Tano Bora ya Vita kubwa zaidi zilizowahi kutokea duniani

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,539
4,672
1.World war II
Vita hii iliyotokea kati ya 1939 na 1945. Ndio vita iliyopelekea vifo vingi zaidi katika historia ya dunia. Zaidi ya watu mil 70 walidhurika(vifo na ulemavu).
Vita hii ilihusisha mataifa makubwa yote duniani na ni vita pekee ambapo bomu la nyuklia lilitumika pale Marekani walipoipiga miji miwili ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki.

Tukio kubwa zaidi kweny vita hii ni lile la mauaji ya waisrael zaid ya mil 6 lilofanywa na kikund cha Nazi kilichokuwa kikiongozwa na Adolf Hitler.
Vita ya pili ya dunia ilipelekea hali ya siasa ya dunia kubadilika kabisa na kuundwa kwa umoja wa mataifa,UN.

2.Mongol conquests
Hii ni vita iliyopiganwa mwanzoni mwa karne ya 13, Himaya ya Mongol ilichukua 20% ya eneo la dunia, himaya hii ilikuwa ikienea Asia na Ulaya Mashariki. Machafuko haya yalipelekea vifo vya watu mil 60 mpaka 70, inakadiriwa zaid ya wachina laki moja walijiua wenyewe kabla ya Mongolians kufika eneo lao.

3.World war I
Vita hii ilipiganwa kati ya 1914 na 1918, ilisababish vifo vya watu mil 17. Vita hii pia ilibadilisha mwenendo wa kisiasa wa dunia pia kupelekea kuundwa kwa League of Nations.

4.The Manchu conquest of China
Vita hii ilikuwa kati ya Qing dynasty na Ming dynasty. Ilipiganwa karne ya 17 na ilichukua miaka 60 kuisha. Ilipelekea vifo vya watu milion 25, kikundi cha Qing dynasty kiliibuka na ushindi na kupelekea kuiongoza China mpaka mwanzoni wa miaka ya 1900 pale Jamhuri ya watu wa China ilipoundwa.

5.Napoleonic wars
Vita hii iliyochangiwa na mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789, ilikuwa ni vita iliyotangazwa na mataifa ya Ulaya yaliyopinga utawala wa Napoleonic Ufaransa. Ufaransa lilikuwa taifa kubwa baada ya Napoleon kutwaa sehemu kubwa ya Ulaya. Mpaka baada ya kupigwa na Urusi 1812 mapigano yaliyosababisha mauaji ya watu mil 6 na nusu.
 
Ongeza Six Days war ya 1967 baina ya Israeli na Arabic alliance,ambayo nchi zaidi ya tano mashariki ya kati zilibafuliwa na Israel,zikiongozwa na Ijipti
Asante kwa kuongeza nyama
 
Ujazungumzia vita vya ulaya vilivyochukua miaka thelathini katika zama za Giza. Kati ya waprotestant na ukatoriki. Hapo utapata sababu ya wazungu weñgi kukimbilia marekani. Maana kabla yao ilikuwa na wahindi wekundu tu.

Ila overall vita vikubwa na vya kudumu dunia nzima ni kati ya WEMA na UOVU. Na sasa tunaelekea kileleni kwa vita hii iliyodumu miaka zaidi ya 6000
 
Ujazungumzia vita vya ulaya vilivyochukua miaka thelasini katika zama za Giza. Kati ya waprotestant na ukatoriki. Hapo utapata sababu ya wazungu weñgi kukimbilia marekani. Maana kabla yao ilikuwa na wahindi wekundu tu.

Ila overall vita vikubwa na vya kudumu dunia nzima ni kati ya WEMA na UOVU. Na sasa tunaelekea kileleni kwa vita hii iliyodumu miaka zaidi ya 6000
Aisee
 
Mm naona vita iliyouwa watu wengi ni vita kati ya marekana na waislamu. Ukianzia kule Afghanstan,Iraq,Libya,Syria.
 
Duuh vita ya Kagera hakuna, na ya Savimbi na Serikali ya Angola?
 
hv kwa nn hii propaganda ya israel kuwa waliuwawa milion 6 mbona kimahesabu aikubali leo wapo c zaid ya milion 15 hyo idadi ya kufa milion 6 tena miaka ya 40 imetoka wapi? napataga wsws sana na swala hili
Hv hawa.israel.hawakutapakaa.dunia nzima kweli
Germany walikuwepo
Ufaransa walikuwepo
Mistri walikuwepo na.place zingine.kibao

So.hata leo wakihesabiwa wote japa dunia hao jamaa n.weng sana....

Kuna.jamaa anasema.ukiona kuna.mahali kuna.ugunduz wowote wa ajabu ajabu ujuwe kuna damu hz jamaa,mbaya zaid hata waishi mbali na.kwao miaka.nenda ludi..huwa hawajisahau kuwa yy si.myahudi,nahisi
 
Conspirancy za wazungu hizo, wala hawataki kusemea mauaji makibwa zaid ya kutisha kwa wakongo yaliyofanywa nashenzi king leopad II wa belgium huko kongo zaire
 
hv kwa nn hii propaganda ya israel kuwa waliuwawa milion 6 mbona kimahesabu aikubali leo wapo c zaid ya milion 15 hyo idadi ya kufa milion 6 tena miaka ya 40 imetoka wapi? napataga wsws sana na swala hili
First thing first tofautisha Waisraeli na Wayahudi.

Hitler hakuua Waisraeli. Israeli kama nchi imekuja 1948 baada ya Hitler kushindwa vita.
 
6 day war ya Israel against Arab world hii ndo ilikua vita ya kibabe sasa
 
hv kwa nn hii propaganda ya israel kuwa waliuwawa milion 6 mbona kimahesabu aikubali leo wapo c zaid ya milion 15 hyo idadi ya kufa milion 6 tena miaka ya 40 imetoka wapi? napataga wsws sana na swala hili
Waisrael waliopo kwao ndio wanaweza kuwa 15mil kwa idadi hao waliouawa walikuwa ni wakazi wa nchi ya German.
 
Back
Top Bottom