Tangu asubuhi leo mitandao ya simu(voda, airtel, tigo) Mwanza na internet havifanyi kazi, kunani?

mxyo16

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
1,243
758
Au ni sababu za kiusalama. Mtuhabarishe wateja wenu, shuguli zetu za kujiingizia vipato zinakwama kutokana na hali hii. Si upande wetu tu walipa kodi, hata huyo mkusanya kodi pato litapungua.
 
Siku hizi kuna material risk kubwa kwa kuwa minara mingi hapo inamilikiwa na kampuni moja inaitwa Helios towers...
 
Mie nakumbuka vijana wa mjini walikua wanapata tender kujenga hii minara na wakitamka kabisa nimepata tender kujenga minara ya voda au tigo etc... ikawaje tena huku mwanza iwe ya helios peke yao...
...sijui kwa wengine ila kwetu sie kazi zinaharibika.
 
Ni kweli. Hiyo minara Tigo na Voda wamewauzia hawa Wamarekani... Ni sawa na wewe unaweza ukakanunua ka Vitz kako huku Dar, kufika Mwanza ukamuuzia mtu mwingine...
 
Kwasasa mitandao ipo hewani, ila bado sijaelewa kama sababu ni hao helios au mkonge wa taifa huko buhongwa.....
 
Au ni sababu za kiusalama. Mtuhabarishe wateja wenu, shuguli zetu za kujiingizia vipato zinakwama kutokana na hali hii. Si upande wetu tu walipa kodi, hata huyo mkusanya kodi pato litapungua.

Leo sijui kuna nini. Ila naona Halotel wapo vizuri.
 
Tayari mtandao umerudi ila wanatakiwa kutuomba radhi.Tangu muda wa saa tano mtandao haupo hapa Mwanza.
 
Back
Top Bottom