Tanzania au Tanganyika?

Tanzania au Tanganyika?

Tanganyika ndo njia kuu, hii Tanzania ni mchepuko tu!!!!!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums app

kwa nini mkuu? Unaweza kushare na sisi sababu zinazokifanya uone kuwa ikitokea hivyo basi turejee kwenye Tanganyika?
 
Mimi nimesoma nimeona katoa maoni yake kuwa anapendekeza kama tutavunja muungano Tanganyika iendelee kuitwa Tanzania tena katoa na sababu kuwa yeye alizaliwa wakati wa Tanzania pamoja na kizazi kikubwa cha aina yake

Mdau hajakosea. Wakati anatuma post yake nilikuwa sijaweka sababu zangu.
 
Tanganyika kwa sababu ndogo tu moja kwamba mfumo mzima wa sheria na taasisi zake unatumia jina hilo, mfano TLS.
 
UKAWA, kikundi haramu, kazi yao ni kuombea tu watu wagawanyike, ili yumkini wao wapate madaraka! Wakati dunia inaelekea kuwa kijiji kimoja, UKAWA wako busy kugawanya nchi!

Samahani mkuu. Ukawa wameingiaje kwenye hii mada?
 
Tanganyika kwa sababu ndogo tu moja kwamba mfumo mzima wa sheria na taasisi zake unatumia jina hilo, mfano TLS.

Kuna ugumu gani kiasi kwamba si rahisi kubadilisha sheria?
 
Kuna ugumu gani kiasi kwamba si rahisi kubadilisha sheria?

Kipi rahisi na kipi kigumu kati ya kubadilisha mfumo mzima wa sheria kuanzia ngazi ya chini hadi juu ama kubadili jina toka Tanzania kuja Tanganyika?
 
Kipi rahisi na kipi kigumu kati ya kubadilisha mfumo mzima wa sheria kuanzia ngazi ya chini hadi juu ama kubadili jina toka Tanzania kuja Tanganyika?

Kwa sababu mimi siyo mwanasheria, ndiyo maana nikaomba kufahamishwa ugumu uliopo katika kubadilisha mfumo mzima wa sheria unaotumia neno Tanganyika ili tutumie Tanzania. Ila naamini katika mabadiliko hayo, kazi haitakuwa kubadili muktadha wa sheria bali neno moja tu la "Tanganyika" kuwa "Tanzania".

Hata hivyo naomba wadau wa sheria wanisaidie ukiwemo wewe,.....sheria tunazotumia sasa ni za Tanganyika au Tanzania?
 
Tanganyika mkuu ni jina letu la asili. Hii Tanganyika zamani ijulikana Kama Mrima, na baadae Tanganyika, sasa Tanzania bara. Kurudi nyuma si Kosa,na kisheria Tanganyika ndiyo nchi halisi iliyoungana na Zanzibar kuzaa TZ. Tanzania ni jina la kufikirika . Muungano ukikoma halina tena uhalali. Wazanzibari watanyofoa ZAN katika jina hili . Historia inajieza wazi kuwa TZ imezaliwa 1964 baada ya muungano
Nawkilisha.
 
Tanganyika ndo njia kuu, hii Tanzania ni mchepuko tu!!!!!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums app

Nakubaliana na wewe kwa 100%. Wanaokataa Tanganyika ni sawa na akina Kalumanzira aliyetaka kuitwa "Bulaza K" eti Kalumanzira limakaa kishamba shamba.

Kuna nchi zilizo achana na majina ya wakoloni zikatunga ya kwao kama Zambia iliitwa North Rhodesia, Zimbabwe iliitwa South Rhodesia, Burkina Faso (Burkina) iliitwa Upper Volta, Congo Kinshansa iliitwa Zaire lakini wakarudia jina lao la Congo (DRC), Malawi iliitwa Nyasaland. Pia kuna nchi zilizo kuwa zimeungana lakini muungano ulivyovunjia zikarudia majina yao ya awali kama Senegambia (Senegal na Gambia), Czechoslovakia (Czech na Slovakia), USSR (Russia, Ukraine, Azerbaijan, Belarus nk).

Kwa hiyo si ajabu Tanzania ikivunjia tukirudia Tanganyika kwa sababu ni jina halisi la Nchi yetu. Hii kusema ni la kishamba ni ujinga tu kwani hata TANU ilivyoungana na ASP ilikuwa ngumu kuingia akilini "Chama Cha Mapinduzi", lakini limezoeleka na linaonekana kama la kawaida lakini TANU ilikuwa mpango mzima katika kulitamka.

Sisi tu watanganyika labda tutafute jina jingine kama walivyofanya nchi zingine.
 
Tanganyika mkuu ni jina letu la asili. Hii Tanganyika zamani ijulikana Kama Mrima, na baadae Tanganyika, sasa Tanzania bara. Kurudi nyuma si Kosa,na kisheria Tanganyika ndiyo nchi halisi iliyoungana na Zanzibar kuzaa TZ. Tanzania ni jina la kufikirika . Muungano ukikoma halina tena uhalali. Wazanzibari watanyofoa ZAN katika jina hili . Historia inajieza wazi kuwa TZ imezaliwa 1964 baada ya muungano
Nawkilisha.

Kwenye post yangu ya kwanza nimeweka assumption kwamba Wazanzibar wanaweza kutokuwa na na tatizo kwa sababu hata sasa hawatumii jina linalowakutanisha na Tanzania. Yaani hawaitwi Tanzania visiwani kama ambavyo wengi wangetemea iwe. Kama mazingira hayo, unadhani Wazanzibar watakuwa na tatizo gani endapo bara watabaki na jina la Tanzania?
 
Back
Top Bottom