Tangu Media iuawe, haijafufuka bado

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,489
40,999
Bila shaka yeyote, sote tunafahamu kuwa sekta ya habari iliuawa wakati wa awamu ya 5, awamu ya uongozi wa marehemu Magufuli.

Tulibakia na media bandia, ambayo kazi yake haikuwa kuhabarisha na kufundisha bali kusifia Serikali na Rais.

Kazi ya kutafuta habari za kweli likawa jukumu la kila mtu kwa namna anavyojua, na kwa vyanzo anavyovijua. Vyombo vya habari vikawa vimepoteza nafasi ya kuaminika, huwezi kuwa na uhakika kinachotangazwa ndivyo kilivyo au kinatangazwa kwa namna ile ambayo watawala wanataka.

Kwa sasa, japo hakujaonekana wazi, uhuru wa habari kubanwa, lakini mazingira hayajabadilika kwa kiasi kikubwa kwa sababu sheria zile gandamizi, sheria za kidikteta bado zipo vile vile kama ambavyo aliziweka marehemu Magufuli kwa dhamira ya kuua uhuru wa vyombo vya habari na kuvikomoa kama havitaki kuendana na matakwa ya watawala.

Leo hii tungekuwa na vyombo vya habari vilivyo huru, vyenye watu wenye weledi na dhamira njema, bila shaka daima tungekuwa na taarifa sahihi katika mambo mengi, kama vinavyofanya vyombo vya habari vya mataifa mengine. Mathalani tungekuwa tayari tuna rating ya uongozi wa Samia, kwa kulinganisha na wakati alipoyachukua madaraka, tungeweza kutambua mambo gani yamempandisha au kumshusha katika utawala wake kwa kuzingatia maoni na fikra za watu anaowaongoza.

Sahizi kuna uchaguzi unaosubiriwa wa Spika, lazima tungekuwa na rating ya wananchi juu ya wagombea mbalimbali wanaotaka kuchaguliwa kuwa spika wa Bunge. Lakini media ipo kimya, ipo vile vile, mara nyingini imebakia kuokoteza habari za DC wa wilaya fulani amesema nini, RC wa mkoa fulani amesafiri kwenda wapi, Waziri fulani leo amekuwa mgeni rasmi kwenye tukio gani, Waziri Mkuu ameona wapi rundo la takataka, n.k. - petty issues ndizo wanazohangaika nazo.

Jamii iliyo duni, watu wake huhangaika na vitu vidogo vidogo kuliko mambo muhimu na makubwa. Rais ataenda kufungua kisima ili tu asikike, Waziri mkuu au Makamu wa Rais ataenda na msururu wa watu kwenda kukagua takataka, Mkuu wa mkoa ataenda kufungua matundu ya vyoo vya shule, Spika ataenda kushiriki sherehe ya vikoba na msururu wa wanahabari, wananchi siku nzima badala ya kuongelea mambo makubwa ya kitaifa, wanabaki wanahangaika na kusifia viongozi hata kwa mambo ambayo ni wajibu wa kawaida wa kiongozi yeyote, polisi watabaki wanafikiria wamfuatilie na kumbambikia kesi nani kwa sababu ameikosoa Serikali au Rais.

Katika jamii yetu, wengi wamefunga mkataba na ujinga, unafiki, uwongo na ulaghai. Lakini, hata tukiwa wachache namna gani, ni muhimu daima tusimame katika ukweli, tukemee unafiki, tukemee siasa za kukomoana, n.k., kuna siku hata hawa wajinga wa leo watabadilika.

Viongozi wetu wengi ni wanafiki, waongo, hawana weledi ni kwa sababu sisi jamii tunayoongozwa tumewalea. Lakini laiti sisi jamii na vyombo vya habari, tukabadilika na kusimama katika ukweli (japo kuna gharama, hasa unapokuwa katika jamii yenye mifumo primitive ya uongozi kama hii yetu) ukweli daima, tungeondokana kabisa na hawa viongozi wanafiki, wanaotafuta sifa kwenye mambo madogo madogo, tungeondokana na utawala duni kabisa wa jeshi la polisi lililogeuzwa na kufanya kazi kama idara ya CCM ili kuhakikisha primitivity ya CCM inabakia kuwa ndiyo ultimate power.

Tusisite kuusema ukweli daima. Vyombo vya habari, badilikeni.
 
Timu gaidi mnateseka sana na awamu ya 5 lakini kutwa kutumia flyover, ndege na zahanati za awamu hiyo
 
Hongera kwa makala nzuri! Ni kweli tasnia ya habari ilikuwa inakuwa vizuri baada ya ujio wa vyama vingi kwenye mid 1990s mpaka Magufuli alipovuruga kwa kuua wakosoaji, kuwafungulia makosa ya kutakatisha fedha na wengine kuwafungia vyombo vyao kupitia sheria haramu za Cyber, Huduma za Habari na Takwimu.

Kwenye hotuba yake ya kwanza akiapishwa Rais Samia mnamo 19/03/2021 alitamka kuwa magazeti yafunguliwe, wananchi waikosoe Serikali kwa mujibu wa sheria. Akasisitiza na kesi za kubambikizwa zifutwe. Akakemea Kodi za DHULUMA zikusanywazo na TRA, na kuikemea TAKUKURU na Polisi kwa kuwanyanyasa watu bila makosa.

Kweli tukaanza kuona nuru mpya baada ya siku chache. Ikawa kama ni kupindua kabisa mambo ya ukatili na uuaji ambayo yalitamalaki wakati wa Magufuli. Kwa Mara ya kwanza tukasikia kauli ya "Mama anauoiga mwingi".

Kesi ya Akwilina ikapinduliwa na Mahakama ya Rufaa, yule Mdude CHADEMA wa Mbozi maarufu kwa matusi naye akashinda kesi, Ole Sabaya akatiwa nguvuni na Akaunti za Mbowe zikaachiliwa.

Mara tukaanza kusikia kauli za matusi kwenye mikutano ya CHADEMA. Mfano ni ile kauli ya Mdude siku 4 tu baada ya kuachiwa alisikika akiongea Jukwaani Barracuda Tabata kuwa "Mwambieni huyo Mama yenu, nitamnyoa kwa wembe uleule niliotumia kumnyoa mtangulizi wake"

Alitamka maneno mbele ya Mbowe na viongozi wengine wa CDM na hawakumchukulia hatua mpaka leo.

Kwa mtazamo wangu Serikali imeona pengine bado hatuna busara katika kutumia uhuru wa maoni. Tunaleta matusi badala ya kutoa maoni.
 
Back
Top Bottom