Mwaka wa uchaguzi huu maneno matamu matamu yatakuwepo mengi tu. Kwa ukuaji wa sekta ipi growth itarebound na kufikia 5.7% ?
Fukuto la kutetereka kwa uchumi wa dunia ndio kwanza tumeanza kulisikia na bado halijaonyesha makali yake kisawasawa. Huko kwenye makampuni ya mawasiliano mnawapigia makelele,
kwenye usafirishaji mnazidi kujifisadi na mabarabara hayako sawa,
mafuriko ya December/January bado gharama zake hazijajulikana,
kilimo cha kutegemea mvua isiyo na ratiba,
utalii unaododa,
gharama za uchaguzi,
kushindwa kwa TRA kufikia malengo ya ukusaji kwa robo ya tatu consecutively sasa (i think, it could be more),
Gharama zinazopanda kila leo za nishati na irregularity ya supply yake,
mishahara duni ya wafanyakazi,
lundo la kodi kwa wazalishaji wanaofuata sheria na taratibu,
Dhahama nchi jirani,
uvivu wetu etc.
Hapa kitakachofanyika NBS watacheza na weighting ya some of the goods in the CPI basket. Najua weighting ya chakula itashuka mpaka kwenye asilimia 44 au 45, halafu tutakuja kupewa takwimu za kupikwa.