Tani 13 za dawa za kulevya zakamatwa na watuhumiwa 4983 Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Dar es salaam.

Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya hapa Nchini limefanikiwa kukamata tani 13 .717 za dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 4987 katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa kitengo cha kuzuia nakupambana na dawa za kulevya Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP. Amon Kakwale amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni 2023, ambapo kitengo hicho cha kuzua na kupambana na dawa za kulevya kilifanikiwa kukamata kiasi cha Kilogramu 9,358.77 sawa na Tani 9.36 za dawa za kulevya aina ya Bhangi.

Ameongeza kuwa tani 4.357 za Mirungi, kilogramu 1.86 za Heroin pamoja na gramu 220.05 za Cocaine zilikamatwa na ekari 105.25 za mashamba ya bhangi na mirungi yaliteketezwa.

Katika hatua nyingine ACP Kakwale amesema Operesheni hiyo ilifanikiwa kukamata watuhumiwa 4983 ambapo kesi 3784 zilifunguliwa na kesi hizo zipo katika hatua mbalimbali Mahakamani.

Mkuu huyo ametoa onyo kali kwa wanaoendelea kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kuacha mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wakijihusisha na vitendo hivyo.
IMG-20230729-WA0011.jpg
IMG-20230729-WA0013.jpg
IMG-20230729-WA0010.jpg
IMG-20230729-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom