zilizopo zinaonesha kuongezeka kwa kiasi cha mafuta kinachoingia nchinikama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 5 kwa kulinganisha kipindi cha sasa nakipindi kama hiki kwa mwaka mwaka wa fedha 2010/2011.
  Jedwali Na. 5 Mlinganisho wa ujazo wa mafuta yanayoingizwanchini

  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 436"]
  [TR]
  [TD="width: 93"]Mwezi[/TD]
  [TD="width: 151"]Mwaka wa Fedha 2011/2012[/TD]
  [TD="width: 152"]Mwaka wa Fedha 2010/2012[/TD]
  [TD="width: 186"]Asilimia ya Ongezeko/ Pungufu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 93, bgcolor: transparent"]Januari[/TD]
  [TD="width: 151, bgcolor: transparent"] 168,189,555 [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"] 216,391,302 [/TD]
  [TD="width: 186, bgcolor: transparent"]-22%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 93, bgcolor: transparent"]Februari[/TD]
  [TD="width: 151, bgcolor: transparent"] 244,523,240 [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"] 165,870,575 [/TD]
  [TD="width: 186, bgcolor: transparent"]47%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 93, bgcolor: transparent"]Jumla[/TD]
  [TD="width: 151, bgcolor: transparent"]412,712,795[/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]382,261,877[/TD]
  [TD="width: 186, bgcolor: transparent"]8%[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  3.
  Ongezekola Kodi kwa Serikali

  Moja ya mikakati ya Serikali ni kuongeza kodi hivyopamoja na mambo mengine, kuanzishwa kwa mfumo huu kulilenga kuongeza kodi natayari matunda yameanza kuonekana kama inavyoonyesha kwenye tawkimu za hapo juuambao kumekuowa na ongezeko la mafuta kwa asilimia 47. Ongezeko hililinahusisha pia kuongezeka kwa kodi.

  4. Udhibitiwa upungufu wa mafuta yanayopotea wakati wa usafirishaji

  Upotevu wa mafuta (ocean loss) wakati wa kuyasafirisha kutokabandari moja hadi nyingine ni jambo la kawaida katika tasnia ya biashara yamafuta. Kumekuwa na udhibiti wa upungufu wa mafuta yanayopotea wakatiyanaposafirishwa kuja nchini. Hiiinatokana na kwamba kwa sasa zinatumika takwimu halisi ya mafuta yaliyopoteabadala ya makadirio kwa utaratibu wa zamani

  .
  5. Kupunguakwa bei ya mafuta hapa nchini

  Mfumo huu umefanikishakudhibiti ongezeko la bei kubwa zaidi ambalo lingekuwepo kama mafutayasingeletwa kwa kupitia mfumo huu. Madhalani gharama ya ucheleweshaji wa MeliBandarini (Damurage cost ni dola za Marekani 30,000 kwa siku na mfumo huuumepunguza ucheleweshaji kutoka siku 15 hadi siku nne. Hii ingeingia kwenye gharama kwa mlaji. Bei zilizopo sasa badozimedhibitiwa na mfumo huu ambao unapoanza Janurai pipa moja lilikuwa linauzwadola 100 na sasa linauzwa dola 125.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu hivi unajua uongozi wa nchi ama unazungumza uchumi wa machinga!.. Ubaya wake ni kwamba tunaponunua mafuta toka shirika hili sisi hatupati kitu... inatakiwa tukinunua mafuta yao sisi pia tunawauzia mali zetu hivyo mabadilishano yanakuwa baina ya chumi mbili na sio upande mmoja tu wahitaji yaani iinakuwa two way traffic ya kibiashara kama ilivyokuwa barter system of exchange na sii swala la serikali kufahnya biashara bali mashirika yenu ndio yatakayopata soko.. Sio kazi ya wananchi kutafuta masoko ya bidhaa zetu bali serikali inatafuta masoko hayo..Ndio maana unawaona viongozi wakitembelea nchi nyingine kujenga makubaliano ya kibishara..

