Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imeshughulikia kwa haraka hitilafu ndogo iliyotokea katika eneo la barabara ya mchepuko la Daraja la Somanga Mtama, na kwa sasa barabara hiyo inapitika kama kawaida.
Asubuhi ya leo Machi 24, 2025 majira ya saa 12:30, maji kutoka milima ya Kitumbi na Kinjumbi yalipita katika eneo la barabara ya mchepuko na kusababisha mojawapo ya makalvati kushuka chini, hali iliyokatisha sehemu ya barabara hiyo kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Fredy Sanga, baada ya kupata taarifa hiyo, TANROADS ilimtaarifu mara moja mkandarasi ambaye yuko katika eneo la ujenzi, na kazi ya kurejesha mawasiliano ilianza mara moja.
“Kwa sasa eneo hilo limeimarishwa na linapitika kama kawaida. Tumefanya kazi kwa haraka ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kutumia barabara hii bila usumbufu,” alisema Mhandisi Sanga.
Naye Diwani wa Kata ya Somanga, Said Bakari, amethibitisha kuwa wahandisi waliwasili kwa haraka na kurekebisha changamoto hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Daraja la Somanga Mtama, lenye urefu wa mita 60, linatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2025. Mpaka sasa, piles (nguzo za msingi za daraja) 16 kati ya 43 zimeshachimbiwa, na kazi inaendelea kwa kasi.
mwaka 2006 nakiwa chuo nilipita hapa,hali ilikuwa hivi hivi na madai yakawa Mkapa amemuachia JK amalizie hapo.
kaondoka JK,kaja JPM ,sasa Samia,Somanga bado ni habari ile ile,LEO tarehe 06/04/2025 habari imerudi tena,MAWASILIANO YA DAR NA MTWARA YAMEKATIKA.