  Kama leo tunaagiza mafuta ya Billioni 500 wakati huo huo Saudia nao watanunua mali yetu ya thamani hiyo hiyo ama karibu na hiyo inaondoa kazi na gharama ya sisi kuuza mali zetu ili kulipia mafuta hayo (Partner trade balance by country). Kwa mfano tuna ushirikiano na nchi za EU ambao walikuwa wakinunua samaki wetu Sangara, kwa makubaliano na serikali yetu lakini waliokuwa wakisafirisha samaki hao ni mashirika binafsi sio serikali. Mbona serikali ilihusika ktk hilo? Hiyo kampuni ya Swiss wao wanachimba mafuta? au watatuuzia ili kuongeza hesabu yao ktk soko huria (wallstreet) kama maagent wa mafuta hali haitusaidii kitu chochote.

  Hivi sasa tunachukua mafuta ya Billioni 500 hatujui tutapata wapi fedha za kulipia mafuta hayo kama sii tunachota toka mfuko wa Taifa wakati bidhaa zetu zinakosa soko, yaani tunachouza leo ktk mafuta ndicho kitakwenda kulipia gharama? hii sii biahsara ya machinga au vitu feki toka China wanayoifanya wajarisiamali wetu na mikopo ya benki!. Hakuna kitu Free market mkuu wangu kwa tafsiri ya tender, Marekani inanunua mafuta toka nchi kibao kwa mikataba baina yake na nchi hizo na ndio maana wamepiga marufuku kukununua mafuta ya Syria au Iran na sii maamuzi ya mashirika binafsi au tender zilizoshinda. Leo hii Marekani wananunua mafuta ya Canada wakati huo huo Canada pia inalazimika kununua vitu vyake toka Marekani iwe magari au parts, hakuna cash transactions. Bado mnafikiria sana Kijamaa na elimu ya vitabuni, lakini ni jukumu la serikali kuandaa mazingira ya chumi ya nchi husika.
   
 19. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kamundu, hapa tunajadiliana. Ukianza ku note eti "naona umekuwa hodari wa kujieleza" ni statement za kitoto zinazoonyesha namna ulivyo...kama kawaida, dont attack personality, jenga hoja za msingi. Kuwa USA hakukufanyi ujue kila kitu hadi udharau wengine. Kama ungekuwa unajua unachoongea nadhani usingeleta makisio ya CIA tena ya mwaka 2010.

  Lengo la majadiliano haya ni kupeana elimu na wala si kuwatisha watu wakuone unajua sana bada ya kuwaeleza unachojua.

  Muundo uliopo, labda nifafanue kuwa anayeshinda zabuni anakupa bei ya Premium kwa maana ya Freight na Insurance. Bei halisi ya mafuta itakuwa determined na soko wakati huo atakapokuwa akikuletea, na wala si kwamba anakuwa amekupa bei ya mafuta kwa ku "hedge" kama unavyotaka tuelewe.

  Hata Mkuu Mkandara unaposema haya yanatokea Tanzania tu, ni kwa kuwa hujui kuwa Mozambique, Malawi, Kenya, Namibia Ghana etc wanatumia mfumo kama huu. Na Rwanda, Burundi na Zambia pia wanaonyesha interest ya kutumia mfumo huu pia.  Kwa muundo wa Tanzania ulivyo, unadhani ni namna gani hasa nchi inaweza kupata mafuta kwa bei rahisi, nieleza kwa ufasaha bila kubabaisha. Hii itanisaidia mimi na wengine kujua,
   
 20. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu, nimecheka sana hii hofu yako. Hizi ni fedha wanazotoa Oil Marketing companies kwa mahitaji yao ya muda huo, na wala si serikali. Ni kwamba, badala ya wao kununua mmoja mmoja, sasa wameform kampuni inayokusanya mahitaji yao na kutangaza zabuni kwa ajili ya kuwaletea. Nitakutafutia literature proper nikutumie, ilimradi usiwe mvivu wa kusoma. Nitapenda u argue ukiwa na full knowledge.
   
Loading...